Showing posts with label featured. Show all posts
Showing posts with label featured. Show all posts

Angalizo utoaji wa Dawa za Semaglutides,baada ya dawa bandia kuongezekaAfyaclass Forum •

Hii ni notisi ya kwanza rasmi iliyotolewa na WHO baada ya kuthibitisha baadhi ya ripoti hizo.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari WHO imeeleza kuwa tahadhari hiyo ni kwa ajili ya makundi matatu ya bidhaa ya Semiglutide hususan kwa chapa ya Ozempic ambayo wameeleza imegundulika huko nchini Brazili mwezi Oktoba 2023, Uingereza na Ireland Kaskazini mwezi Oktoba 2023, na Marekani mwezi Desemba 2023.

Mfumo wa Ufuatiliaji na Uangalizi wa WHO (GSMS) umekuwa ukiangalia ongezeko la ripoti kuhusu bidhaa zisizo halisi (feki) za semaglutide katika maeneo yote ya kijiografia tangu mwaka 2022.

Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa WHO wa Upatikanaji wa Dawa na Bidhaa za Afya Dkt. Yukiko Nakatani

Amewashauri wataalamu wa afya na mamlaka za udhibiti na umma kufahamu kuhusu makundi haya ya dawa zisizo halisi, “Tunatoa wito kwa wadau kuacha matumizi yoyote ya dawa zinazotiliwa shaka na kutoa taarifa kwa mamlaka husika”.

Uhaba wa dawa wachangia bidhaa bandia

Dawa hizi za Semaglutides, pamoja na bidhaa maalum za chapa ambayo si halisi zinatolewa kwa wagonjwa wa kisukari cha aina ya 2 ili kupunguza viwango vyao vya sukari kwenye damu. Semaglutides pia hupunguza hatari ya magonjwa ya moyo na mishipa.

Bidhaa nyingi za semaglutide zinapaswa kudungwa chini ya ngozi kila wiki lakini pia zinapatikana kama vidonge vya kumeza kila siku.

Katika nchi nyingine dawa hizi zimeonesha kupunguza hamu ya kula pamoja na kupunguza viwango vya sukari ya damu, na kwa hivyo zinazidi kuagizwa kwa ajili ya matumizi ya kusaidia kupunguza uzito wa mwili kwa watu.

WHO imekuwa ikifuatilia kwa ukaribu ongezeko la mahitaji ya dawa hizi pamoja na ripoti kuhusu bidhaa bandia. Bidhaa hizi zisizo halisi zinaweza kuwa na madhara kwa afya ya watu; dawa bandia zinaweza kusababisha matatizo makubwa ya kiafya.

Katika hali nyingine, kiungo tendaji ambacho hakijatangazwa kinaweza kuwa kwenye kifaa cha sindano, kama insulini, na kusababisha anuwai isiyotabirika ya hatari za kiafya au shida.

Semaglutides si sehemu ya matibabu yanayopendekezwa na WHO kwa ajili ya udhibiti wa kisukari kutokana na gharama yake kuwa ya juu kwa sasa. Kizuizi cha gharama kinafanya bidhaa hizi kutofaa kama mbinu ya afya ya umma.

Pia, kuna matibabu ya bei nafuu zaidi yanayopatikana kwa ugonjwa wa kisukari, na yana matokeo sawa na yale ya semaglutides kwenye sukari ya damu na hatari ya moyo na mishipa.

Wito kwa watu wote

Ili kujilinda dhidi ya dawa zisizo halisi na madhara yake, wagonjwa wanaotumia bidhaa hizi wanaweza kuchukua hatua kama vile kununua dawa kutoka kwa madaktari walio na leseni na kuepuka kununua dawa kutoka kwa vyanzo visivyojulikana au ambavyo havijathibitishwa.

Watu wanapaswa kuangalia vifungashio na tarehe za mwisho wa matumizi ya dawa wanapozinunua, na watumie bidhaa kama ilivyoelekezwa.

Watumiaji wa semaglutides ya sindano, wanapaswa kuhakikisha kuwa wamehifadhiwa kwenye jokofu.

Iwapo utagundua dawa uliyonunua ni bandia unaweza kuwajulisha WHO kupitia barua pepe rapidalert@who.int.

