Aliyekuwa Mke wa Trump,Vanessa Trump agundulika ugonjwa wa Saratani ya Matiti

Aliyekuwa mke wa Donald Trump Jr, Vanessa Trump, amethibitisha kuwa amegundulika na ugonjwa wa saratani ya matiti baada ya kushirikisha taarifa hiyo kupitia mitandao ya kijamii.

Kupitia ujumbe wake wa Instagram, Vanessa alisema hakutarajia kupata taarifa hiyo ya kushtua, lakini kwa sasa ameanza kushirikiana kwa karibu na madaktari wake ili kupanga matibabu yatakayomsaidia kupambana na ugonjwa huo.

“Nisingetarajia kupata habari kama hizi, lakini ninaendelea kufanya kazi na timu yangu ya kitabibu kupanga hatua za matibabu,” aliandika Vanessa katika ujumbe wake.

Vanessa alifafanua kuwa tayari amefanyiwa utaratibu wa kitabibu mapema wiki hii na sasa anaendelea na hatua za mwanzo za matibabu huku akiomba apewe faragha ili aweze kuzingatia afya yake na safari ya uponaji.

Aidha, alisema nguvu kubwa anayoipata kwa sasa inatokana na msaada wa familia yake, watoto wake pamoja na watu wake wa karibu ambao wameendelea kuwa naye katika kipindi hiki kigumu.

Vanessa na Donald Trump Jr walifunga ndoa mwaka 2005 katika makazi ya kifahari ya Mar-a-Lago kabla ya kutengana rasmi mwaka 2018. Wawili hao wana watoto watano pamoja.

Baada ya taarifa hiyo kusambaa, Vanessa amepokea jumbe nyingi za faraja na maombi kutoka kwa mashabiki, marafiki pamoja na watu maarufu, akiwemo Ivanka Trump ambaye alimtakia afya njema na nguvu katika kipindi hiki cha matibabu.

Kwa mujibu wa wataalamu wa afya duniani, saratani ya matiti ni miongoni mwa magonjwa yanayoathiri wanawake wengi zaidi, lakini kugundulika mapema kunaongeza nafasi kubwa ya mafanikio katika matibabu na uponaji.

Kwa sasa, Vanessa ameendelea kusisitiza umuhimu wa faragha wakati akiendelea na matibabu yake na kuomba watu kumuombea katika kipindi hiki kigumu cha maisha yake.

...See more

1 Comments

  1. Wakati mwingine sio rahisi kupokea Taarifa kama hii halafu usipate mshtuko wa hali ya juu, Mana unajikuta upo normal tu! du!

    ReplyDelete

Post a Comment

Related Discussions...