Showing posts with label Ugonjwa wa fistula. Show all posts
Showing posts with label Ugonjwa wa fistula. Show all posts

Ugonjwa wa fistula kwa wanaume,chanzo,dalili na TibaAfyaclass Forum •

 Ugonjwa wa fistula kwa wanaume,chanzo,dalili na Tiba

Watu wengi hawajui kwamba Ugonjwa wa Fistula sio kwa Wanawake pekee, hata wanaume wanaweza kupata Ugonjwa wa Fistula,

Ugonjwa wa fistula ni nini?

Ugonjwa wa Fistula huhusisha kuwepo kwa tundu au uhusiano usio wa kawaida kati ya sehemu mbili za mwili, kama vile kiungo kimoja na kingine,mishipa ya damu,tishu na tishu n.k.

Zipo aina mbali mbali za fistula kama vile;

  • Vesicovaginal fistula(kwa wanawake)
  • Uterovaginal fistula(kwa wanawake)
  • Anal fistula(Kwa wote) n.k

Fahamu kwamba,Hata Wanaume huweza kupata Fistula, na Leo tunachambua zaidi kuhusu Ugonjwa wa fistula kwa wanaume,chanzo,dalili na Tiba yake.

Anorectal fistula ni aina ya fistula ambayo hutokea zaidi kwa wanaume kuliko kwa wanawake, Ingawa fistula aina ya anorectal inaweza kutokea kwa watu wa umri wowote na jinsia yeyote.

Chanzo cha Ugonjwa wa fistula kwa wanaume

Kama tulivyokisha kueleza wanaume hupatwa Zaidi na fistula aina ya Anorectal fistula,

na kwa asilimia kubwa aina hii ya anal fistula husababishwa na maambukizi ya vimelea vya magonjwa ambayo huanza ndani ya tezi linalojulikana kama anal gland,

Maambukizi haya husababisha jipu ambalo hutoka lenyewe au kutolewa kwa upasuaji kupitia ngozi karibu na njia ya haja kubwa.

Sababu zinazoongeza hatari ya Mtu kupata anal fistula

Sababu zinazoongeza hatari ya Mtu kupata fistula aina ya anal fistula ni pamoja na;

1. Kuwa na Jipu eneo la haja kubwa lililotolewa hapo awali

2. Kuwa na magonjwa kama vile;

  • Crohn's disease
  • Au inflammatory bowel disease n.k

3. Kuumia eneo la haja Kubwa

4. Kupata maambukizi ya vimelea vya magonjwa sehemu ya haja kubwa

5. Kufanyiwa upasuaji eneo la haja kubwa

6. Upasuaji au mionzi kwa ajili ya matibabu ya saratani ya eneo la haja kubwa(anal cancer) n.k

Dalili za anal fistula

Dalili za anal fistula ni pamoja na ;

- Kupata muwasho kuzunguka eneo la haja kubwa

- kupata maumivu eneo la haja kubwa ambayo ni endelevu na yanayozidi wakati wa;

  • kukaa,
  • kutembea,
  • kujisaidia haja kubwa
  • au kukohoa

- Kutokwa na uchafu wenye harufu mbaya eneo karibu na njia ya haja kubwa

- Kutokwa na damu au Usaha wakati wa kujisaidia haja kubwa

- Kupata Homa hasa pale ukiwa na jipu n.k

-  Eneo la kuzunguka njia ya haja kubwa kuvimba na kubadilika rangi na kuwa jekundu n.k

- Kushindwa kudhibiti haja kubwa, na kutoka pasipo kujizuia wewe mwenyewe.n.k

Matibabu ya Ugonjwa wa Fistula kwa Wanaume

Matibabu ya Ugonjwa wa Fistula hutegemea na chanzo chake, ila kwa ujumla mgonjwa huweza kupata matibabu ya;

  • Upasuaji
  • Pamoja na Dawa mbali mbali

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comment

Story: Tatizo la Fistula ya uzazi na Bi. MbonimpaAfyaclass Forum •

Story: Tatizo la Fistula ya uzazi na Bi. Mbonimpa

Bi. Mbonimpa ambaye enzi za ujana wake alikumbwa na tatizo la Fistula ya uzazi anaeleza kuwa alihisi kifo kinakaribia siku aliyoshikwa na uchungu wa kujifungua, alipiga kelele kuita majirani zake kwa msaada,

walijaribu kumpeleka kwenye kituo cha matibabu lakini haikuwa heri kwake, alijifungulia njiani mtoto akiwa amefariki, na kupata fistula ya uzazi katika mchakato huo.

