Showing posts with label Mdomo. Show all posts
Showing posts with label Mdomo. Show all posts

Dawa nzuri ya kutoa harufu mbaya mdomoniAfyaclass Forum •

Dawa nzuri ya kutoa harufu mbaya mdomoni

Shida hii ya kutoa harufu mbaya kinywani huwasumbua watu wengi, na wengine hushtuka baada ya kuambiwa kwamba Wakati wanaongea kuna harufu mbaya inatoka mdomoni,

Katika makala hii tumechambua zaidi kuhusu chanzo cha tatizo la kutoa harufu mbaya mdomoni pamoja na Dawa nzuri ya kutoa harufu mbaya mdomoni.

Chanzo cha tatizo la kutoa harufu mbaya mdomoni

Tatizo hili husababishwa na nini? zipo sababu mbali mbali ambazo huchangia kinywa kutoa harufu mbaya,

BAADHI YA SABABU HIZO NI PAMOJA NA;

- Baadhi ya vyakula, baada ya chakula kuvunjwa vunjwa na baadhi ya mabaki ya chakula kuganda kuzunguka meno huweza kupelekea mashambulizi ya bacteria pamoja na kinywa kuanza kutoa harufu mbaya,

Kula VITUNGUU MAJI, vitunguu saumu(garlic) au viungo vingine huweza kuongeza harufu mdomoni

- Uvutaji wa Sigara ikiwemo Tumbaku, mbali na kuwa kwenye hatari ya kupata magonjwa ya fizi(gum disease) na meno,wavutaji wa sigara ikiwemo tumbuku wapo kwenye hatari ya kupata shida ya kutoa harufu mbaya mdomoni

- kUtokusafisha kinywa vizuri(Poor oral and dental hygiene), Hii ni miongoni mwa sababu kubwa ambazo hupekea kutoa harufu mbaya kinywani,

Mbali na kutoa harufu mbaya kinywani, kutokusafisha meno na kinywa vizuri hupelekea mabaki ya chakula kuganda kwenye meno, hali ambayo hupelekea watu wengi sana kuwa na matatizo ya Meno.

KUMBUKA; Wataalam wa meno na kinywa wanasema,miongoni mwa sababu kubwa za matatizo ya meno kwa wagonjwa wengi ambao wanawapata, ni kuganda kwa uchafu kwenye meno kutokana na meno kutokusafishwa vizuri.

- Shida ya mdomo kuwa mkavu(Dry mouth), Mate husaidia sana kusafisha mdomo na kuondoa mabaki ya chakula(Food particles) ambayo huweza kusababisha harufu mbaya mdomoni,

Tatizo hili la mdomo kuwa mkavu yaani Dry mouth or xerostomia huweza kusababisha harufu mbaya kutoka kinywani kwa sababu ya upungufu mkubwa wa mate mdomoni,

Hali hii ya mdomo kuwa mkavu mara nyingi hutokea usiku ukiwa umelala, ndyo maana ukiamka asubuh mdomo hutoa harufu zaidi, mbali na kuwa na mabaki ya chakula mdomoni na kwenye meno kama hukupiga mswaki.

Endapo shida hii ya mdomo kuwa mkavu(xerostomia) hutokea wakati wote bila kuondoka,inabidi upate matibabu ya tatizo hili.

- Matumizi ya dawa, baadhi ya dawa huweza kuchangia tatizo hili la kutoa haruf u mbaya kinywani kwa kukausha mdomo(dry mouth) au kwa kutoa chemicals baada ya uvunjwaji wake,ambazo huweza kuongeza harufu mdomoni.

- Maambukizi ya magonjwa kwenye meno,Fizi na kinywa, kuwa na shida ya fangasi mdomoni, maambukizi ya bacteria, kidonda baada ya kutoa jino au meno,meno kuoza,vidonda mdomoni,n.k vyote hivi huweza kusababisha tatizo la kutoa harufu mbaya mdomoni.

matatizo mengine kama vile; Kansa au saratani, metabolic disorders,(gastroesophageal reflux disease, or GERD),N.k, vyote hivi huweza kuchangia uwepo wa tatizo hili.

Dawa nzuri ya kutoa harufu mbaya mdomoni

MATIBABU YA TATIZO HILI LA KUTOA HARUFU MBAYA KINYWANI

Baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kina pamoja na Vipimo,kisha wataalam wa afya kujua chanzo chake,ndipo tiba sahihi ya tatizo lako hufanyika.

Kama nilivyokwisha kueleza hapo juu baadhi ya sababu za tatizo hili, na matibabu yake yatahusu vyanzo vyake.

