Showing posts with label Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI). Show all posts
Showing posts with label Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI). Show all posts

WATOTO 25 wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi wafanyiwa UPASUAJIAfyaclass Bongo Social •

WATOTO 25 WENYE VICHWA VIKUBWA NA MGONGO WAZI WAFANYIWA UPASUAJI AWAMU YA KWANZA YA KAMBI YA MATIBABU MOI

Na Abdallah Nassoro-MOI

Watoto 25 wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi wamefanyiwa upasuaji katika awamu ya kwanza ya kambi ya upasuaji inayoendelea Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI), iliyoratibiwa na MOI kwa ushirkiano na chama cha wazazi wenye watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi Tanzania (ASBATH) chini ya ufadhili wa taasisi ya MO Dewji Foundation.

Daktari bingwa wa Mbobezi wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu MOI Dkt. Hamisi Shabani amesema watoto hao ni kati ya 50 wanaotarajiwa kufanyiwa upasuaji katika kambi hiyo ya matatibu.

“Jumla ya watoto wote katika mpango huu ni 50, katika awamu hii ya kwanza ya upasuaji watoto 25 wamefanyiwa upasuaji na Mei, 4, 2024 watoto 25 waliobakia watafanyiwa upasuaji ili kukamilisha malengo ya kambi hii” amesema Dkt. Shabani ambaye pia ni mratibu wa kambi hiyo na kuongeza kuwa

“Watoto hawa wanafanyiwa upasuaji kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu ya upasuaji wa kutumia matundu, ETV, upasuaji ambao humfanya mgonjwa kuruhusiwa kurudi nyumbani ndani ya siku chache tangu kufanyiwa upasuaji”

Amesema bado tatizo la vichwa vikubwa na mgongo wazi ni kubwa hapa nchini ambapo takwimu zinaonesha kuwa watoto 7500 wanazaliwa na tatizo hilo ila mwaka.

“Sisi MOI kwa mwaka jana tuliweza kuwafanyia upasuaji watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi 800 hii inaonesha bado kuna wimbi kubwa la watoto ambao hawajapata matibabu”

Kwa upande wake Mratibu wa Miradi wa MO Dewji Foundation Amina Ramadhani amesema lengo la msaada huo ni kuwawezesha watoto hao kupata matibabu ili waweze kurejea katika hali zao za kawaida.

“Maisha ya kila mtu ni muhimu, iwapo kutakuwa na ongezeko la watoto zaidi ya 50 tutaangalia namna ya kuwasaidia ingawa lengo la mwaka huu lilikuwa watoto 50, tunawashukuru MOI na chama cha wazazi wenye watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi (ASBATH)”

Merina Damon na Mohamed Hamisi ni wazazi wa watoto wenye vichwa vikubwa waliofanyiwa upasuaji wameishukuru MOI, chama cha wazazi wenye watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi (ASBATH) MO Dewji Foundation kwa msaada wa matibabu hayo.

WATOTO 25 wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi wafanyiwa UPASUAJI
0 Comment

WATOTO 50 wenye tatizo la Vichwa vikubwa na Mgongo wazi watafanyiwa upasuaji bureAfyaclass Bongo Social •

DAR ES SALAAM; WATOTO 50 wenye tatizo la Vichwa vikubwa na Mgongo wazi watafanyiwa upasuaji bure katika kambi maalum itakayofanyika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI).

Kambi maalum ya upasuaji huo Itafanyika kwa kwa awamu mbili, ambapo awamu ya kwanza itafanyika Aprili 20 na ya pili mwezi Mei.

Akizungumza leo Mkurugenzi wa Idara ya Upasuaji MOI, Dk Lemeri Mchome amesema wamekuja na mkakati ambao utahakikisha huduma hiyo inawafikia watoto wengi ambao hawajaipata.

“Tumepanga kufanya kambi ya upasuaji tarehe 20 Aprili na Mei, itatanguliwa na kliniki kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa watoto na kuwapanga kwa ajili ya kambi,” amesema.

Amesema MOI kwa kushirikiana na wadau wanafanya huduma hiyo, wakiwemo chama cha wazazi wenye watoto hao na MO Dewji Foundation.

“Kwa niaba ya Watanzania tunawashukuru kwa kuamua kuwasaidia watoto waliopata changamoto, tumeona kwa sasa watoto wapate huduma wote wengine wanakuja na kushindwa kupata matibabu kwa ajili ya fedha tuko na timu nzima kuhakikisha huduma endelevu na jumuishi,”ameeleza.

Mwakilishi wa MO Dewji Foundation, Amina Ramadhani amesema wamepanga kusaidia watoto hao kabla na baada ya kufanyiwa upasuaji.

“Kuanzi vipimo na gharama za upasuaji na kufuatilia baada ya huduma na tutawasaidi watoto hawa kwa kipindi cha mwaka tutafatilia hapa MOI na kutoa gharama zote wapate huduma.

Amesema ili kufanikisha hilo watasaidiana kuleta watoto kutoka mikoa ya Iringa, Dodoma na Tanga huku wazazi wakipewa nauli na malazi kwa kushirikiana na ASBATH.

