Showing posts with label jinsi ya kupunguza uzito. Show all posts
Showing posts with label jinsi ya kupunguza uzito. Show all posts

Jinsi ya Kupunguza Uzito kwa Ufanisi: Mbinu Rahisi ZaidiAfyaclass Forum •

Jinsi ya Kupunguza Uzito kwa Ufanisi: Mbinu Rahisi Zaidi

Linapokuja Swala la Uzito,Zipo Makala nyingi na njia nyingi Sana utazikuta mtandaoni zinazohusu kupunguza Uzito, Je zinafanya kazi? na je hazina madhara yeyote?

Kwanza,Ili ujue Una Uzito Mkubwa kupita kiasi ni Lazima upime, na Vipimo vinategemea na nchi au Mahali Ulipo,Kitaalam ukienda kwa ajili ya Checkup za aina hii vitu hivi huweza kufanyika;

  • Kupata historia ya afya yako kwa Ujumla, ikiwemo historia ya uzito wako,njia ulizowahi kutumia kupunguza uzito,aina ya kazi unayofanya,mazoezi,historia ya watu kuwa na Uzito mkubwa kwenye familia yako n.k
  • Vipimo muhimu kama vile,Uzito wako,Urefu wako,Mapigo ya Moyo,Presha,afya ya moyo,mapafu n.k
  • Baada ya Vipimo hivi tunafanya mahesabu ya BMI, Hii sasa ndyo itakuambia Uzito wako umezidi,upo kawaida,au mdogo sana.

#SOMA KWA kina Hapa,Jinsi ya kufanya mahesabu ya BMI,

Baada ya kufanya vyote hivo na Kujua Una shida ya Uzito mkubwa(Overweight), Hapa ndyo tunakuja na njia za jinsi ya kupunguza Uzito wako wa mwili;

Jinsi ya Kupunguza Uzito kwa Ufanisi: Mbinu Rahisi Zaidi

Hapa kuna Vidokezo rahisi vya kufuata,Ingawa tumekuandalia kitabu mfumo wa ebook ambacho ukikipata utafuata hatua Zote kwa Kina na kupunguza Uzito hata ukiwa mwenyewe nyumbani. Kukipata Bofya Hapa.

1. Badilisha aina ya Mlo unaokula

Tafiti zinaonyesha kupunguza kiwango cha calories na kula mlo unaotakiwa kiafya ni NJIA KUU ya kukabiliana na tatizo la Uzito Mkubwa.

Punguza kalori; Njia kubwa ya kupunguza uzito ni kupunguza kalori,Hatua ya kwanza ni kukagua tabia zako za kawaida za kula na kunywa.

Unaweza kuona ni kalori ngapi unazotumia kwa kawaida na wapi unaweza kupunguza. Wewe na mtaalamu wako wa afya mnaweza kuamua ni kalori ngapi unazohitaji kutumia kila siku ili kupunguza uzito. Kiasi cha kawaida ni kalori 1,200 hadi 1,500 kwa wanawake na 1,500 hadi 1,800 kwa wanaume.

Fanya chaguzi bora la Mlo kwa Afya; Unashauriwa kula vyakula vya mimea zaidi yaani plant-based foods. Hapa ni pamoja na MATUNDA,MBOGA ZA MAJANI pamoja na Nafaka nzima,

Pia unashauriwa kula vyanzo bora vya proteins kama vile maharage,soya,nyama,samaki n.k kwa kiwango kidogo.

Dhibiti Matumizi ya chumvi nyingi,Sukari nyingi au Mafuta mengi

Epuka kula vyakula vyenye kiwango kikubwa cha Wanga, vyakula vya Mafuta mengi sana, au Vinywaji vyenye kiwango kikubwa  cha Sukari kama POMBE n.k.