- Epuka uvutaji wa sigara ikiwemo tumbaku,

- Epuka matumizi ya Pombe,Ugoro n.k

- Hakikisha unasafisha kinywa na meno vizuri hasa baada ya kula

- Tumia mouth wash kama vile hydrogen perioxide n.k

- Epuka kutafuna vitunguu maji,vitunguu saumu,kula viungo vingi n.k

- Hakikisha unakunywa maji ya kutosha

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

 

0 Comment

Tatizo la mdomo kukauka chanzo chake na Tiba yakeAfyaclass Forum •

 Tatizo la mdomo kukauka chanzo chake na Tiba yake

Je unasumbuliwa na tatizo la kukauka mdomo pamoja na Lips zake?

Tatizo la Kukauka Mdomo kwa kitaalam hujulikana kama xerostomia na hutokea pale ambapo Tezi za mate (Salivary glands) hushindwa kutengeneza mate ya kutosha mdomoni hali ambayo hupelekea kushindwa kutengeneza mazingira ya unyevu unyevu mdomoni,

Na hii hutokea kwa Sababu mbali mbali ikiwemo;

- Matumizi ya baadhi ya Dawa, baadhi ya dawa zina side effect ya kukausha mdomo,

mfano; baadhi ya dawa za kutibu tatizo la depression,Wasiwasi(anxiety),Presha(high blood pressure), baadhi ya dawa za maumivu, dawa kwenye kundi la antihistamines,decongestants,pamoja na muscle relaxants.

- Umri kuwa Mkubwa(Aging), tafiti zinaonyesha watu wengi kadri umri unavyokuwa mkubwa zaidi ndivo hupata shida hii ya mdomo kukauka,

Na hili huenda sambamba na matumizi ya baadhi ya dawa,Mabadiliko kwenye mwili hasa kwa upande wa uwezo wa mwili kuchakata dawa, Lishe Duni pamoja na kuwa na matatizo mengine ya kiafya ya muda mrefu.

- Kukosa Virutubisho muhimu mwilini kama vile madini pamoja na Vitamins, mfano vitamin B,A N.k

Hii hutokana na Lishe duni, au kukosa Mlo wenye virutubisho vyote kwa kiwango sahihi kinachohitajika mwilini yaani balance diet.

- Matibabu ya Kansa au Saratani(Cancer therapy),

Mfano;Dawa za Chemotherapy huweza kubadilisha asili ya mate na kiasi kinachozalishwa.

Japo hali hii sio ya kudumu ni ya muda mfupi tu, mara baada ya mgonjwa kumaliza tiba, Uzalishwaji wa kawaida kwa mate hurudi tena kama awali.

Huduma ya Mionzi(Radiation treatments), hasa ikifanyika eneo la kichwani na shingoni, hii huweza kusababisha uharibifu wa tezi za Mate hali ambayo hupelekea kupungua sana kwa uzalishwaji wa Mate,

Hii nayo huweza kuwa ya muda mfupi au ya kudumu kutegemea na radiation dose pamoja na eneo lililokuwa linatibiwa.

- Uharibifu wa Neva, hii huweza kutokea baada ya mtu kuumia(Injury) au kufanyiwa Upasuaji ambao husababisha uharibu wa nerves eneo la Kichwani na Shingoni,

Hii huweza kupelekea mtu kupata tatizo la mdomo kukauka.

- Matatizo mengine ambayo huweza kuchangia tatizo la Mdomo kukauka ni pamoja na;

• Ugonjwa wa Kisukari(Diabetes)

• Tatizo la kiharusi(Stroke)

• Maambukizi ya fangasi wa Mdomoni-yeast infection (thrush)

• Alzheimer's disease

• Au magonjwa yanayohusisha mfumo wa kinga mwili(autoimmune diseases), kama vile Sjogren's syndrome

• Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(HIV/AIDS).

• Tatizo la Kukoroma na kupumua mdomo wako ukiwa wazi pia huweza kuchangia kinywa kuwa kikavu zaidi. n.k

- Matumizi ya tumbaku na Pombe. Uvutaji wa Sigara,kutumia tumbaku pamoja na Pombe, vyote hivi huweza kuchangia zaidi tatizo la mdomo kuwa mkavu

- Matumizi ya dawa za kulevyia,Mirungi(Marijuana) n.k

- Matumizi ya Recreational drugs kama vile Methamphetamine huweza kusababisha hali ya mdomo kukauka sana na kuharibu meno, tatizo ambalo kwa kitaalam hujulikana kama "meth mouth."