“Kuna watoto ambao wanatoka mikoani kama 25 hivi na wazazi wao hawana uwezo wa kuja, watawezeshwa ili waweze kufika wataandaliwa makazi na ASBATH na tutawasaidia kupata chakula.

Aidha MKurugenzi wa Chama cha Wazazi wa Wwatoto Wenye ulemavu wa Kichwa kikubwa na Mgongo wazi(ASBATH), Suma Mwaipopo amewashukuru wote kwa ushirikiano kwa ajili ya kambi na kuwasihi wazazi kutoka mikoa yote wasikose kwa faida yao.

WATOTO 50 wenye tatizo la Vichwa vikubwa na Mgongo wazi watafanyiwa
upasuaji bure
0 Comment

komwe ni nini? na chanzo chake kikubwa ni kipi?Afyaclass Bongo Social •

komwe ni nini? na chanzo chake kikubwa ni kipi?

Huko mtaani kwa sasa ni kitu cha kawaida kusikia Watu wakitaniana kuhusu komwe ‘varanda ya uso’ au kukuta utani na comments kuhusu komwe mitandaoni,

lakini je umewahi kukutanishwa na Mtaalamu akalielezea komwe lenyewe na sababu zinazolisababisha ?

Sababu za kuwa na Komwe

Daktari Bingwa wa ubongo, mgongo, uti wa mgongo na mishipa Doctor Max Gama Ndosi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) anasema zipo sababu nyingi za kitaalamu ambazo zinasababisha Binadamu awe na komwe ambapo kuna sababu za kawaida na kuna nyingine ni kubwa au zinazotokana na magonjwa.

“Sababu za kuwa na komwe ni nyingi lakini kubwa zaidi ni maumbile,

tunatofautiana tulivyoumbwa kwahiyo unakuta wengine ni jinsi tu Familia zao zilivyo wana vichwa vikubwa na wana uwanda mpana wa uso wao kwahiyo wanaonekana kama wanakomwe lakini kuna sababu nyingi za kitaalamu zinazosababisha komwe’ ——— Dr. Gama.

“Moja ya sababu ni kuwa unaweza kuwa na homoni… katika zile ogani ambazo zinatengeneza homoni kwenye mwili wako mojawapo inaweza kutengeneza homoni ya ukuaji ikawa kubwa kuliko kawaida,

hiyo itafanya mifupa yako ikue kwa haraka na pia sehemu nyingine zifunge kwa haraka kwahiyo utakuta hawa Watu wanamifupa mikubwa sana ya uso, viganja vikubwa, pua kubwa, nyayo kubwa… hii ni kutokana na hii homoni ambayo ni kichocheo” – Dr. Gama.

komwe ni nini? na chanzo chake kikubwa ni kipi?
0 Comment

Wengine 9 kufanyiwa Upasuaji wa kuondoa Uvimbe kwenye UbongoAfyaclass Bongo Social •

Wengine 9 kufanyiwa Upasuaji wa kuondoa Uvimbe kwenye Ubongo.

WAGONJWA 9 KUFANYIWA UPASUAJI MPYA WA KUONDOA UVIMBE KWENYE UBONGO.

Na Abdallah Nassoro-MOI

Madaktari bingwa wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) kwa kushirikiana na madaktari bingwa wabobezi kutoka Chuo Kikuu cha Colorado cha nchini Marekani wanatarajia kuwafanyia upasuaji wagonjwa Tisa wenye matatizo ya uvimbe kwenye Ubongo kwa njia ya kisasa ya kutoboa tundu ndogo bila ya kufungua fuvu katika kambi ya mafunzo ya wiki moja inayoendelea MOI jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo wa tatu wa kimataifa wa mafunzo ya matibabu ya kisasa upasuaji wa uvimbe kwenye ubongo yanalenga kubadilishana uzoefu na kuwajengea uwezo madaktari bingwa wazawa, wauguzi wabobezi na wataalam wengine umefunguliwa leo Februari, 19, 2024 na na muwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt. Lemeri Mchome.

“Mwaka 2017 tulianza upasuaji wa uvimbe vya chini ya ubongo(Pituitary tumors) bila kupasua fuvu kwa mara ya kwanza. Madaktari wa MOI baada ya mafunzo na mashirikiano hayo wameendelea na upasuaji huo mpaka sasa kwa ufanisi mkubwa…

Kwa sasa hapa MOI takribani wagonjwa 572 tunawafanyia upasuaji wa vivimbe kwenye ubongo na karibia asilimia nne ya wagonjwa hawa bado wanaenda nje ya nchi kupata matibabu kwa vivimbe vilivyo ndani kabisa ya ubongo ambapo upasuaji wa kawaida unaweza kuleta madhara zaidi.

Hivyo mafunzo haya yatasadia uanzishwaji wa huduma hii mpya ya upasuaji wa uvimbe ndani ya ubongo (Stereotactic procedures).

Wengine 9 kufanyiwa Upasuaji wa kuondoa Uvimbe kwenye Ubongo
0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Bongo Social Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Bongo Social ASANTE.
UNDERSTOOD