Showing posts with label Miguu. Show all posts
Showing posts with label Miguu. Show all posts

Chanzo Cha Tatizo La Kuvimba Miguu Na Matibabu YakeAfyaclass Forum •

Chanzo Cha Tatizo La Kuvimba Miguu Na Matibabu Yake

Tatizo la kuvimba miguu na vifundo vyake ni shida ya kawaida sana kutokea haswa kwa watu ambao umri umeenda au wazee,

japo siku hizi ni tatizo ambalo huweza kutokea kwa kila mtu. Mkusanyiko usiokuwa wa kawaida wa Majimaji ya mwili au (body fluid) ndani ya Tissues kwenye vifundo na miguu, huweza kusababisha Miguu kuvimba au kwa kitaalam huitwa edema.

Kuwa na shida ya Mkusanyiko wa maji sehemu moja kwenye miguu ambapo tunaita Fluid retention huweza kusababisha hali hii.

Chanzo Cha Tatizo La Kuvimba Miguu

VISABABISHI VYA TATIZO LA KUVIMBA MIGUU

Zipo Sababu mbali mbali ambazo huleta shida hii,na baadhi ya Sababu hizo ni pamoja na;

  1.  Kuwa na uzito mkubwa au uliopitiliza huweza kusababisha miguu kuvimba mara kwa mara
  2. Kuambukizwa magonjwa ya miguu ambayo huathiri kusukuma damu vizuri 
  3. Kukaaa kwa Muda Mrefu sehemu Moja Mfano wakati wa Safari Ndefu,watu wengi hupata tatizo la kuvimba miguu
  4. Kusimama kwa muda mrefu, mara nyingi husababisha kuvimba kwa miguu na vifundo vyake
  5. kupata matatizo au magonjwa ya moyo
  6. Kugongwa na kitu,au kuumia kwenye Miguu huweza kusababisha kuvimba
  7. Upasuaji unaojumuisha mguu, au kifundo cha mguu huweza kusababisha kuvimba
  8. Ugonjwa wa Figo, Pia wagonjwa wa Figo huweza kupata shida hii ya kuvimba miguu
  9. Tatizo la Miguu kuvimba linaweza kutokea Pia kwa wanawake WAJAWAZITO au wakati Flani katika mzunguko wa hedhi.  Wanawake wengi  huvimba Miguu wakati wa ujauzito.  Ingawa Uvimbe wa miguu kupita kiasi wakati wa ujauzito inaweza kuwa ishara mojawapo ya Ugonjwa wa kifafa cha Mimba
  10. Miguu  kuvimba inaweza kuwa ishara ya kushindwa kwa moyo kufanya kazi, figo kushindwa kufanya kazi, au ini kushindwa kufanya kazi.
  11. Matumizi ya baadhi ya Dawa;Dawa zingine pia zinaweza kusababisha miguu yako kuvimba:

JINSI YA KUGUNDUA UWEPO WA TATIZO LA KUVIMBA MIGUU

Wataalam wa afya au Daktari wako atachukua historia ya Tatizo lako,kufanya uchunguzi kamili wa mwili, akizingatia moyo wako, mapafu, tumbo, nodi za limfu,  na miguu kwa ujumla.

Utaulizwa maswali kama haya yafuatayo:

 ➖ Sehemu gani za mwili zinavimba? miguu?  Juu ya goti au chini?

 ➖ Je! Una uvimbe wakati wote au hutokea wakati wa safari,umekaa,umesimama mda mrefu,asubuhi au jioni? 

➖Ni nini ukikifanya uvimbe wako hupungua au kuisha?

 ➖ Ni nini kinachofanya uvimbe wako kuongezeka zaidi?

➖Je! Uvimbe unapungua wakati unainua miguu yako?

 ➖ Je! Una dalili gani zingine?

 Uchunguzi ambao unaweza kufanywa ni pamoja na:

- Vipimo vya damu

 - X-ray ya kifua

- ECG

- Uchunguzi wa mkojo n.k

Vipimo hivo vitakusaidia kujua sababu ya Kuvimba kwa Miguu yako

UKIONA VIASHIRIA KAMA HIVI HAPA CHINI TAFTA MSAADA WA HARAKA

Hali ya Kuvimba Miguu inaambatana na Dalili hizi;

(1) Unajisikia kukosa pumzi.

