afyatips
TATIZO LA MWANAMKE KUPATA HEDHI MARA MBILI KWA MWEZI
MWANAMKE KUPATA HEDHI MARA MBILI KWA MWEZI
Kupata hedhi mara mbili ndani ya mwezi mmoja kunaweza kutokea ikiwa mzunguko wa hedhi ni mfupi (chini ya siku 21–24), lakini pia inaweza kuwa ishara ya tatizo la kiafya linalohitaji uchunguzi.
Moja ya vitu ambavyo mwanamke hutakiwa kuvizingatia sana ni kuhusu mzunguko wake wa hedhi, Mzunguko wa hedhi huweza kumpa mwanamke kila aina ya ishara hata pale akiwa ni mgonjwa,kupitia mzunguko wa hedhi mwanamke anaweza kujua ana tatizo flani.
Mizunguko ya hedhi ipo tofauti kwa wanawake mbali mbali, Lakini kuna migawanyiko mikuu mitatu kwa kuangalia mda wa mzunguko wa hedhi yaani;
(i) Kuna mzunguko wa hedhi mfupi mfano; siku 21
(ii) Kuna Mzunguko wa hedhi wa wastani au kawaida wa siku 28
(iii) Na kuna Mzunguko wa hedhi mrefu mfano; siku 35
Lakini kuna mizunguko ya aina mbili kwa kuangalia mabadiliko ya mzunguko wa hedhi yaani;
(i) Kuna mzunguko usio badilika badilika au kwa kitaalam hujulikana kama REGULAR MENSTRUAL CYLCE
(ii) Na kuna mzunguko unaobadilika badilika yaani kwa kitaalam hujulikana kama IRREGULAR MENSTRUAL CYCLE
Takwimu
- Mzunguko wa kawaida wa hedhi kwa wanawake wengi ni siku 21–35. Ikiwa hedhi inakuja chini ya siku 21 kati ya hedhi moja na nyingine, huonekana kama hedhi mara mbili kwa mwezi.
- Tafiti zinaonyesha kuwa hadi asilimia 25 ya wanawake wanaweza kupata hedhi zisizo za kawaida katika kipindi fulani cha maisha yao.
SABABU ZA MWANAMKE KUPATA HEDHI MARA MBILI AU ZAIDI NDANI YA MWEZI MMOJA NI PAMOJA NA;
1. Kuwa na tatizo la Mvurugiko wa vichocheo mwilini ambalo kwa kitaalam hujulikana kama Hormone imbalance.
2. Matumizi ya baadhi ya njia za uzazi wa mpango ambazo zina vichocheo kama progestrone na estrogen Mfano,Sindano,au vipandikizi(Vijiti).
3. Mwanamke kubadilisha mazingira au hali ya hewa,Mfano; kutoka sehemu moja ambayo amekaa kwa mda mrefu na kwenda sehemu nyingine ambayo hajawahi kukaa kabsa.
4. Mwanamke Kuwa na tatizo la uvimbe kwenye kizazi
5. Mwanamke kufanya kazi ngumu kupita kiasi
6. Pia mwanamke akifanya sana mazoezi ya mwili kupita kiasi huweza kupatwa na tatizo hili
Kuna baadhi ya wanawake hupata period mara mbili au zaidi kwa mwezi ambayo huambatana na maumivu makali sana ya tumbo hadi wengine kufikia hatua ya kulazwa kabsa hosptal.
Chanzo/Sababu Kuu kwa Kifupi
- Mabadiliko ya homoni mwilini.
- Msongo wa mawazo (stress).
- Ugonjwa kama polycystic ovarian syndrome(PCOS).
- Tatizo la tezi ya shingoni (thyroid gland).
- Uvimbe kwenye kizazi (fibroids).
- Polyps kwenye mfuko wa uzazi.
- Maambukizi ya mfumo wa uzazi.
- Matumizi au kubadilisha njia za uzazi wa mpango.
- Tatizo la Endometriosis.
- Kuwa Karibu na kipindi cha kukoma hedhi (perimenopause).
KUMBUKA; Ukiona shida hii ni vizuri kukutana na wataalam wa afya ili kujua chanzo cha tatizo lako kwani hata magonjwa hatari kama uvimbe kwenye kizazi huweza kuwa na dalili kama hizi pia,hivo usipuuzie tatizo hili.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
Dalili za Kumwona Daktari Haraka
- Kutokwa damu nyingi sana.
- Hedhi kudumu zaidi ya siku 7.
- Maumivu makali ya tumbo au nyonga.
- Kizunguzungu, uchovu mkubwa au kupungukiwa damu.
- Kutokwa damu kati ya hedhi mara kwa mara.
Mwisho: Hedhi mara mbili kwa mwezi inaweza kusababishwa na mabadiliko ya kawaida ya homoni, lakini pia inaweza kuashiria tatizo kama PCOS, fibroids au ugonjwa wa tezi. Ikiwa hali hii inaendelea kwa miezi kadhaa au inaambatana na maumivu makali na damu nyingi, ni muhimu kumwona daktari wa wanawake.
Vyanzo(Links used):
Cleveland Clinic: https://my.clevelandclinic.org/health/diseases/14633-abnormal-menstruation-periods
Mayo Clinic Health System: https://www.mayoclinichealthsystem.org/hometown-health/speaking-of-health/why-are-my-periods-so-irregular-heavy-and-painful
Healthline: https://www.healthline.com/health/womens-health/two-periods-in-one-month
Wikipedia (Menstrual cycle): https://en.wikipedia.org/wiki/Menstrual_cycle
Office on Women’s Health (U.S.): https://www.womenshealth.gov/menstrual-cycle
NIKID (U.S. NIH): https://www.nichd.nih.gov/health/topics/menstruation



.webp)