Showing posts with label Kidonda kutoa usaha. Show all posts
Showing posts with label Kidonda kutoa usaha. Show all posts

Kidonda cha upasuaji kutoa usahaAfyaclass Forum •

Kidonda cha upasuaji kutoa usaha Sababu ni nini?

Kidonda cha upasuaji kutoa usaha sio dalili nzuri,asilimia kubwa ni Dalili ya maambukizi kwenye Kidonda.

Usaha kutoka kwenye mshono au kidonda cha Upasuaji ni ishara muhimu ya maambukizi ya eneo la upasuaji, na huonekana kama majimaji mazito ya rangi ya kijani, manjano, au kahawia na mara nyingi huambatana na maumivu yanayoongezeka, uwekundu, uvimbe, na hali ya kuwaka moto pia. 

Wasiliana na daktari mara moja ukiona dalili hizi, au homa zaidi ya 37.5°C, kwani maambukizi kwa kawaida huonekana siku au wiki baada ya upasuaji.

Dalili kuu za Kidonda cha Upasuaji kupata Maambukizi

1. Kutoa Usaha au maji maji mazito ya rangi ya kijani,njano au kahawia au kutoa maji maji yenye harufu mbaya.

2. Hali ya wekundu au eneo la kuzunguka Kidonda kubadilika rangi na kuwa jekundu

3. Hali ya kuhisi moto eneo la kuzunguka kidonda

4. Kupata Maumivu makali zaidi au hali ya kuvimba kwenye eneo la Kidonda,

Maumivu haya huongezeka badala ya kupungua kadri muda unavyokwenda

5. Kupata Homa,mwili kutetemeka n.k

7. Sehemu ya Kidonda Kuanza kuachia yaani(Wound Separation: The edges of the wound are pulling apart). 

Tafuta Msaada Haraka ikiwa:

  • Unapata Dalili hizi nilizozitaja
  • Epuka Kusugua eneo Zaidi unaweza kusambaza maambukizi zaidi

Je,Una tatizo hili na unahitaji Msaada wa Haraka,Tuwasiliane +255758286584.


0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Forum Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Forum ASANTE.
UNDERSTOOD