Fistula ya uzazi ni majeraha ya kujifungua ambayo husababishwa hasa na uzazi uliokwamishwa kwa muda mrefu.

Duniani kote, majeraha haya huathiri karibu nusu milioni ya wanawake na wasichana hasa wale ambao wanakosa Msaada wa huduma ya MATIBABU ya haraka na yenye ubora wa juu.

Matokeo ya ugonjwa wa fistula kwa mhanga yanaweza kuwa mabaya kwani mara nyingi hawaheshimiki katika jamii na hutengwa pamoja na kuwa na umasikini wa kiwango cha juu.

Unyanyapaa

“Wanawake katika wodi ya uzazi waliniomba niondolewe katika wodi hiyo kwasababu nilikuwa nikilowanisha kitanda, mbali na maumivu ya kupoteza mtoto, nilikuwa sielewi nini kinanitokea katika Maisha yangu” Donavine Ndayikengurukiye, mwanamke mwingine aliyepona fistula, aliliambia UNFPA.

Kutokana na aibu aliyoipata kutokana na Fistula, mume wa Bi. Mbonimpa alimtelekeza kwa sababu ya kushindwa kuvumilia hali hiyo. “Nilikuwa natoa harufu isiyovumilika, hakuna anayestahili kupitia haya” alisema Bi. Mbonimpa

Fistula inatibika, licha ya hayo, utafiti unaonesha kuwa wahanga wengi hawajui kuwa upasuaji unaweza kusaidia kuponya majeraha hayo.

Mwanzoni, Bi. Ndayikengurukiye alikuwa mmoja wao, lakini kugundua kwake kuwa anaweza kupona ikaleta tabasamu mpya usoni mwake.

Nchini Burundi, kituo kimoja cha afya, kituo cha Urumuri kilichoko katika mji mkuu wa Burundi, Bujumbura, kina vifaa vya kushughulikia wagonjwa wa fistula.

Kati ya mwaka 2010 na 2023, wanawake takribani 3,000 walifanyiwa upasuaji wa kurekebisha hali zao kituoni hapo. Bi. Mbonimpa alikuwa mmoja wao.

Mwaka 2022, alitafuta matibabu katika kituo hicho wakati wa kampeni iliyoungwa mkono na UNFPA iliyotoa fursa ya huduma bure kwa wahanga wa ugonjwa wa fistula.

Wanawake walio katika umri wa kubalehe wanaweza kuwa katika hatari ya kupata fistula, kwani mifupa yao ya nyonga haijakomaa vya kutosha kwaajili ya kujifungua.

“Nadhani nilipata hii fistula kwasababu nilijifungua nilipokuwa mdogo sana” Bi. Ndayikengurukiye aliliambia UNFPA

Ni miaka 23 sasa Bi. Ndayikengurukiye anaishi bila fistula, akiwa ni mama wa msichana mdogo ambaye alizaliwa baada ya kupona kwake, tangu wakati huo, yeye na mumewe wamekubali kufuata huduma ya uzazi wa mpango.

“Mume wangu na mimi tulichagua uzazi wa mpango ili mwili wangu upate kupumzika kutoka katika hatari ya kupata fistula ya uzazi nyingine, na kusubiri msichana wetu mdogo aweze kukua kidogo”

Story: Tatizo la Fistula ya uzazi na Bi. Mbonimpa
0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Forum Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Forum ASANTE.
UNDERSTOOD