 (2) Unapata maumivu ya kifua, kifua kuwa kizito au kubana.

 (3) Una ugonjwa wa moyo au ugonjwa wa figo na Kuvimba kunazidi kuongezeka

 (4) Una historia ya ugonjwa wa ini na sasa unapata tatizo la kuvimba miguu yako au tumbo.

(5) Mguu wako umevimba na unabadilika rangi na kuwa mwekundu au unahisi hali ya kuwaka moto sana hasa ukiushika.

 (6) Unavimba Miguu na Unapata homa.

 (7) Wewe ni mjamzito na miguu umevimba kupita kiasi.

MATIBABU YA TATIZO LA KUVIMBA MIGUU

-Inua miguu yako juu wakati umelala chini. Zoezi hili husaidia kusukuma maji kutoka kwenye miguu yako kurudi sehemu ya juu ya mwili wako,hivo kuondoa Uvimbe miguuni,Ingawa hii inaweza isiwe tiba ya kudumu kulingana na chanzo husika.

 - Wakati wa kusafiri,mara nyingi jitahidi uwe unasimama na kuzunguka mara kwa mara, Ikiwa shida ya kuvimba Miguu hutokea wakati wa Safari.

- Epuka kuvaa mavazi ya kubana sana Miguu au eneo karibu na mapaja yako.

 - Punguza uzito wa mwili ikiwa inahitajika

 - Epuka matumizi ya dawa zozote ambazo zinaweza kusababisha tatizo la kuvimba Miguu

- Pia Tiba zingine kama Dawa,Upasuaji n.k, kulingana na sababu au chanzo cha Tatizo hili la miguu kuvimba huweza kuhitajika 

KWA USHAURI ZAIDI/ELIMU/TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584

0 Comment

Maambukizi ya fangasi ambao husababisha Madoa meusi kwenye Miguu na MikonoAfyaclass Forum •

Maambukizi ya fangasi ambao husababisha Madoa meusi kwenye Miguu na Mikono(Tinea nigra)

Tinea nigra ni maambukizi ya Fangasi ambao huweza kusababisha Mtu kuwa na madoa meusi au brown kwenye miguu kwa chini,kwenye viganja vya Mikono n.k

Aina hii ya Fangasi ni adimu na Hujulikana kwa Kitaalam kama Hortaea werneckii,

ambapo hawa fangasi kwa asilimia kubwa ndyo husababisha maambukizi ya tinea nigra

Fangasi hawa wanaweza kupenya Kwenye mwili wako kupitia kidonda n.k

DALILI ZA MAAMBUKIZI YA FANGASI HAWA

- Kusababisha madoa meusi au brown Chini ya Miguu kwenye sole au kwenye viganja vya Mikono

-Madoa haya huanza kidogo kidogo hali ambayo inaweza kuwa ngumu kugundua wakati yanaanza

- Madoa miguuni au mikononi kuanza kutokea baada ya kuumia n.k

(Tazama mfano wa madoa haya kwenye picha)

CHANZO CHA MAAMBUKIZI HAYA YA TINEA NIGRA

Tinea nigra ni maambukizi ya Fangasi ambao hujulikana kama Hortaea werneckii; Cladosporium werneckii, Exophiala werneckii, au Phaeoannellomyces werneckii.

Japokuwa fangasi wengine kama Stenella araguata pia wanaweza kusababisha tinea nigra.

Jamii ya Fangasi hawa hupatikana mazingira ya Unyevu unyevu sana, kwenye mizoga,vitu vilivyoharibika,mbao/mti,udongo n.k

Na huingia kwa Mtu baada ya kupata upenyo kama wa kidonda, na Moja kwa moja kuishi kwenye eneo la mwili ambapo kuna tezi nyingi za jasho kama vile miguuni na mikononi.

