Showing posts with label Mjamzito. Show all posts
Showing posts with label Mjamzito. Show all posts

Mjamzito Mapigo Ya Moyo Kwenda MbioAfyaclass Forum •

Mjamzito Mapigo Ya Moyo Kwenda Mbio

Mapigo ya moyo kwenda mbio kwa mjamzito (moyo kudunda haraka) ni jambo linaloweza kutokea mara nyingi wakati wa ujauzito. Wakati mwingine ni kawaida, lakini wakati mwingine linaweza kuashiria tatizo.

Sababu za kawaida (zisizo hatari)

Hizi hutokana na mabadiliko ya mwili kipindi cha ujauzito:

  • Kuongezeka kwa ujazo wa damu mwilini (Blood volume)(moyo hufanya kazi zaidi)
  • Homoni za ujauzito
  • Wasiwasi au msongo wa mawazo
  • Uchovu au kukosa usingizi
  • Kunywa kahawa/ chai nyingi au vinywaji vyenye caffeine

Sababu zinazoweza kuwa hatari

  • Upungufu wa maji mwilini (dehydration)
  • Upungufu wa damu (anemia)
  • Kiwango cha sukari mwilini kuwa chini (low blood sugar)
  • Shinikizo la juu la damu au preeclampsia

Muone daktari haraka kama kuna dalili hizi:

  • Mapigo ya moyo yanaenda kwa kasi sana na hayapungui,Dalili zinaendelea muda mrefu
  • Kizunguzungu au kuzimia
  • Maumivu ya kifua
  • Kupumua kwa shida
  • Mapigo yasiyo ya kawaida (kuruka-ruka)
  • Kuvimba sana mwilini
  • Homa

Nini cha kufanya nyumbani

  • Kunywa maji ya kutosha
  • Pumzika na lala ubavu wa kushoto
  • Epuka kahawa nyingi na soda
  • Kula milo midogo mara kwa mara
  • Epuka joto kali na msongo
0 Comment

Mama mjamzito kuumwa tumbo na kuharishaAfyaclass Forum •

Mama mjamzito kuumwa tumbo na kuharisha

Sababu za Kuumwa tumbo na Kuharisha Wakati wa Ujauzito

Kuumwa tumbo na Kuharisha wakati wa ujauzito ni hali inayowakumba wanawake wengi na inaweza kuwa na athari kubwa kwa afya ya mama na mtoto. Hii ni hali inayoweza kusababishwa na mambo mbalimbali, na ni muhimu kuelewa sababu za kuumwa tumbo na kuharisha kwa mjamzito pamoja na jinsi ya kudhibiti hali hii. 

Katika makala hii, tutaeleza kwa kina sababu za kuumwa tumbo na kuharisha kwa mama mjamzito, jinsi ya kukabiliana na hali hii, tiba zinazopatikana, mapendekezo muhimu, na ushauri kwa wanawake wajawazito.

Sababu za Kuumwa tumbo na Kuharisha Wakati wa Ujauzito

Sababu za kuumwa tumbo na kuharisha wakati wa ujauzito zinaweza kuwa nyingi na hutofautiana kutoka kwa mama mmoja hadi mwingine. Hapa chini ni baadhi ya sababu kuu zinazoweza kusababisha kuumwa tumbo na kuharisha kwa mama mjamzito:

1. Mabadiliko ya Homoni

Mabadiliko ya Progesterone: Wakati wa ujauzito, kiwango cha homoni ya progesterone kinaongezeka. Progesterone inasaidia kulegeza misuli ya mfuko wa uzazi ili kuzuia kuharibika kwa mimba, lakini pia inaweza kulegeza misuli ya mfumo wa mmeng'enyo wa chakula, hivyo kusababisha kuumwa tumbo, kuharisha au kujaa kwa tumbo.

