Connect with us

Ugonjwa wa kwashakoo,chanzo,dalili na Tiba

Doctor Ombeni

Published

on

Ugonjwa wa kwashakoo,chanzo,dalili na Tiba

• Kwashakoo ni Ugonjwa gani?

Kwashakoo ni ugonjwa unaohusisha upungufu mkubwa wa protini mwilini,

Ugonjwa wa kwashakoo kwa kiasi kikubwa huathiri watoto wadogo, watoto ambao wapo kwenye mazingira ambayo hawapati mlo wenye virutubisho vya kutosha ikiwemo proteins,

Watu wenye kwashakoo wanaweza kuwa na chakula cha kula, lakini hakina protini ya kutosha.

Dalili za Ugonjwa wa Kwashakoo

Dalili za ugonjwa wa Kwashakoo ni Pamoja na;

1. Ukuaji duni kwa watoto au Mtoto kudumaa

2. Kuvimba kwenye vifundo vya miguu na miguu kwa ujumla

3. Kuvimba Tumbo au tumbo kujaa

4. Kuwa na mabadiliko mbali mbali kwenye nywele ikiwemo;

  • Nywele kukauka sana,
  • Nywele kunyonyoka au kupoteza nywele
  • Nywele kupoteza rangi yake. n.k

5. Kuwa na Ugonjwa wa ngozi(dermatitis)- tatizo ambalo huhusisha ngozi kuwa kavu,ngozi kubanduka, ngozi kuwa na magamba au mabaka mekundu.

6. Kuongezeka ukubwa au kuvimba kwa Ini, kama dalili ya ugonjwa ambao kitaalam hujulikana kama “fatty liver disease”.

7. Misuli kupungua na kuwa dhaifu lakini mafuta huhifadhiwa chini ya ngozi (subcutaneous fat).

8. Kuwa na dalili za tatizo la Upungufu wa maji mwilini(Dehydration).

9. Kukosa hamu ya chakula(anorexia).

10. Mwili kuchoka kuliko kawaida n.k

Madhara ya Ugonjwa wa Kwashakoo

Madhara ya Ugonjwa wa Kwashakoo ni pamoja na;

– Kusababisha udumavu kwenye ukuaji wa watoto(watoto kudumaa)

– Kusababisha tatizo la kuwa na kiwango kidogo cha sukari kwenye damu(Hypoglycemia).

– Kusababisha tatizo la joto la mwili kushuka zaidi-Hypothermia (low body temperature).

– Kusababisha kiwango cha ujazo wa damu kuwa chini-Hypovolemia (low blood volume), kisha kupelekea matatizo kama vile hypovolemic shock.

– kusababisha tatizo la Electrolyte imbalances hasa kutokana na upungufu wa maji mwilini.

– Kusababisha kinga ya mwili kuwa dhaifu sana, hali ambayo husababisha mwili kushambuliwa na magonjwa mara kwa mara pamoja na vidonda kuchelewa kupona pale unapopata vidonda.

– Kupata Matatizo kweye Ini ikiwemo;

  • tatizo la Cirrhosis
  • Au Ini kushindwa kufanya kazi(liver failure).

– Kudhoofika  kwa kongosho, hali ambayo huweza kusababisha matatizo mbali mbali kwenye umeng’enyaji wa chakula

– Na Wakati mwingine kusababisha Kifo

Chanzo cha Ugonjwa wa Kwashakoo

Kwashakoo ni ugonjwa unaohusisha upungufu mkubwa wa protini mwilini, hivo chanzo kikubwa cha Ugonjwa wa kwashakoo ni upungufu wa Protini mwilini,

Sababu za msingi zinazohusiana na kwashiorkor ni pamoja na:

• Mtu kula vyakula vyenye Wanga nyingi, Katika idadi ya watu ambayo inachukuliwa kuwa kwenye hatari zaidi, haswa maeneo ya Afrika, Amerika ya Kati na Asia ya Kusini-Mashariki, mara nyingi chakula kinachopatikana ni aina ya wanga kama vile:

  • mchele,
  • mahindi
  • au mboga za wanga.

Mazao haya yanaelekea kuwa ya bei nafuu na hupatikana kwa wingi kuliko vyakula vyenye protini nyingi, hasa katika maeneo ya vijijini ambako wengi ni wakulima. Akina mama ambao hawana protini ya kutosha mwilini wanaweza kupitisha tatizo hili la upungufu wa protini kwa watoto wao.

• Kuachishwa kunyonya na kusababisha mtoto kukosa virutubisho vya kutosha. Jina “kwashiorkor” linatokana na lugha ya Ga ya Ghana-Afrika, Ikimaanisha “Ugonjwa ambao mtoto anapata wakati mtoto mpya(mwingine) anakuja.”

