Afyaclass Bongo Social DALILI ZA MAWE KWENYE FIGO

 MAWE YA FIGO

••••••••


DALILI ZA MAWE KWENYE FIGO


Tatizo hili kwa Kitaalam hujulikana kama Kidney Stones,ambapo watu wengi wanapata tatizo hili na pia wengi wao hawafahamu hata Dalili moja ya ugonjwa huu wa kuwepo kwa Mawe kwenye Figo yaani Kidney stones kwa kitaalam.



Dalili za mawe kwenye Figo ni Pamoja na;

- Kupata homa ambacho hiki ni kiashiria kwa magonjwa mengi kwamba ndani ya mwili kuna shida.

- Kupata maumivu wakati wa kukojoa na pia kukojoa Mkojo mdogo sanaa

- Mkojo wa mgonjwa wa tatizo hili hunuka sana

- Kupata shida ya kukojoa ndani ya mda mfupi kidogo kidogo

- Kukojoa mkojo wenye rangi ya tofauti kama vile; kahawia,nyekundu au pink

- Mgonjwa kupata maumivu makali chini ya kitovu mara kwa mara,na wakati mwingine maumivu huwa makali wakati wa kukojoa

- Kupata shida ya Mgongo kuuma sana


Uchunguzi ni muhim kabla ya kunywa Dawa yoyote,ili kugundua kwanza chanzo sahihi cha tatizo, na ili uweze kupata tiba sahihi.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





You, Mehreen and others
Hashtag:

WEKA MAONI HAPA(Reply)

Notification
Karibu Afyaclass Bongo Social Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Bongo Social ASANTE.
UNDERSTOOD