2. Fanya Mazoezi ya Mwili,

Baadhi ya Tafiti zinaonyesha Mtu mwenye Uzito Mkubwa anatakiwa kufanya Mazoezi angalau kwa dakika 150 ndani ya wiki Moja,

Hii inaweza kusaidia kuzuia kupata uzito zaidi au kudumisha upotezaji wa uzito wa kawaida. Pengine utahitaji kuongeza hatua kwa hatua kiasi unachofanya mazoezi kadri ustahimilivu wako unavyoboreka.

3. Mabadiliko ya Kitabia ikiwemo Msongo wa Mawazo

Hapa unaangalia ni vitu gani vinakusababishia Uzito wako kuongezeka,kisha unavibadilisha,

Watu wengi hawafahamu Msongo wa mawazo huweza kusababisha baadhi ya Watu Uzito wao wa mwili kuongezeka kwa kasi sana

#SOMA ZAIDI hapa madhara ya Msongo wa mawazo(Stress)

4. Pata Ushauri kutoka kwa Wataalam

Hii ni hatua muhimu sana,kwani huwezi kupunguza kitu ambacho hukijui,

Hakikisha unapata Maelekezo kutokwa kwa Wataalam au

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE NDANI YA AFYACLASS,HIZI HAPA NI NJIA ZA MAWASILIANO

Jinsi ya Kupunguza Uzito kwa Ufanisi: Mbinu Rahisi Zaidi
0 Comment

Sindano ya kupunguza uzito 'inaweza kupunguza mshtuko wa moyo'Afyaclass Forum •

Sindano ya kupunguza uzito ‘inaweza kupunguza mshtuko wa moyo

Sindano iliyoundwa kukabiliana na unene wa kupindukia inaweza kupunguza hatari ya mshtuko wa moyo na kiharusi kwa watu bila kujali kiwango cha uzito wanachopoteza wakati wa kutumia dawa hiyo, kulingana na utafiti mpya.

Watafiti waliangalia athari za semaglutide, ambayo ni dawa iliyoagizwa na daktari ambayo inapunguza hamu ya kula na inauzwa chini ya majina ya chapa Wegovy, Ozempic na Rybelsus.

Walisema sindano ya kupambana na unene kupindukia inaweza pia kusaidia afya ya moyo na mishipa ya mamilioni ya watu wazima.

Prof John Deanfield, ambaye aliongoza timu ya watafiti, alisema dawa hiyo ya asili inaweza kuwa na athari chanya kwenye sukari ya damu, shinikizo la damu au uvimbe, pamoja na athari za moja kwa moja kwenye misuli ya moyo na mishipa.

Utafiti wa miaka mitano wa Chuo Kikuu cha London (UCL) ulitumia data kutoka kwenye jaribio linaloendeshwa na semaglutide Novo Nordisk, kuchunguza watu wazima 17,604 zaidi ya umri wa 45 kutoka nchi 41.

Akizungumza kabla ya kuwasilisha utafiti huo katika Kongamano la Ulaya kuhusu Unene wa Kupindukia (ECO) huko Venice, Prof Deanfield alisema matokeo hayo yalikuwa na “athari chamga za kiafya”.

Alisema ulikuwa ugunduzi muhimu, akiufananisha na wakati statins zilianzishwa katika miaka ya 1990.

“Hatimaye tuligundua kuwa kulikuwa na dawa ambazo zilibadilisha biolojia ya ugonjwa huu kufaidisha watu wengi. Hayo yalikuwa mafanikio makubwa.

“Sasa tuna aina hizi za dawa ambazo pia zinaweza kusaidia magonjwa mengi sugu ya uzee.”

Sindano ya kupunguza uzito 'inaweza kupunguza mshtuko wa moyo'
0 Comment

jinsi Ozempic, dawa maarufu ya kupunguza uzito inavyosababisha tatizo la wasiwasi, mfadhaiko na vitendo vya kujiuaAfyaclass Forum •

Wataalamu wanaeleza jinsi matumizi ya Ozempic yanavyoonekana kubadilisha haiba ya watu na kupunguza tamaa yao ya dawa za kulevya, pombe na hamu ya tendo.