Hii inaelezea hali ya kawaida ambayo mtoto anayenyonyeshwa anaachishwa haraka ili mtoto mchanga aanze kunyonyeshwa.

Kwa sababu ya uhaba wa rasilimali au kutojua lishe vizuri, au vyote viwli, mtoto anayeachishwa kunyonya hapati lishe ya kutosha, hali ambayo huathiri afya yake,kupelekea ukosefu mkubwa wa virutubisho muhimu kama vile Proteins,kisha kupata magonjwa kama vile Kwashakoo.

• Sababu zingine zinazoweza kuchangia kuwepo kwa Ugonjwa wa kwashakoo ni pamoja na;

  1. Ukosefu wa Virutubisho muhimu kama vile vitamins na madini mwilini
  2. Ukosefu wa Lishe yenye antioxidants.
  3. Aflatoxins – sumu kutoka kwa ukungu ambayo kwa kawaida hukua kwenye mazao katika hali ya hewa ya joto na unyevunyevu.
  4. Uwepo wa vimelea vya magonjwa aina ya Parasites pamoja na magonjwa kama vile; surua, malaria na HIV.
  5. Pamoja na Matatizo mengine mbali mbali ya kimaisha, ikiwa ni pamoja na njaa, vita na majanga ya asili pia huweza kuchangia uwepo wa Ugonjwa wa Kwashakoo.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

✚

Ushauri,Elimu,Tiba

Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)

🏆Certified| Doctor from Afyaclass. Maudhui haya ni kwa ajili ya elimu ya jumla ya afya. Unapohitaji ushauri wa kina, uchunguzi, au matibabu binafsi, wasiliana na daktari kupitia namba:+255758286584.Pia tufwatilie kupitia: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Guest Avatar

LATEST POSTS

Afya News18 hours ago

Serikali yaimarisha huduma za Lishe kupunguza madhara ya Utapiamlo

Serikali yaimarisha huduma za Lishe kupunguza madhara ya Utapiamlo Na Shaban Juma, WAF – Dodoma Serikali inaendelea kuimarisha huduma za...

Utafiti19 hours ago

Teknolojia ya Upimaji wa Vinasaba Iliyosaidia Kugundua COVID-19 Sasa Inasaidia Madaktari Kuokoa Maisha

Maendeleo ya sayansi na teknolojia katika sekta ya afya yamewezesha wataalamu kugundua magonjwa kwa usahihi zaidi, hata pale ambapo vipimo...

Saratani21 hours ago

Saratani ya Utumbo mpana ni Saratani inayoongezeka kwa kasi

Saratani ya Utumbo mpana ni Saratani inayoongezeka kwa kasi kwa hivi sasa,Mfano takwimu za hivi karibuni zinaonyesha;Saratani ya utumbo mpana...

Stars Health2 days ago

Hali ya Papa Leo XIV imeendelea kuimarika baada ya upasuaji wa mapafu

Papa Leo XIV anaendelea kuimarika baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye pafu. Vatican yasema alikuwa na usiku mtulivu...

Ebola1 day ago

Ugonjwa wa Ebola: Jinsi Ujerumani inavyowafundisha wahudumu WA afya kupambana na mlipuko wa Ebola

Ugonjwa wa Ebola ni miongoni mwa magonjwa hatari ya kuambukiza yanayosababishwa na virusi. Ugonjwa huu unaweza kusababisha homa kali, kutokwa...

WHO2 days ago

Sumu ya Madini ya Risasi: WHO yaonya kuhusu madhara yake kwa watoto na watu wazima

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa wito kwa nchi mbalimbali kuimarisha hatua za kuzuia watu kuathiriwa na sumu ya madini...

EVENTS2 days ago

Siku ya Kunawa Mikono Duniani, Leo, tarehe 15 Oktoba 2026

Siku ya Kunawa Mikono Duniani, Leo, tarehe 15 Oktoba 2026 Leo, tarehe 15 Oktoba 2026, Tanzania inaungana na nchi nyingine...

magonjwa ya wanawake2 days ago

Mashavu ya Uke Kuwasha,sababu, dalili na Matibabu yake

Kuwashwa kwa mashavu ya uke ni tatizo linaloweza kumpata mwanamke katika umri tofauti. Tatizo hili linaweza kuathiri mashavu ya nje...

Ebola2 days ago

Kenya yathibitisha mgonjwa wa pili wa Ebola,ugonjwa wa Ebola aina ya Bundibugyo

Kenya imethibitisha kisa cha pili cha ugonjwa wa Ebola aina ya Bundibugyo, huku mamlaka za afya zikieleza kuwa mgonjwa huyo...

Afya News2 days ago

Vifo vya Wajawazito barani Afrika mada hii imeibuka tena

Tatizo la wajawazito kupoteza maisha kwa kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua, limetajwa katika mkutano wa kanda wa kuimarisha...