Showing posts with label COVID-19. Show all posts
Showing posts with label COVID-19. Show all posts

WHO Ripoti mpya: kuna uhusiano wa COVID-19 na unene au utipwatipwa kwa WatotoAfyaclass Bongo Social •

WHO Ripoti mpya: kuna uhusiano wa COVID-19 na unene au utipwatipwa kwa Watoto

Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la afya la duniani WHO imesema kuna uhusiano baina ya COVID-19 na Watoto kukabiliwa na changamoto ya utipwatipwa au obesity barani Ulaya.

Ripoti hiyo ya WHO inasema imethibitisha ilichokuwa inakishuku kwa muda mrefu ambacho ni uhusiano baina ya janga hilo la COVID-19 na ongezeko la viwango vua utipwatipwa miongoni mwa Watoto wa kati ya umri wa miaka 7 hadi 9.”

Ripoti hiyo iliyopewa jina “Athari za COVID-19 kwa Maisha ya kila siku na tabia za Watoto wa umri wa Kwenda shule: Matokeo katika nchi 17 wanachama wa kanda ya Ulaya ya WHO”  inawasilisha utafiti unaoonyesha kwamba;

 “Janga la COVID-19 lilisababisha Watoto wengi kutumia muda mwingi kutazama vifaa vya kielecktroniki kama televisheni, Ipad , simu na vifaa vingine na kuwa na shughuli chache za mazoezi ya kimwili, na hivyo kuakisi ongezeko la watoto walio na uzito uliopitiliza katika umri ulioanishwa”

Utipwatipwa kwa watoto Ulaya

Ofisi ya Kanda ya WHO ya Ulaya ilianzisha mpango wa ufuatiliaji wa utipwatipwa kwa Watoto mwaka wa 2007 ili kukabiliana na hitaji la takwimu sanifu na sahihi za uchunguzi kuhusu kuenea kwa tatizo la uzito kupita kiasi na unene uliopitiliza miongoni mwa watoto wenye umri wa kwenda shule.

WHO imesisitiza kuwa “Upatikanaji wa taarifa kama hizo ni muhimu ili kuendeleza sera na mikakati madhubuti ya kukabiliana na unene wa kupindukia wa watoto katika Kanda ya Ulaya ya WHO.”

Awamu hii ya sita ya ukusanyaji wa twakimu za COSI inahusisha nchi wanachama 37 na ukusanyaji wa takwimu bado unaendelea katika baadhi ya nchi hizi.

Ripoti hii inawasilisha matokeo kutoka kwa majimbo 13 yaliyokusanya taarifa katika mwaka wa shule wa 2021-2022 kuhusu athari za janga la COVID-19 kwa afya ya watoto, na nne zilizokusanya taarifa katika mwaka wa shule wa 2022-2023.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo “Matokeo ya utafiti huu juu ya matokeo ya janga hili ni muhimu sana kwa Nchi Wanachama zinazoshiriki ili kusaidia kujiandaa kwa siku zijazo.”

Via; https://news.un.org/sw/story/2024/05/1174811

WHO Ripoti mpya: kuna uhusiano wa COVID-19 na unene au utipwatipwa kwa
Watoto
0 Comment

Matumizi makubwa ya dawa za Antibiotics kipindi cha COVID-19,hatari ya kuongeza UsuguAfyaclass Bongo Social •

Matumizi makubwa ya dawa za Antibiotics kipindi cha COVID-19,hatari ya kuongeza Usugu.

Ushahidi mpya uliotolewa na shirika la afya ulimwenguni, WHO unaonesha kuwa wakati wa janga la COVID-19 kulikuweko na matumizi yasiyo ya lazima na ya kupita kiasi ya viuavijasum au antibiotics ambayo huenda yamesababisha kusambaa kwa usugu wa viuavijiumbe maradhi au Antimicrobials.

Taarifa iliyotolewa leo Geneva, Uswisi na WHO inasema ingawa ni asilimia 8 tu ya wagonjwa waliolazwa kwa ajili ya COVID-19 ndio walikuwa na maambukizi yatokanayo na bakteria au vimelea na hivyo kuhitaji viuavijasumu, takwimu zinaonesha kuwa wagonjwa watatu kati ya wanne sawa na asilimia 75 ya wagonjwa walitibiwa kwa viujavijasumu pengine tu ingaliweza kuwasaidia hata kama haikuwa inahitajika.