Mabadiliko ya Estrogen: Homoni ya estrogen pia inabadilika kwa kiasi kikubwa wakati wa ujauzito. Hii inaweza kuathiri jinsi mfumo wa mmeng'enyo wa chakula unavyofanya kazi, ikichangia katika tatizo la kuumwa tumbo na kuharisha.

2. Mabadiliko ya Chakula na Lishe

Kubadilika kwa Lishe: Mama wajawazito mara nyingi hubadilisha mlo wao ili kuendana na mahitaji ya ujauzito. Mabadiliko haya yanaweza kusababisha kuharisha, hasa ikiwa mama anaanza kula vyakula vipya au vyenye viungo vingi au  mafuta mengi.

Vyakula Vilivyochafuka: Kula vyakula vilivyochafuka au vya kuandaliwa kwa usafi mdogo kunaweza kusababisha maambukizi ya bakteria kama vile Salmonella au E. coli, ambayo yanaweza kusababisha kuumwa tumbo na kuharisha.

3. Maambukizi ya Bakteria na Virusi

Infection ya Bakteria: Maambukizi ya bakteria kutoka kwa vyakula vilivyochafuka au maji yasiyo safi yanaweza kusababisha kuumwa tumbo na kuharisha. Bakteria kama vile Campylobacter, Salmonella, na Shigella ni baadhi ya vyanzo vya maambukizi.

Infection ya Virusi: Virusi kama vile rotavirus na norovirus vinaweza kusababisha maambukizi ya mmeng'enyo wa chakula,kuumwa tumbo na kuharisha.

4. Magonjwa ya Mfumo wa Mmeng'enyo wa Chakula

Irritable Bowel Syndrome (IBS): Hali hii inaweza kuwa mbaya zaidi wakati wa ujauzito kutokana na mabadiliko ya homoni na msongo wa mawazo.

Inflammatory Bowel Disease: Magonjwa kama vile Crohn's disease na ulcerative colitis yanaweza kuathiri mfumo wa mmeng'enyo wa chakula na kusababisha kuumwa tumbo na kuharisha.

5. Matumizi ya Dawa

Antibiotics: Dawa za antibiotics zinaweza kuua bakteria nzuri kwenye utumbo, na hivyo kusababisha kuumwa tumbo na kuharisha kama athari.

Vitamini na Virutubisho: Baadhi ya virutubisho vya vitamini, hasa kwa kiwango kikubwa, vinaweza kusababisha matokeo ya kuumwa tumbo na kuharisha.

6. Msongo wa Mawazo na Mabadiliko ya Kihisia

Msongo wa Mawazo: Msongo wa mawazo kwa mjamzito unaweza kuathiri utendaji wa mfumo wa mmeng'enyo wa chakula, hivyo kusababisha kuuma tumbo na kuharisha.

Mabadiliko ya Kihisia: Hali ya kihisia na hali ya kiakili zinaweza kuathiri mfumo wa mmeng'enyo wa chakula, na kusababisha hali ya kuumwa na tumbo na kuharisha.

Namna ya Kukabiliana na kuumwa na tumbo na Kuharisha wakati wa Ujauzito

Namna ya kuzuia kuumwa na tumbo na kuharisha wakati wa ujauzito ni muhimu ili kuepuka athari zinazoweza kutokea. Hapa chini ni vidokezo na hatua zinazoweza kuchukuliwa:

a. Kudumisha Usafi wa Chakula na Maji: 

Hakikisha unakula vyakula vilivyoandaliwa kwa usafi. Epuka vyakula vilivyoandaliwa kwa usafi duni huweza kuwa na vimelea vya magonjwa. Safisha mikono yako mara kwa mara kabla ya kula au baada ya kutumia choo ili kupunguza hatari ya maambukizi. Kunywa maji safi, Epuka kunywa maji yasiyo na uhakika wa usalama.

b. Kufuata Lishe Bora:

 Kula milo midogo midogo mara kwa mara inaweza kusaidia kupunguza mzigo kwenye mfumo wa mmeng'enyo wa chakula. Epuka vyakula vyenye mafuta mengi, vyakula vyenye viungo vikali, na vyakula vilivyoandaliwa kwa usafi mdogo.

c. Kudhibiti Msongo wa Mawazo: 

Dhibiti msongo wa mawazo,hii inaweza kusaidia katika kudhibiti athari za kihisia kwenye mfumo wa mmeng'enyo wa chakula. Ikiwa msongo wa mawazo ni tatizo kubwa kwako, tafuta msaada kutoka kwa mshauri au mtaalamu wa afya ya akili.

