Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia leo Novemba 8, 2025 imewatangazia Wanafunzi wote wa elimu ya juu na ya kati kuwa Vyuo Vikuu na Vyuo vya kati Nchini vitafungukiwa kuanzia Novemba 17, 2025.
Hayo yamebainishwa kupitia taarifa rasmi iliyotolewa na Wizara ambapo imeeleza kuwa kwa mujibu wa kalenda ya mwaka wa masomo 2025/2026 mwaka wa kwanza wataanza kuripoti Novemba 17 ili kushiriki programu ya utangulizi (Orientation Day) na Wanafunzi wanaoendelea watarejea Vyuoni Novemba 24, 2025.
“Wanafunzi wa mwaka wa kwanza wanatakiwa kufika vyuoni kuanza Program ya Utangulizi (Orientation Program) kuanzia Novemba 17, 2025 kabla ya kuanza masomo rasmi, Wanafunzi wanao endelea watarejea Vyuoni kuanza rasmi masomo kwanzia Novemba 25, 2025.”
“Aidha Wizara inawahimiza Wanafunzi wote kufika vyuoni kwa wakati kufuata ratiba zilizopangwa na kushiriki kikamilifu katika shughuli za kitaaluma” imeeleza taarifa hiyo.





.jpeg)



image quote pre code