Angalizo utoaji wa Dawa za Semaglutides,baada ya dawa bandia kuongezeka
0 Comment

Faida za karafuu,Soma hapa kufahamuAfyaclass Forum •

Faida za karafuu,Soma hapa kufahamu

Katika Makala hii tumekuandalia faida za karafuu ambazo pengine ulikuwa huzijui kabsa, Kwa kweli, utafiti unaonyesha kwamba karafuu inaweza kuwa na manufaa kadhaa ya afya, ikiwa ni pamoja na kusaidia afya ya ini na kusaidia kuweka Sawa Kiwango cha sukari kwenye damu.

Hapa tumekuchambulia Faida Kadhaa za Karafu ambazo pengine ulikuwa huzifahamu kabsa;

1. Karafuu ina virutubisho muhimu sana mwilini ikiwemo;

  • nyuzi nyuzi(fiber),
  • Vitamins,
  • Pamoja na Madini

Tafiti zinaonyesha kijiko kimoja cha Karafuu huweza kutoa;

Calories: 6
Carbs: 1 g
Fiber: 1 g
Manganese: 55% of the Daily Value (DV)
Vitamin K: 2% of the DV

Madini ya Manganese ni muhimu sana kwenye kusaidia afya ya na utendaji kazi wa Ubongo pamoja na kujenga Mifupa Imara.

2. Karafuu ina kiwango kikubwa cha antioxidants;

Mbali na kusheheni Vitamins na madini,Pia Karafuu ina antioxidants za kutosha,

Antioxidants hizi husaidia kupunguza uwezekano wa mtu kupata magonjwa ya Muda mrefu yaani chronic disease.

Mfano wa antioxidants muhimu sana ndani ya Karafuu ni hii inaitwa eugenol,

Hivo hii husaidia kuboresha afya ya Mwili kwa Ujumla.

3. Karafuu huweza kusaidia kuboresha afya ya Ini

Antioxidants kama vile eugenol husaidia kuzuia uharibifu wa Ini dhidi ya viambato vya Sumu kama vile thioacetamide.

Ingawa pia,Matumizi ya Karafuu kwa kiwango kikubwa sana huweza kuleta athari kwenye Ini.

#Soma Zaidi Madhara ya Karafuu Mwilini,Hapa

4. Karafuu huweza kukulinda dhidi ya Saratani,

Baadhi ya Tafiti zinaonyesha Mafuta ya Karafuu husaidia ulinzi dhidi ya Saratani, Hasa hasa kwa Sababu ya antioxidants hii ya eugenol,

Tafiti zinaonyesha eugenol huzuia Saratani ya matiti kwa kuhamasisha Zaidi seli zenye Saratani kufa Zaidi na kuacha zile zenye afya.

5. Karafuu huweza kuua Viini vya magonjwa kama vile bacteria,

Karafuu zina tabia ambayo kitaalam tunasema antimicrobial properties, hii ina maana Karafuu huweza kuzuia ukuaji wa viini vya magonjwa kama vile bacteria.

Hivo basi,Kwa kujumuisha na njia nyingine za Usafi wa kinywa karafuu huweza kusaidia kwenye afya ya Kinywa na Meno, kama ukiitumia wakati wa kusafisha kinywa.

6. Karafuu huweza kusaidia kuweka Sawa kiwango cha Sukari kwenye damu,

Karafuu inaweza kusaidia kudhibiti kiwango cha sukari kwenye damu,
Misombo inayopatikana kwenye karafuu inaweza kusaidia kudhibiti sukari kwenye damu.

Kwa mfano, katika utafiti uliofanyika mwaka 2019 watu walio na prediabetes na wasio na ugonjwa wa kisukari ambao walitumia miligramu 250 (mg) ya karafuu kila siku kwa siku 30 walionyesha kiwango kidogo cha sukari kwenye damu baada ya kula.

Katika utafiti mwingine wa wanyama, nigricin, kiambato kinachopatikana kwenye karafuu, kiligundulika kuongeza uchukuaji wa sukari kutoka kwenye damu hadi kwenye seli, kuongeza utolewaji wa insulini, na kuboresha utendaji kazi wa seli zinazozalisha insulini kwenye panya.

