Baada ya miaka zaidi ya 50 tangu enzi za Apollo program
Binadamu amerudi tena kwenye ndoto ya kwenda Mwezini.Lakini safari hii si ya kawaida.Hii ni safari ya hatari zaidi… ndefu zaidi… na yenye siri nzito zaidi.
Hii ni Artemis.
Safari Iliyofwatiliwa na Watu wengi Duniani Kote.
Kupitia chombo kipya cha kisasa kiitwacho Orion Spacecraft wanaanga wanatumwa mbali zaidi kuliko hapo awali.
Safari hizi:
- Zinachukua muda mrefu zaidi angani
- Zinawaweka wanaanga kwenye mionzi hatari ya anga (space radiation)
- Zinawatoa mbali kabisa na ulinzi wa Dunia
Hii si safari ya majaribio…
Hii ni safari ya kujaribu mipaka ya binadamu.
Walichokutana Nacho Angani
Wakiwa mbali na Dunia, wanaanga wanaripoti:
- Ukimya mzito usioelezeka
- Giza la kina lisilo na mwisho
- Na hisia ya kutengwa kabisa na ulimwengu
Baadhi yao wanasema…
“Unaanza kujisahau wewe ni nani…”
Kurudi Duniani… Lakini Sio Kama Walivyoondoka
Wengi hudhani safari inaisha wakirudi.
Lakini kwa wanaanga…
hapo ndipo changamoto huanza.
1. Athari za Akili (Psychological Effects)
Baada ya kuona ukubwa wa anga:
- Dunia inaonekana ndogo sana
- Maisha ya kawaida yanaonekana hayana maana
- Baadhi ya Wanaanga hupata tatizo la msongo wa mawazo
Hii hali inajulikana kama OverView Effect
2. Mwili Kudhoofika
Kutokana na Kuwa muda mrefu Angani:
- Mifupa hupoteza nguvu
- Misuli hudhoofika
- Moyo hubadilika namna ya kufanya kazi
Wanarudi wakiwa dhaifu… hata kutembea huwa changamoto kwa baadhi yao. Ndyo Mana Wanaanga hufanya sana mazoezi hata wakiwa Angani.
3. Hatari ya Mionzi ya Anga
Tofauti na zamani, safari za Artemis zinawaweka wanaanga kwenye:
- Mionzi mikali ya jua
- Hatari ya kupata magonjwa ya muda mrefu n.k
Baadhi ya wanaanga:
- Hujitenga na jamii
- Hupoteza mwelekeo wa maisha
- Hupata matatizo ya kifamilia
Kwa sababu akili yao… bado iko angani.
UKWELI USIOSEMWA SANA
Safari za anga zinaonekana kama ushindi mkubwa…
Lakini ukweli ni huu:
Si kila mwanaanga hurudi akiwa yule yule.
HITIMISHO
Pamoja na Mambo yote,Afya za Wanaanga ni muhimu sana,Ndyo Maana kufwatiliwa kwa karibu sana,ili kukuabiliana na mabadiliko yoyote yaliyotokea kwenye miili yao wakiwa nje ya Dunia.




0 Comments