Wagonjwa wasio mahututi Afrika walipatiwa viuavijasumu

Matumizi ya viuavijasumu yalikuwa ni kuanzia asilimia 33 kwa wagonjwa ukanda wa Pasifiki Magharibi hadi asilimia 83 ukanda wa Mediteranea Mashariki na Afrika.

Kati ya mwaka 2020 hadi 2022 kitendo cha daktari kuandikia dawa aina ya viuavijasumu kwa wagonjwa kilipungua huko Ulaya na Amerika, ilhali kiliongeza katika nchi za Afrika.

Kwa wastani kiwango kikubwa cha matumizi ya dawa hizo miongoni mwa wagonjwa wa COVID-19 waliokuwa mahututi kilifikia asilimia 81.

Ingawa hivyo kulikuwa na utofauti mkubwa wa utoaji wa dawa hizo kwa wagonjwa ambao hawakuwa mahututi lakini ukanda wa Afrika uliongoza kwa kupatiwa wagonjwa wa kiwango hicho kwa asilimia 79.

Matumizi holela ya viuavijasumu huweza kusababisha usugu wa dawa

“Pindi mgonjwa anapohitaji viuavijasumu, manufaa yake yanazidi hatari zitokanazo na matumizi ya dawa hizo au hatari za kuleta usugu hapo baadaye,” ameesma Daktari Silvia Bertagnolio, Mkuu wa kitengo cha Ufuatiliaji, Ushahidi na uimarishaji wa Maabara WHO.

Amesema “hata hivyo pindi viuavijasumu vinapotumika pale isipo lazima, hazina faida yoyote zaidi ya kuongeza hatari na matumzi yake yanaweza kusababisha kuibuka au kusambaa kwa usugu wa dawa hizo kwa vijiumbe maradhi, au microbes.”

Daktari Bertagnolio  amesema takwimu hizi mpya zinataka sasa kuimarisha matumizi sahihi ya viuavijasumu na kupunguza madhara yasiyo ya lazima kwa wagonjwa na jamii.

Kwa ujumla matumizi ya viuavijasumu hayakuimarisha tiba ya wagonjwa wa COVID-19. Badala yake, inaweza kuwa iliongeza hatari kwa watu ambao hawakuwa na maambukizi ya bakteria au vimelea ikilinganishwa na wale ambao hawakupatiwa dawa hizo wakati wanaugua COVID-19.

Utafiti huu kuchangia kwenye mapendekezo yajayo

Uchambuzi zaidi utafanyika wa takwimu hizi mpya ili ziweze kujumuishwa kwenye mapendekezo yajayo ya matumizi ya viujavijasumu kwa wagonjwa wa COVID-19, kama sehemu ya mwongozo wa tiba dhidi ya ugonjwa huo. Mkutano utafanyika Hispania mwezi ujao.

Na baadaye mwezi Septemba mwaka huu, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa litakuwa na kikao cha viongozi kukubaliana hatua za kupunguza usugu wa viuavijiumbe maradhi kwa ajili ya afya ya binadamu, Wanyama, na sekta ya kilimo pamoja na mazingira, halikadhalika kusongesha uongozi na ufadhili wa fedha ili kupunguza usugu wa dawa hizo au AMR.

Matumizi makubwa ya dawa za Antibiotics kipindi cha COVID-19,hatari ya
kuongeza Usugu
0 Comment

Una dalili zote za COVID-19 lakini ukipima hauna UgonjwaAfyaclass Bongo Social •

Una dalili zote za COVID-19 lakini ukipima hauna Ugonjwa.

JN.1, lahaja kuu kwa sasa ya COVID-19 inayochangia takriban asilimia 86% ya aina zote zinazozunguka za SARS-CoV-2, inaweza kuchukua muda mrefu kuonyesha matokeo chanya kwenye kipimo cha COVID ambacho watu wengi hujipima wakiwa nyumbani hasa kwenye nchi kama Marekani(home antigen tests),

Hali hii hupelekea watu wengi wana Dalili Zote za COVID-19 lakini wakifanya vipimo ugonjwa hauonekani.