7. Karafuu huboresha afya ya Mifupa,

Tatizo la Low bone mass ambalo hupelekea shida ya mifupa inayojulikana kama osteoporosis huwapata watu wengi, Mfano kwa nchi tu kama Marekani,inakadiriwa watu takribani Million 43 hupata shida hii kwa mujibu wa utafiti uliofanyika mnamo mwaka 2014.

Lakini, Tafiti zilizofanyika kwa wanyama,zilionyesha kwamba antioxidant ya eugenol kutoka kwenye Karafuu huweza kuboresha bone mass na kuzuia tatizo hili.

8. Karafuu huweza kusaidia kupunguza Vidonda vya Tumbo,

May reduce stomach ulcers
Tafiti nyingine za wanyama,zilionyesha Faida kubwa ya eugenol kutoka kwenye karafuu hata kwa kutibu Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo.

Hizo Ni baadhi ya FAIDA za KARAFUU tulizokuandalia kwa Siku ya Leo…!!!!

Faida za karafuu,Soma hapa kufahamu
0 Comment

Mtu mmoja amefariki, Na 5 wamelazwa hospitalini huku Kipindupindu kikienea katika Jimbo la Ogun,NIGERIAAfyaclass Forum •

Kipindupindu kimegharimu maisha ya mwanamke mwenye umri wa miaka 62 huko Ijebu-Igbo, eneo la Serikali ya Mtaa ya Ijebu Kaskazini katika Jimbo la Ogun,Nchini Nigeria.

Mwanamke aliyefariki aliambukizwa ugonjwa huo alipokuwa akimhudumia mtoto wake aliyeambukizwa, ambaye sasa amelazwa hospitalini.

Tukio hilo lilisemekana kutokea siku tatu zilizopita.

Akithibitisha kuzuka kwa ugonjwa huo, Dk. Tomi Coker, Kamishna wa Afya, alisema: “Mwanamke mwenye umri wa miaka 62 alikufa na watu watano walilazwa hospitalini. Ilitokea Ijebu-Igbo katika eneo la serikali ya mitaa ya Ijebu-Kaskazini katika jimbo hilo.”

Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari wa Nigeria, NMA, katika jimbo hilo, Dk. Kunle Ashimi, katika mkutano na waandishi wa habari Alhamisi, Juni 20, alikiri kuenea kwa athari za ugonjwa wa kipindupindu, ambao, kulingana naye, umeathiri majimbo 30 kote nchini, ikiwemo Ogun.

Alibainisha kuwa kesi zitatibiwa bila malipo katika vituo vilivyotengwa na kuwataka wananchi kuchukua hatua za kuzuia kuenea kwa kipindupindu.

Ashimi alisema: “Wagonjwa kama hao watasafirishwa na kutibiwa bure katika vituo vilivyotengwa kwa ajili ya kudhibiti kesi za kipindupindu katika jimbo zima.

“Tunatumia fursa hii kuwaomba wananchi wetu kuchukua hatua za kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Kipindupindu ikiwa ni pamoja na kujiepusha na kujisaidia wazi, kuepuka kutupa taka ovyo, kunawa mikono mara kwa mara, kunawa matunda na mboga mboga vizuri kabla ya kula na kutibu maji kabla ya kuyanywa. ama kwa kuchemsha au kutibu kwa mawakala wa kusafisha kemikali.

“Tunatetea kwamba pale ambapo hakuna sababu ya kufanya hivyo, matone mawili ya bleach ya nyumbani katika lita 1 ya maji ni mbadala nzuri. Pia tunazisihi shule kufuatilia wachuuzi wa vyakula, matunda na vitafunwa karibu na shule ili kuhakikisha kuwa wanazingatia usafi. Vile vile, shule zinapaswa kuanzisha tena vituo vya kunawia mikono kama ilivyofanywa wakati wa COVID-19.”

Mtu mmoja amefariki, Na 5 wamelazwa hospitalini huku Kipindupindu
kikienea katika Jimbo la Ogun,NIGERIA
0 Comment

Kuna zaidi ya aina 700 za bakteria zinazojulikana MdomoniAfyaclass Forum •

Je,Wajua Mdomoni Kuna zaidi ya aina 700 za bakteria zinazojulikana?

Fahamu Mdomoni,Kuna zaidi ya aina 700 za bakteria zinazojulikana, pamoja na vimelea vingine kama vile, virusi na protozoa.

