Ugonjwa wa tb unasababishwa na nini
Ugonjwa wa Tb au Kifua kikuu,ambapo kwa kitaalamu Zaidi hujulikana kama TUBERCULOSIS ni ugonjwa wa kuambukiza ambao husababishwa na maambukizi ya bacteria kwenye maeneo kama vile kwenye Mapafu.
Bakteria anayesababisha Ugonjwa huu wa kifua kikuu hujulikana kama mycobacterium tuberculosis. Kifua kikuu kinaweza kuambukiza wanyama pia kama vile ng'ombe n.k,
Ikiwa Mnyama kama Ng'ombe ana maambukizi haya, bacteria wa kifua kikuu wanaweza pia kutoka kwenye ng'ombe na kupitishwa kwenda kwa binadamu kwa njia mbali mbali ikiwemo kupitia maziwa yaliyoambukizwa.
➖ Ugonjwa wa Kifua kikuu kwa kawaida huenea kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia nyingi ikiwemo wakati mtu mwenye Ugonjwa huu anapopiga chafya, kukohoa au kutema mate. Kutoka kwenye mapafu, bakteria hawa wanaweza kuenea pia kwenye sehemu zingine za mwili na kusababisha kifua Kikuu,
Haya hapa ni baadhi ya Maeneo ambapo Bacteria wa Kifua kikuu huweza kuathiri mbali na Mapafu;
- Figo
- Ini.
- Ubongo na Uti wa Mgongo, bacteria hawa huweza kushambulia Kwenye Majimaji yanayozunguka ubongo pamoja na uti wa mgongo.
- Misuli ya moyo.
- Sehemu za siri.
- Kwenye lymph nodes.
- Kwenye Mifupa
- Joints
- Kwenye Ngozi.
- Kwenye damu, hapa nazungumzia kwenye Kuta za mishipa ya damu.
- Kwenye koo,eneo la Kisanduku cha sauti(voicebox) pia huitwa larynx
Dalili za Ugonjwa wa TB,Kifua kikuu
Dalili za Ugonjwa wa TB ni pamoja na hizi;
(1) Kupumua kwa shida sana
(2) kuwa na kikohozi kinachoendelea, kinachoambatana na makohozi yenye damu
(3) Pia homa za usiku huibuka.
(4) Kuanza kupungua uzito kwa kasi sana
(5) kupoteza rangi halisi ya Ngozi,
(6) mwili kukosa nguvu au kuwa dhaifu.
(7) Mwili kukonda sana baaada ya Kupata Ugonjwa wa kifua kikuu au TB
(8) Mwili kutoa sana Jasho hasa wakati wa Usku n.k
🔺KAMA UNA TATIZO HILI LA UGONJWA WA KIFUA KIKUU AU TB/TUBERCULOSIS NI BORA KWENDA HOSPTAL NA KUKUTANA NA WATAALAM WA AFYA WA BOBEZI KATIKA ENEO HILI ILI KUPATA TIBA SAHIHI NA SALAMA KWAKO.
ILA KWA USHAURI ZAIDI/ELIMU/TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584