Wanasayansi wamejitokeza kueleza jinsi Ozempic, dawa maarufu ya kupunguza uzito sasa inavyoathiri haiba ya watu kwa kuwafanya wawe na wasiwasi, mfadhaiko na kukabiliwa na vitendo vya kujiua.

Idadi inaongezeka ya wagonjwa wanaodai kuwa dawa ya GLP-1 na zingine kama hiyo zimesababisha wasiwasi, unyogovu,mfadhaiko na mawazo ya kujiua, hata kama wanapunguza uzito.

Ozempic, na matibabu mengine maarufu kama Wegovy, yana athari kwa viwango vya dopamini, ambavyo vinawajibika kwa anuwai ya utendaji.

Pamoja na kuathiri msukumo wetu wa kihisia na kimwili kwa ajili ya chakula, kemikali ya ubongo huathiri hisia za, furaha, motisha na harakati.

Wanasayansi sasa wanaamini kuwa viwango hivi vinavyobadilika katika dopamini vinaweza kueleza kwa nini baadhi ya watumiaji wamedai kuwa dawa hizo pia zimepunguza hamu yao ya dawa za kulevya, pombe na kufanya ngono.

Dk Kent Berridge, profesa wa saikolojia na sayansi ya neva katika Chuo Kikuu cha Michigan, anasema vitu vyote vya kulevya na chakula huwezesha ishara sawa za dopamini na maeneo ya kujifunza katika ubongo.

“Tamaa ya dawa za kulevya pia inaongezeka pamoja na njaa.” Aliambia Daily Mail.

“Watafiti wanapojaribu kuwafanya wanyama wajifunze kutumia kokeini, mara nyingi watawafanya kuwa wawe na njaa kwa muda kidogo, kwani hii huwasaidia kujifunza,” Dk. Berridge alieleza.

“Njaa inamaanisha unahitaji chakula lakini inaweza kuwa zaidi ya hiyo, njaa inaamsha hamu ya vitu vingi. Ikiwa una njaa, Unakuwa na motisha ya vitu vingi, hata vile ambavyo sio chakula,hamu inaonekana kuongezeka.

Kwa sababu dawa hizi huwasaidia wagonjwa kuhisi kushiba kwa muda mrefu, wataalam wanaamini kwamba pia hupunguza tamaa ya vitu vingine mbali na chakula pia, kama vile dawa za kulevya, ngono na pombe.

“Kushiba kunaweza kuwa sio tu kupunguza hamu ya chakula lakini uwezekano wa mambo mengine,” Dk Berridge alisema.

Dawa za GLP-1 zinaonekana kubadilisha mifumo ya motisha ya dopamini, kudhoofisha lakini sio kuondoa matamanio. Kwa mfano, wagonjwa wamegundua kuwa hawapotezi hamu ya kula lakini hula kidogo wakati wanatumia dawa hizi ambazo wataalam wanaamini kuwa zinaweza kuleta madhara mengine.

Pia Utafiti unaonyesha kwamba unaweza kupata matokeo ya kupungua kwa hamu ya tendo wakati wa kutumia dawa za GLP-1 “inawezekana.”

Dk Berridge alieleza kuwa kwa sababu ngono ni tamaa ya asili ya kufurahisha, kukandamiza njia hizi kunaweza kusababisha kupungua kwa hamu ya kufanya ngono.

“Ikiwa unakandamiza [uwezeshaji wa dopamine] Pia matokeo yake ni kupungua kwa hamu ya kufanya ngono” mtaalam wa matibabu alisema.

Mfumo wa kuripoti matukio mabaya yanayohusu Chakula na Dawa wa Marekani ulipokea ripoti 606 za matatizo ya akili yaliyounganishwa na matumizi ya Ozempic, pamoja na ripoti 324 zilizounganishwa na Saxenda na 190 kwa Wegovy mwaka wa 2023.

