Makombora 15 kutoka Iran yapiga Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE)
Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), imesema imekumbwa na shambulio jipya kutoka Iran lililohusisha makombora 15 pamoja na ndege zisizo na rubani (droni), katika tukio linaloendelea kuongeza mvutano katika eneo la Ghuba.
Kwa mujibu wa wizara ya ulinzi ya UAE, shambulio hilo lilijumuisha makombora 12 ya balistiki, makombora matatu ya cruise pamoja na droni nne. Watu watatu waliripotiwa kujeruhiwa kufuatia tukio hilo.
UAE inasema mifumo yake ya ulinzi ilifanikiwa kudhibiti sehemu kubwa ya mashambulizi hayo kutoka Iran
Taarifa hiyo imeongeza kuwa mifumo ya ulinzi wa anga ya nchi hiyo imekuwa ikikabiliana na mashambulizi hayo tangu kuanza kwa mgogoro wa Marekani na Iran Februari 28, ikidai kuwa imezuia jumla ya makombora 549 ya balistiki, makombora 29 ya cruise na zaidi ya droni 2,260. Via BBC
...See more





Post a Comment
Related Discussions...