Viumbe hivi vyote vinaweza kuonekana tu kwenye maabara, na vina jukumu muhimu katika kulinda afya yako.

Magonjwa ya kawaida yanayosababishwa na bakteria hawa ni kuoza meno na ugonjwa wa fizi.

Baadhi ya Tafiti Zinaonyesha viumbe hivi pia vinahusika na hali nyingine mbaya za afya zinazotokea katika mwili wa binadamu.

Yapo baadhi ya Magonjwa ambayo hutokana na shida hii ya Mdomo,Ikiwemo;

✓ Ugonjwa wa mapafu

Kwa kuwa kuvuta pumzi huanzia mdomoni na kisha kwenye mapafu, haishangazi kwamba baadhi ya viumbe vilivyo kinywani huishia kwenye mapafu.

Na mara nyingi husababisha magonjwa kama vile nimonia, Maambukizi haya hutokana na kutokufanya usafi wa mdomo na kusababisha bakteria kukua.

Kulingana na utafiti, usafi wa kinywa unaweza kupunguza bakteria hawa.

✓ Ugonjwa wa moyo

Moja ya magonjwa yanayosababishwa na viumbe wa mdomoni ni kuoza meno.

Ugonjwa huo ni uvimbe unaosababisha uharibifu wa mfupa wa jino pamoja na mizizi midogo ndani yake, na hatimaye husababisha jino kung’olewa.

Ugonjwa huu husababishwa na bakteria kukua kati ya ufizi na meno, kutokana na kutokufanya Usafi vizuri wa kinywa.

Lakini jambo ambalo limewashangaza watafiti kwa miaka mingi ni uhusiano kati ya ugonjwa wa fizi na ugonjwa wa moyo.

Uhusiano huu unaweza kuwa ni kutokana na mambo kadhaa. Mfano, watu wanaovuta sigara au kemikali za sumu – huwa na ugonjwa wa fizi na ugonjwa wa moyo.

Watafiti wengine pia wameripoti kwamba bakteria katika mifupa ya pua wanaweza pia kusafiri kwenda kwenye moyo, na kusababisha maambukizi. Ingawa hilo bado halina ushahidi wa kutosha.

✓ Matatizo ya kumbukumbu

Moja ya magonjwa ya kushangaza zaidi yanayohusiana na usafi wa mdomo ni kupoteza kumbukumbu.

Madaktari wa kinywa huhusisha usafi wa kinywa na matatizo ambayo husababisha kupoteza kumbukumbu au kuchanganyikiwa.

Mara nyingi matatizo ya kumbukumbu na matatizo ya meno hutokea uzeeni, ni vigumu kuamua ikiwa kuna uhusiano kati ya magonjwa mawili.

Lakini mwaka 2019, kikundi cha watafiti kiliripoti, ubongo wa watu wenye shida ya akili una bakteria wa P gingivalis, ambao ni moja ya bakteria wakuu wanaosababisha ugonjwa wa fizi.

Ingawa wazo kwamba ubongo, ambao ni sehemu safi zaidi katika mwili wa binadamu, huathiriwa na bakteria kutoka kinywani bado linahitaji utafiti zaidi. Halijakubalika na wataalamu wengi.

Pia, ugonjwa wa moyo na kupoteza kumbukumbu kuhusishwa na bakteria kutoka mdomoni, yanahitaji utafiti zaidi.

Ijapokuwa athari za uchafu wa kinywa zinaonekana kuongezeka, habari njema ni kwamba tuna uwezo wa kudhibiti uchafu na kuishi vyema na bakteria waliopo katika vinywa vyetu, na tunaweza kuzuia magonjwa.

Kudumisha usafi wa mdomo ni muhimu. Miongoni mwa mambo unayoweza kufanya ni kupiga mswaki kinywa chako mara mbili kwa siku.

Vilevile kuondoa mabaki ya chakula kati ya meno na fizi na meno mara kwa mara. Haya yanaweza kupunguza kuoza kwa meno na ugonjwa wa fizi.

Via:Bbc

Kuna zaidi ya aina 700 za bakteria zinazojulikana Mdomoni
0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Forum Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Forum ASANTE.
UNDERSTOOD