Afyaclass Bongo Social Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa tayari amewasili katika viwanja vya Shule ya Sekondari Katesh kuaga miili ya waliofariki kwa mafuriko

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa leo Disemba 4, 2023 tayari amewasili katika viwanja vya Shule ya Sekondari Katesh katika Wilaya ya Hanang kwa ajili ya kuongoza shughuli ya kuaga miili ya marehemu 49 waliofariki kwenye mafuriko.

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ameongozana na Mawaziri wengine katika shughuri hiyo ya kuaga wapendwa wetu akiwemo Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel, Viongozi na Watendaji wengine wa Serikali na wananchi wa Hanang katika kutoa pole za dhati kufuatia maafa ya mafuriko hayo.

You, Mehreen and others
Hashtag:

WEKA MAONI HAPA(Reply)

Notification
Karibu Afyaclass Bongo Social Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Bongo Social ASANTE.
UNDERSTOOD