Hitimisho

Sababu za kuumwa tumbo na kuharisha kwa mama mjamzito ni nyingi na zinaweza kuwa na athari kubwa kwa afya ya mama na mtoto. Kutambua sababu za kuharisha kwa mama mjamzito, jinsi ya kudhibiti hali hii, na ushauri wa kitaalamu ni muhimu ili kuhakikisha kuwa ujauzito unaendelea vizuri. Kwa kufuata vidokezo vya afya, mapendekezo ya lishe, na kutafuta msaada wa kitaalamu, mama wajawazito wanaweza kupunguza hatari na kuhakikisha afya bora kwao na kwa mtoto wao.

0 Comment

Mama mjamzito anatakiwa alale vipiAfyaclass Forum •

Mama mjamzito anatakiwa alale vipi

Staili za kulala kwa mama mjamzito,Soma hapa kufahamu

Inaweza isiwe mara ya kwanza kwako kusikia kwamba,si kila staili ya kulala ni nzuri kwa mama mjamzito,

huenda ukawa umesikia mama mjamzito akilala sana chali atagandamiza mshipa mkubwa wa damu uonapita eneo la mgongoni na kusababisha mzunguko mbaya wa damu, mtoto kukosa hewa,chakula na hata kupoteza maisha.

Ni kweli kabsa sio kila staili ya kulala ni nzuri na salama kwa mama mjamzito, na Leo tunakuchambulia baadhi ya staili za kulala kwa mama mjamzito;

Staili za kulala kwa mama mjamzito

✓ Ulale ubavu wa Kushoto Au Kulia?

Siku zote madaktari wanashauri kina mama wajawazito kulala ubavu mmoja hasa upande wa kushoto ili kuepuka kuzaa mtoto mfu au mtoto mwenye uzito mdogo kwa sababu mwanamke mjazito anapolalia ubavu wake wa kushoto huongeza mzunguko wa damu kwa kiumbe kilichomo ndani yake.

Ukweli ni kwamba, Kulala upande wa kushoto wakati wa ujauzito huwezesha mtiririko mzuri wa damu na kuhakikisha kwamba viungo muhimu na mtoto hupokea virutubisho na oksijeni.

Sleeping on the left side during pregnancy facilitates blood flow, ensuring that vital organs and the baby receive the nutrients and oxygen. 

Pengine wajiuliza namna gani sahihi ya kulala kwa mjamzito? Wakati wa ujauzito madaktari wanapendekeza zaidi ulae kwa ubavu hasa kama mimba yako imeshakuwa kubwa. Hii ni kwasababu ya kuepuka kubonyeza mshipa mkubwa wa damu na kuzuia mtiririko mzuri wa damu inayozunguka kuelekea kwenye kizazi.

Kulala Kwa Ubavu wa Kushoto

Kulala kwa ubavu wa kushoto ni mkao sahihi zaidi kwa mama mjamzito ikilinganishwa na staili zingine za kulala kwa mjamzito. Kwasababu mkao huu unaruhusu mzunguko mzuri wa damu kutoka kwenye moyo wa mama kuelekea kwa mtoto.

Kulala kwa ubavu wa kushoto pia kunapunguza mgandamizo kwenye ini na figo. Hii itasaidia kupunguza kuvimba kwa vidole vya mikono , miguu na kwenye enka.

Je ni kweli Kulala Upande flani Ni kigezo cha Jinsia ya Mtoto?