Baadhi ya Wataalam wa afya pamoja na wagonjwa wamekuwa wakiripoti kwamba; Vipimo walivyofanya siku kadhaa baada ya dalili kujitokeza vilileta majibu NEGATIVE, Kisha baada ya siku Zaidi hapo baadae majibu yakawa POSITIVE. (link Source)

Soma Zaidi hapa; hali ilivyo kwa Sasa kuhusu ugonjwa wa COVID-19

Hii inasababisha kuwa na wasiwasi juu ya ubora wa Vipimo. “Je, vipimo vya nyumbani(home-antigen tests) vinaweza kugundua JN.1?” alitweet mtumiaji mmoja kwenye mtandao wa X, ambayo zamani ulijulikana kama Twitter, akionyesha pia wasiwasi wa wengine kwenye mitandao ya kijamii.

Kabla ya kulaumu Vipimo kwa kupoteza ufanisi — au lahaja hii ya COVID(JN.1) kuwa vigumu kugunduliwa — wataalam wa magonjwa ya kuambukiza hutoa ufafanuzi mwingine;

mifumo yetu ya kinga ni imara kuliko-2020. Pia wanaelekeza kwenye utafiti uliochapishwa mnamo Septemba ambao uligundua wagonjwa wengi hawapati majibu CHANYA kwenye kipimo hadi siku 4 baada ya kuambukizwa.

Mifumo yetu ya kinga inazidi kuimarika, alisema Peter Chin-Hong, MD, mtaalamu wa magonjwa ya kuambukiza na profesa wa dawa katika Chuo Kikuu cha California, San Francisco, Shule ya Tiba.

Wakati janga hilo likiendelea na idadi kubwa ya watu wamepata maambukizo, chanjo, au zote mbili, “Ni muhimu kuchukua tahadhari. Anaendelea kwa kusema..!!!

Hiyo inamaanisha kuwa tunaweza kugundua wagonjwa mapema wenye COVID kwa hivi sasa ikilinganishwa na hapo awali kwenye janga hili.

Una dalili zote za COVID-19 lakini ukipima hauna Ugonjwa
0 Comment

COVID-19: Maambukizi yaongezeka kwa asilimia 52 katika mwezi mmoja, yasema WHOAfyaclass Bongo Social •

COVID-19: Maambukizi yaongezeka kwa asilimia 52 katika mwezi mmoja, yasema WHO.

Shirika la Afya Duniani, WHO, jana limethibitisha idadi ya wagonjwa wa COVID-19 duniani kote inaongezeka kwa kasi na kwamba “tutarajie idadi kubwa zaidi ya wagonjwa katika miezi ijayo ya msimu wa baridi kali kwenye maeneo ya kaskazini mwa dunia.”

Takwimu za hivi karibuni kutoka WHO zikijikita katika wiki nne za kuanzia mwezi Novemba hadi Desemba 17 mwaka 2023 zinaonesha ongezeko la asilimia 52 ya idadi ya wagonjwa ikilinganishwa na siku 28 zilizotangulia.

Msemaji wa WHO Christian Lindmeier, amewajulisha waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi hii jana kuwa ongezeko hilo ni sawa na wagonjwa wapya 850,000, lakini takwimu kamili zinaweza kuwa za juu.

“Unafahamu kuwa duniani kote na umeshuhudia hata wengi wenu kwenye nchi zetu kwamba utoaji wa taarifa umepungua, vituo vya ufuatiliaji navyo vivyo hivyo, kwingine vimevunjwa kabisa au vimefungwa… kwa hiyo hii bila shaka inatupeleka kwenye kukosa picha halisi na tunatarajia kwa bahati mbaya idadi kubwa zaidi ya wagonjwa kuliko tulivyoripoti,” amesema Bwana Lindmeir.

Maambukizi mengi yamesababishwa na aina na mnyumbuliko mpya wa COVID uitwao JN.1 ambao kwa sasa unachunguzwa kwa kina na WHO kama mnyumbuliko unaopaswa kufuatiliwa kwa karibu.

Kwa mara ya kwanza aina hiyo  JN.1 ilibainika Marekani kabla ya kusambaa kwenye maeneo mengine kadhaa ya nchi.

Inatokana na mnyumbuliko wa COVID uitwao Omicron ambao ulihusishwa na ongezeko kubwa la maambukizi ya COVID-19 mwaka 2022.

COVID-19: Maambukizi yaongezeka kwa asilimia 52 katika mwezi mmoja,
yasema WHO
0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Bongo Social Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Bongo Social ASANTE.
UNDERSTOOD