FDA inahitaji dawa za kudhibiti uzito zinazofanya kazi kwenye mfumo mkuu wa neva, ikiwa ni pamoja na Saxenda na Wegovy, ziwe na onyo kali.

Mwandishi mkuu wa utafiti Dk. Alexis Conason, mwanasaikolojia aliyeidhinishwa katika NYC, alisema;

“Watu huweka hisia nyingi na matumaini katika kupunguza uzito, na wanaamini ikiwa tu watapunguza uzito kila kitu kitakuwa sawa na mambo yote mazuri wanayotaka maishani yatakuja watakapopunguza uzito,” Conason aliiambia The Post hapo awali.

NB; Ni vizuri sana kiafya kupunguza Uzito, lakini Zingatia njia Salama za kupunguza Uzito

#SOMA Hapa Jinsi ya Kupunguza Uzito

•Rejea Link;Uzito journal of tips, FDA

BonusTips; MADHARA ya Kuwa na Uzito Mkubwa kiafya

jinsi Ozempic, dawa maarufu ya kupunguza uzito inavyosababisha tatizo
la wasiwasi, mfadhaiko na vitendo vya kujiua
0 Comment

Mbinu za jinsi ya kupunguza tumbo kwa harakaAfyaclass Forum •

Mbinu za jinsi ya kupunguza tumbo kwa haraka

Kila mtu ana mafuta tumboni(belly fat),hata watu ambao wana tumbo dogo,Hiyo ni kawaida. Lakini ukiwa na mafuta mengi ya tumbo yanaweza kuathiri afya yako kwa njia ambayo mafuta mengine hayaathiri.

Baadhi ya mafuta yako yanahifadhiwa chini ya ngozi yako. Mafuta mengine huhifadhiwa ndani zaidi, karibu na moyo wako, mapafu, ini, na viungo vingine.

Sasa basi,mafuta yale ambayo huhifadhiwa ndani zaidi — yanayoitwa “visceral” fat — ndyo ambayo yanaweza kuwa tatizo kubwa, hata kwa watu wembamba.

Fahamu kama una mafuta mengi mno ya aina hii(Visceral fat), huenda ukaweza kupata matatizo mbali mbali ya kiafya kama vile;

Katika Makala hii tunaeleza madhara ya kuwa na tumbo kubwa(mafuta mengi tumboni), lakini baada ya madhara hayo,hizi ni mbinu muhimu za kukusaidia kukabiliana na tatizo hili.

jinsi ya kupunguza tumbo

1. Fanya Mazoezi ya mwili

Kufanya mazoezi ya mwili husaidia kupunguza mafuta mwilini yakiwemo Visceral fat.

Unashauriwa kufanya mazoezi angalau kwa dakika 30, kwa muda wa angalau siku 5 za wiki,

Fanya Mazoezi mbali mbali kama vile kuruka kamba,kutembea n.k

Pata Zaidi hapa: Maelekezo kamili ya Mazoezi kwa Ajili ya kukusaidia kupunguza Uzito wako pamoja na Tumbo kwa ujumla

2. Aina ya chakula unachokula(Diet):

Kula vyakula vyenye kiwango kikubwa cha nyuzinyuzi(fibers),

Na tafiti zinaonyesha,unapopanga Diet yako kwa ajili ya kupunguza Uzito, Moja ya vitu ambavyo ni vyakwanza kabsa kupungua ni pamoja na mafuta ya Tumbo(belly fat).

Pata Zaidi hapa: Full diet plan kwa Ajili ya kukusaidia kupunguza Uzito wako pamoja na Tumbo kwa ujumla

3. lala kwa muda Sahihi

Kupata kiwango sahihi cha usingizi husaidia kupunguza matatizo mengi ikiwemo hili la tumbo na Uzito wa mwili kwa ujumla.