Unaweza kuwa umesikia tetesi kwamba mwanamke akipenda kulalia upande flani basi ni jinsia fulani ya mtoto. Hii ni tetesi tu haina ukweli wowote. Hakuna utafiti wowote unaoonesha ukweli wa jambo hili.

Miezi Mitatu Ya Kwanza Ya Ujauzito(First Trimester)

Kipindi hiki unaruhusiwa kulala kwa namna yoyote, aidha kwa ubavu wa kushoto, kulia, kulalia tumbo au hata mgongo. Lakini kama unataka kujizoesha mapema kwa ajili ya baadae basi anza kulala kwa kuweka mto katikati ya miguu yako. Hii itakusaidia ufurahie usingizi na usipate kashkashi zozote.

Miezi Mitatu Ya katikati ya ujauzito(Second trimester)

Kadiri tumbo linavoongezeka utahitaji kupata godoro imara ambalo halibonyei sana kujizuia mgongo kujikunja sana unapolala. Endelea kutumia mto katikati ya miguu.

Miezi mitatu ya mwisho(Third trimester)

Endelea kutumia mto kukupa sapoti katika miezi hii ya mwisho kuelekea kujifungua. Katika kipindi hiki pendelea zaidi kulala kwa ubavu wa kushoto. Na mara chache lala kwa ubavu wa kulia, hakikisha pia unaweka mto mwingine eneo la kichwa liwe juu kidogo.

✓ Kulala Chali je ni Sahihi na Salama?

Wanawake wajawazito wanaopenda kulala chali wapo kwenye hatari ya kuzaa mtoto mfu(stillbirth),kulingana na wanasayansi. Katika utafiti uliofanyika nchini Ghana, wanawake wajawazito ambao walipenda kulala chali wakati wa ujauzito walikuwa kwenye hatari mara tano zaidi ya kuzaa watoto wenye uzito mdogo na kwa wanawake wengine walizaa watoto wafu.

Utafiti huu ulifanyika nchini Ghana kutokana na kuwa kati ya watoto 1000 wanaozaliwa 20 hadi 50 kati yao hufariki dunia. Hata hivyo, utafiti mpya uliofanyika nchini New Zealand pia umehusisha kulala chali kwa mwanamke mjamzito na idadi kubwa ya watoto kufariki wanaozaliwa katika nchi zenye raia wenye kipato kikubwa.

✓ Kulala kwa Tumbo ni Salama?

Pengine umekuwa ukijiuliza vipi naweza kulala kwa tumbo nikiwa na mimba na isilete madhara yoyote? Jibu ni ndio unaweza kulala kwa tumbo kwa week 16 za kwanza za mimba. Kadiri mimba inavokuwa kubwa wewe mwenyewe itakushinda kulala na tumbo na itabidi ubadili mkao.

Usiwe na hofu kwamba mimba itaharibika pengine ikitokea kwa bahati mbaya umelala na tumbo. Mtoto analindwa na majimaji ya amniotic fluid kwenye chupa yake.

✓ Kulala kwa Mgongo

Kulala kwa mgongo ni salama ukiwa kwenye miezi mitatu ya mwanzo. Baada ya hapo kulala kwa mgongo itakuwa siyo salama kwani itasababisha upate matatizo ya maumivu chini ya mgongo, bawasili, matatizo ya tumbo na pia damu kutozunguka vizuri inavotakiwa.

Ikitokea mara chache usiku ukajisahau na kulala kwa mgongo basi usiwe na hofu badilisha tu mkao na maisha yaendelee vizuri mpaka ukishajifungua.

Ni matumaini yangu umejifunza na kuelewa vizuri kuhusu Staili za kulala kwa mama mjamzito.... Mungu akujalie Uzazi Salama, na Ujifungue salama katika Safari hii....!!!!!!!