MATIBABU YA MAAMBUKIZI HAYA YA TINEA NIGRA

Jamii ya dawa mbali mbali huweza kutumika,kama vile keratolytic agents mfano;
• wart cream
• salicylic acid
• Whitfield’s ointment n.k

KUMBUKA; Dawa hizi ni hatari kwa Ujauzito, hivo epuka kutumia dawa hizi ukiwa Mjamzito,ongea na wataalam wa afya Kwanza, kupata Ushauri wa kina zaidi.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comment

Ugonjwa Wa Mycetoma (Mguu Wa Madura),Chanzo,Dalili Na Tiba YakeAfyaclass Forum •

 UGONJWA WA MYCETOMA (MGUU WA MADURA),CHANZO,DALILI NA TIBA YAKE

Mycetoma ni ugonjwa ambao husababishwa na bacteria pamoja na Fangasi ambao huingia mwilini kupitia kwenye ngozi iliyo na upenyo maeneo ya miguuni.

Bacteria wanaosababisha ugonjwa wa Mycetoma hujulikana kama ACTINOMYCETOMA na Fangasi wanaosababisha Ugonjwa wa Mycetoma hujulikana kama EUMYCETOMA.

Mara nyingi ugonjwa huu hushambulia ngozi na tishu laini maeneo ya miguuni, hasa mguu mmoja peke yake,Ugonjwa huu hushambulia mtu wa umri wowote ila kwa asilimia kubwa wanaume huonekana kushambuliwa zaidi ya wanawake, Pia miongoni mwa watu ambao huathirika zaidi na ugonjwa huu ni pamoja na Wakulima na Wafugaji.

Hakuna takwimu za moja kwa moja kwamba ugonjwa wa mycetoma umeathiri watu wangapi Duniani mpaka sasa,ila Kuna wastani wa Cases 17,607 ambazo ziliripotiwa mwaka 2017 katika "Review of Scientific articles ya mwaka 1950 na 2017"

VISABABISHI VYA UGONJWA WA MYCETOMA(MGUU WA MADURA)

Kama nilivyokwisha kuelezea hapo juu,Ugonjwa wa Mycetoma husababishwa na Bacteria ambao hujulikana kama ACTINOMYCETOMA pamoja na Fangasi wanaojulikana kama EUMYCETOMA.

Kwa ujumla miongoni mwa vimelea vinavyosababisha ugonjwa huo ni pamoja na; Madurella mycetomatis, Nigrograna mackinnonii, Trematosphaeria grisea (formerly Madurella grisea), Falciformispora senegalensis, Medicopsis romeroi, Pseudoallescheria boydii/Scedosporium apiospermum), Acremonium falciforme na Fusarium solani. Vimelea hawa huishi au hupatikana katika udongo na humuingia mtu kupitia mipasuko midogo midogo kwenye mguu ambao mtu anaweza kupata endapo akichomwa na miiba,vifuu,au kitu chochote katika eneo la kazi.

DALILI ZA UGONJWA WA MYCETOMA(MGUU WA MADURA) NI PAMOJA NA;

- Mgonjwa kuwa na vijinundu nundu (subcutaneous nodules) katika ngozi ambavyo mwanzoni haviumi lakini vinaongezeka ukubwa kadiri siku zinavyokwenda

- Baada ya muda, vijinundu hivo huanza kuungana na kutengeneza uvimbe mkubwa (tumors) katika eneo husika

- Uvimbe huu unaweza kutengeneza usaha kwa maana ya kua jipu (necrotic abscesses) na baadae kuanza kutokea vijinjia vidogo vidogo (draining sinus tracts) ambavyo vinakua vinatoa maji maji au usaha kutoka ndani ya uvimbe uliopo kwenye mguu husika.

- Kama hali hii isipotibiwa ugonjwa huzidi kua mkubwa,uvimbe huzidi kuongezeka na hatimae mguu unaweza kuharibika kabisa (uharibifu wa kudumu). Wakati mwingine hali hii inaweza kuingia ndani kabisa na kuhusisha nyama za ndani,mishipa ya damu na limfu na mifupa.

- Baada ya vijinundu kuwa vikubwa zaidi huweza kugeuka na kuwa vidonda yaani Oozing Sores

- Na pia kama mgonjwa hakupata tiba,ugonjwa huu wa mycetoma huweza kusambaa kutoka mguuni kwenda maeneo mbali mbali ya mwili wake

NAMNA UGONJWA WA MYCETOMA(MGUU WA MADURA) HUGUNDULIKA

Ugonjwa Huu wa mycetoma huweza kugundulika kupitia;

• Kuchukua historia yake kutoka kwa mgonjwa

• Kuangalia kwa macho eneo lililoathirika na ugonjwa huu

• Kuchukua vipimo vya maabara kama vile Biopsy,Damu n.k

• Kufanyiwa kipimo cha X-ray, Ultrasound au vipimo vya mionzi ili kuweza kuona kiundani maneo ya ndani kama kwenye viungo, mifupa n.k.