MADHARA YA TATIZO LA MDOMO KUKAUKA;

Kama huzalishi mate ya kutosha na mdomo wako ukakauka,hii inaweza kusababisha;

1. Meno yako kuwa kwenye hatari zaidi ya kuharibika(tooth decay)

2. Kupata magonjwa ya fizi yaani gum Diseases

3. Kupata vidonda mdomoni(Mouth sores)

4. Kuwa kwenye hatari zaidi ya kushambuliwa na fangasi wa mdomoni(Yeast infection)

5. kuwa na vidonda au ngozi kupasuka kwenye kona za mdomo

6. Lips za mdomo kupasuka(cracked lips)

7. Mdomo kutoa harufu mbaya n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.


0 Comment

Tatizo la mdomo kuwa mwekundu chanzo chake na Tiba yakeAfyaclass Forum •

 Tatizo la mdomo kuwa mwekundu chanzo chake na Tiba yake

CHANZO CHA TATIZO LA MDOMO AU LIPS ZAKE KUWA NYEKUNDU SANA

Tatizo la mdomo kwa ndani au kwenye lips kuwa na rangi nyekundu sana kuliko kawaida huweza kutokea kwa mtu yoyote, na kwa wengine hali hii huambatana na maumivu, kuhisi kuchomwa chomwa mdomoni,kuwashwa,kuvimba n.k

Maeneo ambayo huweza kuathirika na tatizo hili la wekundu usio wa kawaida ni pamoja na; mdomo(ndani),lips, ulimi pamoja na Fizi za meno.

CHANZO CHA TATIZO LA MDOMO AU LIPS ZAKE KUWA NYEKUNDU SANA

- Tatizo hili huweza kumpata mtu kutokana na sababu mbali mbali lakini sababu kubwa huweza kuwa mbili yaani;

1. Mtu kupata tatizo la kuumia mdomoni

2. Au kushambuliwa na vimelea vya magonjwa mbali mbali kama vile;

Bacteria,virusi au Fangasi ambao hushambulia ngozi nyembamba ndani mdomoni au kwenye lips

Hivo basi, tunaweza kusema magonjwa ambayo husababisha hali hii ni kama vile;

- Maambukizi ya virusi vya ukimwi

- Maambukizi ya virusi vya Herpes Simplex Virus

- Maambukizi ya Fangasi wa mdomoni

- Maambukizi ya fangasi wa kwenye ulimi n.k

3. Mtu kuwa na Matatizo kama leukemia pamoja na magonjwa mengine kama ya Ngozi,Saratani mdomoni n.k

4. Mtu kuwa na tatizo la Allergies au Mzio kwenye vitu mbali mbali ikiwemo vyakula,nyama,mafuta n.k

5. Upungufu wa Virutubisho mwilini kama Vile Vitamin B n.k, ambapo moja ya dalili zake ni pamoja na;

- Mdomo au Lips za mdomo kubadilika rangi na kuwa nyekundu n.k

- Mdomo kukauka Sana

- Mdomo,Lips za mdomo au Ulimi kupasuka n.k

DALILI AMBAZO MTU MWENYE TATIZO HILI HUWEZA KUZIPATA

• Joto la mwili kuwa juu au mgonjwa kuwa na homa

• Mgonjwa kupata uchovu wa mwili usio wa kawaida

• Mdomo wa mgonjwa kukauka sana kuliko kawaida

• Mgonjwa kukosa kabsa hamu ya kula chakula

• Mgonjwa kuhisi hali ya kuchomwa chomwa au kuungua moto mdomoni

• Mgonjwa kuanza kupata vipele au vidonda mdomoni

• Na kwa wengine mdomo huanza kuvimba wenyewe

MATIBABU YA TATIZO HILI

- Mgonjwa ataanza kupata matibabu kulingana na chanzo chake, mfano kama ni maambukizi ya fangasi wa mdomoni, mgonjwa ataanza kutibiwa fangasi, Kama ni maambukizi ya bacteria basi tipa itahusu eneo hili n.k

Hivo mgonjwa lazima aende hospital kwanza,kwa ajili ya uchunguzi wa kina ikiwa ni pamoja na vipimo na Tiba.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comment

Chanzo cha Mdomo Kuwa na Ladha ya ChumviAfyaclass Forum •

Chanzo cha Mdomo Kuwa na Ladha ya Chumvi

Chanzo cha Mdomo Kuwa na Ladha ya Chumvi, Unatarajia mdomo wako kuwa na ladha ya chumvi baada ya kula chumvi au vyakula vyenye chumvi, Lakini ikiwa haujala halafu kinywa chako kina ladha ya chumvi, ni nini kinaendelea? 

CHANZO CHA TATIZO LA MDOMO KUWA NA LADHA YA CHUMVI 

Kwa nini mdomo wangu una ladha ya chumvi?