1 Comment

Dalili za hatari kwa mama mjamzito ni zipiAfyaclass Forum •

Dalili za hatari kwa mama mjamzito ni zipi

Moja ya Vitu ambavyo Wakina mama Wajawazito hupewa ELIMU wanapohudhuria kliniki kuanzia Siku ya Kwanza ni Pamoja na kufundishwa Kuhusu Dalili za hatari wakati wa Ujauzito(Danger Signs),

Ukiwa unafahamu Dalili za hatari wakati wa Ujauzito itasaidia sana Kuchukua hatua Mapema Pale unapoona Viashiria vya hatari kwenye Ujauzito wako.

Kwa hali ya Kawaida,Asilimia kubwa ya Mahudhurio ya Kliniki huwa Manne,lakini mabadiliko hutokea kulingana na hali ya Ujauzito wako,

Hivo basi,Mahudhurio ya kliniki huweza kuzidi MANNE(4) kulingana na Hali ya Ujauzito wako

MAHUDHURIO MANNE YA KLINIKI

  1. Hudhurio la Kwanza:Ujauzito ukiwa na umri wa kabla ya wiki 16, Lakini kila hospital huweza kuweka utaratibu wao wa Muda wa kuanza Hudhurio la kwanza la kliniki, Ila Protocol,Baada tu ya kuwa Mjamzito unatakiwa kuanza kliniki
  2. Hudhurio la Pili: Ujauzito ukiwa na wiki 20 mpaka 24
  3. Hudhurio la Tatu: Ujauzito ukiwa na wiki 28 mpaka 32
  4. Hudhurio la Nne: Ujauzito ukiwa na wiki 36 Mpaka 40

Ziko dalili nyingi ambazo zinaweza kumpata mama mjamzito na iwapo utaona dalili hizi ni vyema ukafika katika kituo cha kutolea huduma mapema iwezekanavyo.

Ziko jamii za watu ambazo zimekuwa zikichukulia dalili hizi kama hali ya kawaida na wengine wamekuwa wakijitibia nyumbani pasipo kujua madhara yanayoweza kutokea iwapo hatua stahiki hazitachukuliwa.

Je Dalili za Hatari ni Zipi?

1 Kuvuja damu Ukeni

2. Mwili kutetemeka au kupata convulsions/fits

3. Kupata Maumivu makali sana ya kichwa

4. Pamoja na macho kuona marue rue

5. Kuwa na Homa kali

6. Kupata maumivu makali sana ya Tumbo

7. Kuvimba sana miguu,uso Pamoja na mikono.

HIZI HAPA NI BAADHI YA DALILI ZA HATARI WAKATI WA UJAUZITO

1. Mama mjamzito Kuishiwa nguvu au kushindwa/kukosa nguvu za kutoka kitandani

2. Changamoto ya upumuaji (kuhema haraka haraka au kukosa pumzi)

3. Dalili zote za Degedege

4. Dalili zote za kifafa cha mimba kama vile;

  • mjamzito kuona marue rue
  • mjamzito kuvimba sana miguu,mikono na uso
  • mjamzito kuumwa sana na kichwa
  • presha kuwa juu sana pamoja na uwepo wa protein kwenye mkojo n.k

5. Homa kali au joto la mwili kuwa juu sana

6. Maumivu makali ya tumbo

7. Kupungua kwa kucheza kwa mtoto tumboni kusiko kwa kawaida. Au mtoto kuacha kucheza kabisa.

8.Chupa ya uzazi kupasuka kabla ya wakati yaani premature rupture of membrane

8. Maumivu makali ya kichwa na nuru hafifu

9. Kutokwa na damu ukeni

10. Kuvimba vidole, uso na miguu sana

11. Kutapika sana na kukosa hamu ya kula

N.K

Kila mama mjamzito pamoja na mwenza wake wana haki ya kupata elimu juu ya dalili hizi na iwapo wataziona basi ni vyema wakafika katika kituo cha afya ili kuokoa maisha ya mtoto tumboni pamoja na maisha ya mama mjamzito.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Forum Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Forum ASANTE.
UNDERSTOOD