Showing posts with label madhara ya pornograph. Show all posts
Showing posts with label madhara ya pornograph. Show all posts

Madhara ya kuangalia picha chafu maarufu kama PornographAfyaclass Forum •

Madhara ya kuangalia picha chafu maarufu kama Pornograph

Watu wengi wameathiriwa sana na Utazamaji wa Picha chafu au Video chafu au Pornograph(X) au Video/Picha za Ngono,hali ambayo imewaingiza kwenye Uraibu au Addiction,Kiasi kwamba hata mahusiano halisi hawaridhishwi nayo(relationship satisfaction),
Wengine wameingia kwenye hatari ya kupata athari kubwa ya Ubongo,Matatizo ya afya ya akili ikiwemo;Swala la wasi wasi(Anxiety), huzuni(Depression) pamoja na Aibu ambayo hawajui inatokana na nini.
Hebu tuaangalie Baadhi ya Madhara unayoweza kupata kwa kutazama Video au Picha Chafu(Video au picha za ngono)

Madhara ya kuangalia picha chafu maarufu kama Pornograph

1.Mabadiliko kwenye Ubongo pamoja na Mfumo wa Neva kwa ujumla:

Kutazama video au Picha chafu(za ngono) kunaweza kufanya kazi kama uraibu wa dawa za kulevya, na kusababisha kutolewa kwa dopamini kupita kiasi ambayo huchochea mfumo wa Ubongo unaohusika na hisia,Hali inayoweza kusababisha kupotea kwa hisia. 
Uchunguzi unaonyesha kuwa inaweza kusababisha athari katika maeneo ya ubongo yanayodhibiti kufanya maamuzi na udhibiti wa msukumo.

2.Matatizo kwenye Mahusiano halisi(Relationship Issues): 

Kuangalia Pornograph mara nyingi husababisha kupungua kwa kuridhika kingono na mweza halisi, kupungua katika uhusiano, na kupungua kwa urafiki.
Kwahyo unaweza kuingia katika hali ya kutokuridhika kingono, hali ambayo huweza kuleta matatizo kwenye mahusiano.

3.Matatizo kwenye Afya ya Akili

Kama nilivyosema hapo awali, Ukishaingia kwenye Uraibu wa kuangalia Video au Picha Chafu(Video/Picha za Ngono),tayari upo kwenye athari za afya ya Akili, hapa utaanza kuona matokeo mbali mbali ikiwemo;
  • Kuwa na Wasi wasi Mkubwa(Anxiety)
  • Huzuni au Mfadhaiko(depression)
  • Hali ya kusikia Aibu
  • Au kujihisi na Hatia

4.Mabadiliko ya Kitabia: 

Tafiti mbali mbali huonyesha; Baadhi hukabiliwa na maudhui ya vurugu au ya kudhalilishwa kunahusishwa na kuongezeka kwa tabia za uchokozi kwa wanaume na kupungua kwa kujithamini/taswira mbaya ya mwili kwa wanawake. Inaweza kusababisha unyanyasaji wa kijinsia pia.

5.Matatizo ya nguvu za Kiume

Baadhi ya Tafiti huonyesha pia Kuangalia kupita kiasi Video au Picha za Ngono huhusishwa na hali ambayo hujulikana kama pornography-induced erectile dysfunction (PIED) kwa Wanaume.
Hali ambayo huathiri nguvu za kiume pamoja na uwezo wa Mwanaume Kushiriki tendo kwa Ufasaha Zaidi.

Bonus Point: Fahamu mambo ambayo hutokea kwenye Ubongo wako Ukiacha kuangalia Video au Picha Chafu(Video/Picha za ngono)

Ubongo wako hurudi katika hali yake ya kawaida ndani ya siku 90, Siku hizi 90 ndizo zinazohitajika kujisikia kama mtu tofauti kabisa. Urekebishaji wa vipokezi vya dopamine na ile raha ya kawaida na kuhisi kuridhika hurejea tena. Hamasa inarudi na nishati huelekezwa kwenye kazi ya mazoezi na malengo halisi ndani ya Ubongo.

Mvuto kwa watu halisi huongezeka zaidi ya Video au Picha Chafu(PORN).Umakini au Concentration huongezeka na kujiamini kunaongezeka zaidi.

Unyogovu,huzuni au Mfadhaiko(Depression) hufifia kadri aibu inavyopotea,Kujiamini na furaha ya asili inarudi. Hali ya Kupata Usingizi huanza kuimarika ikiwa ulikuwa hupati Usingizi n.k...

Acha Kuangalia Porn kwa afya ya Ubongo wako,afya ya uzazi na mwili wako kwa ujumla,ni Very addicted Kama Dawa za Kulevyia.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Rejea Links Zilizotumika Pia;

  • https://pmc.ncbi.nlm.nih.gov/articles/PMC10399954/
  • https://culturereframed.org/adolescents-porn-and-mental-health-understanding-the-dangerous-effects-of-porn-on-developing-minds/#:~:text=It%20stimulates%20the%20release%20of,sexual%20problems%20in%20adult%20life
  • https://www.mentalhealth.com/blog/how-pornography-distorts-intimate-relationships#:~:text=Not%20all%20use%20is%20harmful,harm%20than%20the%20material%20itself.

0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Forum Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Forum ASANTE.
UNDERSTOOD