MATIBABU YA UGONJWA WA MYCETOMA(MGUU WA MADURA)

Mgonjwa huweza kupata tiba mbali mbali kulingana na chanzo cha ugonjwa pamoja na hali yake kwa wakati huo,na endapo mgonjwa ataanza tiba mapema hupona vizuri kabsa kwa haraka zaidi,

Matibabu ya ugonjwa huu wa mycetoma ni pamoja na kutumia dawa jamii ya Antibiotics kama umesababishwa na Bacteria(Actinomycetoma) pamoja na matumizi ya dawa jamii ya antifungal kama chanzo chake ni fangasi(Eumycetoma).

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comment

Shida Ya Ganzi Miguuni(Miguu Kufa Ganzi)Afyaclass Forum •

 SHIDA YA GANZI MIGUUNI(MIGUU KUFA GANZI)

Watu wengi wamekuwa wakichanganya ganzi na hisia nyingine kama miguu kuwaka moto, kutekenywa na hata kuhisi kukanyaga kitu chenye ncha kali.

Kufa ganzi ni kitendo cha kupoteza hisia katika sehemu husika. Tatizo/ kitendo hiki kinaweza kuwa ni cha muda mfupi au muda mrefu na kinaweza kuwa baadhi ya sehemu au sehemu mbalimbali.

Hali hii inaweza kuwa ni dalili ya shida katika mfumo wa fahamu.

Mtu anapogusa kitu hisia au taarifa hupokelewa na vipokeo vilivyo katika ngozi kisha husafirishwa na mishipa ya neva mpaka kwenye uti wa mgongo na kisha kwenye ubongo kwaajili ya kutafasiriwa. Na baada ya ubongo kuchakata taarifa hizi hurudisha taarifa kupitia mishipa ya neva mpaka eneo husika.

Kufa ganzi hupelekea kupoteza uwezo wa kuhisi kuguswa, joto, kuhisi maumivu na mitetemo na baadhi ya watu hupelekea kushindwa kutambua zilipo sehemu husika za mwili wao.

Kufa ganzi hupelekea kukosekana kwa hisia/taarifa na kunaweza pelekea mtu kupata maambukizi, vidonda na majeraha yanayoweza kupelekea majanga ya kukatwa mguu au sehemu husika.

SABABU ZA MIGUU KUFA GANZI

Kufa ganzi hutokea iwapo kuna changamoto katika njia ya usafirishaji wa hisia/ taarifa. Shida hii inaweza tokeo kwenye vipokeo(receptors), mishipa ya neva, uti wa mgongo au ubongo.

Miongoni mwa mambo yanayoweza haribu njia hii ya usafirishwaji wa taarifa/hisia ni

1. Kupungua au kuzuiwa kwa usafirishwaji wa damu kwenda kwenye mishipa ya neva mfano kwenye kiharusi (stroke)

2. Ajari au magonjwa ambayo yanashambulia mishipa ya neva

3. Kukandamizwa kwa neva (mfano watu wenye tatizo za pingili za mgongo, uvimbe, usaha au mabonge ya damu yatokanayo na ajari)

4. Upungufu wa vitamin hasa vitamin B12

5. Sumu, madawa na kemikali kali

6. Magonjwa kama kisukari na magonjwa ya figo

7. Magonjwa yatokanayo na kinga mwili kushambulia mishipa ya neva.

DALILI AMBAZO HUWEZA KUAMBATANA NA KUFA GANZI.

Chanzo/sababu ya kufa ganzi inaweza kugundulika kutokana na dalili ambazo zimeambatana kwamfano

1. Maumivu ya mgongo na shingo, kichwa na viungo

2. Homa na mabakamabaka mwilini kwa baadhi ya wagonjwa

3. Miguu kukakamaa sana hasa pale unapohitaji kutembea

4. Kushindwa kunyoosha miguu au mguu n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Forum Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Forum ASANTE.
UNDERSTOOD