Simba na Yanga Watinga Fainali ya Kombe la Muungano Zanzibar
Timu kongwe za soka nchini Tanzania, Simba SC na Young Africans SC, zimefanikiwa kufika hatua ya mwisho ya Kombe la Muungano 2026 baada ya kuonyesha kiwango bora katika michezo ya awali.
Fainali hiyo itachezwa visiwani Zanzibar kwenye New Amaan Complex tarehe 29, ambapo mahasimu hao wa jadi watapambana kuwania ubingwa wa michuano hiyo.
Katika hatua zilizopita, kila timu ilionesha ubora mkubwa kuanzia robo fainali hadi nusu fainali, hali iliyowapa tiketi ya kucheza mchezo wa mwisho wa mashindano hayo.
Pambano hili linatarajiwa kuwa la kuvutia zaidi kutokana na ushindani mkubwa uliopo kati ya klabu hizo mbili zenye mashabiki wengi nchini Tanzania.
Cha kipekee zaidi, baada ya mchezo huo wa fainali, Simba SC na Young Africans SC watakutana tena Mei 3 katika mchezo wa Kariakoo Derby wa NBC Premier League.
Hivyo mashabiki wa soka wanatarajia wiki yenye burudani kubwa, huku wakisubiri kuona ni timu gani itaanza kwa kutwaa Kombe la Muungano kabla ya dabi nyingine ya ligi.
You, Mehreen and others