 Mara nyingi mtu kuwa na ladha ya chumvi kinywani sio tatizo ambalo huhitaji matibabu ya dharura yaani sio medical emergency

 - lakini pia hupaswi kupuuzia tatizo hili,lazima upate tiba. Baadhi ya Sababu za kinywa kuwa na ladha ya chumvi ni pamoja na: 

1. Upungufu wa Maji Mwilini yaani Dehydration Mate yako kwa asili yana kiasi kidogo cha chumvi. 

Lakini wakati una upungufu wa maji mwilini, chumvi kwenye mate yako inakuwa zaidi. Upungufu wa maji mwilini hubadilisha ubora wa mate yako ikiwemo ongezeko la chumvi kwenye mate yako, Mara nyingi, unaweza kuondoa ladha ya chumvi kwenye mdomo wako kwa kunywa maji ya kutosha kila siku. 

2. Kuwa na Tatizo la Mdomo mkavu(Dry mouth) au kwa kitaalam zaidi hujulikana kama xerostomia, Tatizo hili la mdomo kukauka hutokea wakati tezi zako za mate hazitengenezi mate ya kutosha. 

Watu wenye kinywa kikavu wanaweza kuona matatizo ya ladha pia, ikiwa ni pamoja na hili la kupata ladha ya chumvi mdomoni.

 3. Matumizi ya baadhi ya Dawa, baadhi ya dawa ukizitumia huweza kuwa na maudhi madogo madogo(side effects) kama vile;

 Kusababisha mdomo kukauka, kusababisha mdomo kuwa na Ladha ya chumvi n.k, Haya ni baadhi ya makundi ya dawa ambayo huweza kusababisha tatizo hili, 

• Dawa jamii ya Antidepressants hasa hasa tricyclic antidepressants.

 • Dawa jamii ya Antihistamines

 • Matibabu ya Chemotherapy kwa ajili ya Kansa

 • Dawa jamii ya Diuretics, hasa hasa zile zinazotolewa kwa wagonjwa wa moyo au Figo 

• Baadhi ya dawa za maumivu(Pain relievers)

 • Dawa jamii ya Sedatives, kwa ajili ya kutibu tatizo la wasiwasi(anxiety), panic disorders au matatizo ya Usingizi. 

4. Tatizo la Mzio(allergies) au maambukizi ya muda mrefu(sinus infection), ambayo husababisha ukavu mpaka kooni, Hii pia huweza kuleta ladha ya Chumvi mdomoni.

 5. Ujauzito, mabadiliko mengi hutokea kwa mjamzito kutokana na mabadiliko ya vichocheo mwilini, mabadiliko hayo ni pamoja na mama mjamzito kuvimba Pua, kupata sana hamu ya kula,kukosa kabsa hamu ya kula,na wakati mwingine kubadilika kabsa kwa ladha mdomoni ikiwemo kupata ladha ya Chumvi mdomoni. 

6. Tatizo la Gastroesophageal reflux disease (GERD), Hii hutokea pale ambapo Acid kutoka tumboni hupanda juu kwenye esophagus, Tatizo hili huweza kubadilisha ladha mdomoni, na kuleta ladha ya Chumvi, ladha chungu(sour taste) n.k Pia watu wengi wenye tatizo hili la GERD (chronic acid reflux) hupata Kiungulia mara kwa mara, kikohozi ambacho hakiishi, na kuhisi kama kuna kitu kimebakia kooni. 

7. Tatizo la mfumo wa kinga Mwili(Autoimmune conditions), Hapa tunazungumzia wakati mfumo wa kinga yako ya mwili unapoanza kushambulia healthy tissue. Kama una matatizo kama vile lupus au rheumatoid arthritis, upo kwenye hatari zaidi ya kupata Sjögren’s syndrome. Hali ambayo huathiri tezi za Mate,na kusababisha Ukavu mdomoni pamoja na kubadilisha ladha mdomoni. 

8. Matatizo kwenye Neva(Neurological disorders), mabadliko yoyote yasioyakawaida kwenye ladha ikiwemo kupata ladha chungu au ladha ya chumvi mdomoni humaanisha kwamba sehemu ya Ubongo wako inayopokea taarifa zinazohusiana na ladha haifanyi kazi vizuri, 

Japo sio mara nyingi hutokea, lakini Nerves zinazohusishwa na kupeleka taarifa za ladha kwenye Ubongo zikiwa na shida yoyote kama vile; mtu akiwa na uvimbe kwenye ubongo,kuumia ubongo n.k, huweza kusababisha madhara mbali mbali ikiwemo; kubadilika kwa ladha mdomoni,maumivu ya kichwa,kizunguzungu,mtu kutokuona vizuri,kutokusikia harufu ya vitu n.k

 KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584. 



0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Forum Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Forum ASANTE.
UNDERSTOOD