Katika utafiti mmoja, watu waliopata usingizi na kulala muda wa saa 6 hadi 7 kwa usiku walipata mafuta kidogo ya visceral kwa miaka 5 ikilinganishwa na wale waliolala masaa 5 au machache kwa usiku au waliolala masaa 8 au zaidi kwa usiku.

Kulala kunaweza kuwa jambo pekee ambalo lina muhimu mkubwa katika afya ya binadamu.

Soma Zaidi hapa: Faida za kupata muda wa kutosha wa kulala

4. Msongo wa mawazo au Stress:

Kila mtu ana stress, ila Jinsi unavyoshughulikia stress ni muhimu, je,ukiwa katika hali ya Msongo wa mawazo au Stress ni njia gani unatumia ili kukabiliana na tatizo hili?

Mambo bora zaidi unayoweza kufanya ni pamoja na kupumzika na marafiki na familia, kutafakari, kufanya mazoezi ya kupumua, na kupata ushauri n.k Hiyo itakusaidia kuwa na afya njema na kufanya maamuzi mazuri.

Wapo baadhi ya watu wakiwa kwenye hali ya Stress hula Zaidi, sababu inayofanya ongezeko la mafuta tumboni kwa haraka, hivo,kudhibiti unachokula huweza kusaidia kupungua ukiwa katika hali hii.

Ingawa pia,wapo watu wakiwa kwenye hali ya Stress hawawezi kula kabsa.

JINSI YA KUPUNGUZA TUMBO(afyatips)

Kwa hivi sasa watu wengi hupambana na njia mbali mbali za kupunguza matumbo yao hasa wadada ili kuonekana warembo zaidi, na kuvaa nguo ipendeze, Hivo basi huwapelekea kutumia njia mbali mbali ili kupunguza tumbo, huku zingine zikiwa sahihi na zingine zikiwa hatari zaidi kwa afya zao. Hapa kuna baadhi ya mambo ya kuzingatia wakati unahitaji kupunguza tumbo lako,

1. Hakikisha unapendelea zaidi kula vyakula pamoja na matunda yenye nyuzi nyuzi au Fibers kama vile machungwa,maembe,maparachichi n.k

2. Epuka kula vyakula vyenye mafuta zaidi ikiwemo chips

3. Epuka matumizi ya pombe kupita kiasi

4. Kula vyakula vyenye kiwango kikubwa cha PROTEIN na sio kiwango kikubwa cha MAFUTA mfano; Maharage n.k

5. Punguza au epuka kabsa kuwa na msongo wa mawazo,watu wengi hawajui kwamba msongo wa mawazo huweza kusababisha tatizo la kuongezeka kwa tumbo au hata uzito kwa baadhi ya watu

6. Epuka kula vyakula vyenye kiwango kikubwa cha sukari

7. Fanya mazoezi ya mwili kila siku,angalau kwa dakika 30 au Nusu saa kila siku

8. Hakikisha unapata muda wa kutosha wa kupumzika pamoja na kulala

9. Unaweza kupendelea kula vyakula jamii ya samaki zaidi huku ukiepuka mafuta mengi

10. Japo juice za matunda ni nzuri sana, ila baadhi zina kiwango kikubwa sana cha sukari,hivo epuka juice kama hizi

11. Kunywa chai ya kijani maarufu kama GREEN TEA, najua wengi wenu hamjawahi kusikia hii,ila ipo na watu wanaitumia hivo ulizia itakusaidia pia.

12. Pamoja na Tips zingine za Afya

KUMBUKA; kufunga mkanda tumboni ili tumbo lipungue au kushinda na njaa kila siku huweza kuwa hatari kwako na sio njia salama ya kupunguza tumbo

• Soma pia: Jinsi ya Kupunguza Uzito wa Mwili

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Mbinu za jinsi ya kupunguza tumbo kwa haraka
0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Forum Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Forum ASANTE.
UNDERSTOOD