Head

  POVU

• • • • •

KUTOKWA NA POVU UKENI WAKATI WA KUFANYA MAPENZI(je ni tatizo?)

Swali hili nimeulizwa na watu wengi sana, leo nimeamua kulitolea ufafanuzi katika makala hii,

SWALI; JE KUTOKWA NA POVU UKENI WAKATI WA KUFANYA MAPENZI NI TATIZO? NA KAMA NI TATIZO NI TATIZO GANI?

MAJIBU; Kabla ya kutoa majibu unachotakiwa kujua ni kwamba, mazingira ya ukeni katika hali ya kawaida hutakiwa kuwa na unyevuunyevu na sio makavu, yanatakiwa kuwa na ute ute au utelezi n.k

Na kudhihirisha hilo, katika uke wa mwanamke kuna Tezi maalum ambalo huhusika na kazi ya kuleta hali ya unyevuunyevu ukeni pamoja na hali ya utelezi au ute ute. Tezi hili hujulikana kwa kitaalam kama Bartholin's glands

SASA BASI, endapo mwanaume akishiriki tendo la ndoa na mwanamke, kutokana na msuguano wa hapa na pale, ndyo sababu kubwa ya kusababisha Povu kutokea ukeni, ambapo chanzo chake ni ule ute ute,unyevuunyevu pamoja na msuguano,

LAKINI WAKATI MWINGINE uke kutoa povu si hali ya kawaida na mara nyingi inaweza kuashiria tatizo hasa kama kuna dalili nyingine pia. yapo matatizo kama vile;

Maambukizi ya uke – hasa maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama Trichomoniasis ambayo mara nyingi huleta uchafu wenye povu, harufu mbaya, kuwasha au hali ya kuungua.

Bacterial vaginosis – mabadiliko ya bakteria wa kawaida ukeni, yanaweza kusababisha uchafu usio wa kawaida.

Matumizi ya Baadhi ya Sabuni au kemikali zenye muwasho – baadhi ya bidhaa zinaweza kuleta reaction.

Mchanganyiko wa majimaji na hewa – wakati mwingine baada ya tendo la ndoa au movement fulani, inaweza kuonekana kama povu kidogo, lakini si mara kwa mara.

ANGALIZO: Tofautisha pia kati ya Povu na Uchafu mwingine ambao huweza kutoka wakati wa kufanya tendo

 MFANO; kama kuna uchafu wenye harufu mbaya, mzito na wenye rangi kama maziwa mgando au mtindi,Rangi ya njano, n.k wakati wakufanya tendo au hata baada sio dalili nzuri,

Ikiwa hivi sio kawaida na ni dalili za magonjwa mbali mbali kama vile; maambukizi ya fangasi ukeni,PID n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

#1Reply

Discussions