CHANZO CHA HASIRA KWA MWANAMKE WAKATI WA SIKU ZA HEDHIAfyaclass Bongo Social •

HEDHI

• • • • • •

CHANZO CHA HASIRA KWA MWANAMKE WAKATI WA SIKU ZA HEDHI


Bila shaka utakuwa shahidi au hata wewe mwenyewe ni mhusika kwamba kwa baadhi ya wanawake  wakiwa kwenye siku zao za hedhi(menstrual period) huwa na Hasira sana kupita kawaida, je chanzo cha shida hii ni nini?


CHANZO CHAKE NI NINI?


Ukweli ni kwamba mpaka sasa hakuna sababu ya moja kwa moja ambayo imehusishwa kwenye hili la mwanamke kuwa na Hasira sana wakati wa siku za hedhi japo baadhi ya tafiti na majarida mbali mbali ya afya yamehusisha na sababu hizi hapa chini;


• Mabadiliko ya vichocheo au hormones ambayo hutokea wakati wa hedhi, na mabadilko hayo huhusisha vichocheo vikubwa viwili ESTROGEN pamoja na PROGESTERONE ambapo huleta matokeo mpaka kwenye mood ya mtu,


Wakati yai la mwanamke linatoka kwenye vifuko vya mayai yaani ovaries kiwango cha hormone ya ESTROGEN pamoja na PROGESTERONE hushuka sana hali ambayo huweza kupelekea kupungua pia kwa kiwango cha SEROTONIN kwenye mwili wako,


Kushuka kwa kiwango cha Serotonin mwilini huleta matokeo mbali mbali kwenye mwili wako kama vile;


- Mwanamke kuwa na Hasira sana


- Mwanamke Kushindwa kutulia na kufanya kitu kimoja


- Mwanamke kuwa na tatizo la kukosa kabsa Usingizi, utakuwa shahidi kwamba wanawake wengi hukosa usingizi wakiwa kwenye kipindi cha hedhi


- Mwanamke kuhisi huzuni sana


- Mwanamke kuanza kuchagua baadhi ya vyakula na kuchukia vingine n.k


JINSI YA KUDHIBITI HALI YA HASIRA SANA UKIWA KWENYE SIKU ZA HEDHI


Zoezi hili la kuweza kudhibiti hasira wakati wa siku za hedhi kwa mwanamke sio la siku moja,linahitaji muda pamoja na mazoezi ya kila mara, na kujua njia gani sahihi inafanya kazi kwako vizuri zaidi kwani njia zipo zaidi ya moja na wanawake wanatofautiana.


Unashauriwa kuanza kuweka kumbukumbu ya Tarehe kwa kila mzunguko wa hedhi ambapo hasira huanza kujitokeza,hii itakusaidia sana wakati wa kudeal na hili tatizo la hasira wakati wa hedhi,kisha baada ya kujua hizo tarehe kwenye mizunguko mbali mbali ya hedhi fanya mambo haya hapa chini;


• Epuka vitu vyote ambavyo vinakufanya usitulie au kukuletea msongo wa mawazo


• Refresh mind kwa vitu vyepesi zaidi,epuka kazi nyingi sana pamoja na kutoka out kama unapenda


• Fanya mazoezi ya mwili,njia hii husaidia sana kwa kiwango kikubwa


• Kula vyakula unavyovipenda sana


• Pata muda mzuri wa kulala usiku N.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

CHANZO CHA TATIZO LA DEPRESSION PAMOJA NA TIBA YAKEAfyaclass Bongo Social •

DEPRESSION

• • • • • •

CHANZO CHA TATIZO LA DEPRESSION PAMOJA NA TIBA YAKE


Tatizo la depression huhusisha hali ya mtu kuwa na huzuni kubwa,kuhisi hasira na kuhisi kupoteza kila kitu hali ambayo hupelekea hadi kushindwa kufanya kazi zake za kila siku,na tafiti zinaonyesha tatizo hili huzidi zaidi kwa watu wenye matatizo kama vile;


- Asthma

- Magonjwa ya moyo

- Tatizo la arthritis

- Kansa au Saratani

- Tatizo la kisukari

- Unene au uzito kupita kiasi yaani obesity n.k


DALILI ZA TATIZO LA DEPRESSION NI PAMOJA NA;


1. Mtu kuhisi huzuni,kupoteza tumaini,hasira,kutokutulia,au hofu mara kwa mara


2. Mwili kuchoka kupita kawaida,kuhisi kushindwa kufanya kila kitu, kushindwa kukocentrate au kufocus kwenye kile unachokifanya, wengine kuanza kulewa sana pombe, kutamani kujitoa uhai n.k


3. Tatizo la depression pia huweza kusababisha tatizo la mtu kuanza kupoteza kumbu kumbu(memory loss)


4. Kupoteza uwezo wa kufikiri vizuri na kufanya maamuzi sahihi kila mara


5. Mtu kupoteza kabsa interest ya kile kitu anachokifanya na kutamani kuacha kabsa kuendelea


6. Mtu kujiona mkosaji kila mara,na wengine hupenda kuomba msamaha kila mara hata kwa vitu ambavyo kwa hali ya kawaida ni sahihi


7. Mtu kujihisi mpweke,kupenda kukaa mwenyewe na kujitenga na watu, kuhisi aibu mbele za watu kila mara


8. Mtu kupoteza kabsa hamu ya kula chakula hali ambayo hupelekea kukonda sana na kuwa na uzito mdogo wa mwili


9. Mtu kufikiria kujiua au kujidhuru mara kwa mara


10. Mtu Kuwa na tatizo la kukosa usingizi


11. Mtu kuanza kupatwa na tatizo la maumivu makali ya kichwa, Tumbo pamoja na mgongo


12. Baadhi yao huanza kupatwa na matatizo kama vile kuharisha mara kwa mara,kichefuchefu na kutapika


13. Kukosa kabsa hamu ya tendo la ndoa au kushindwa kufanya tendo la ndoa n.k


CHANZO CHA TATIZO LA DEPRESSION


- Family history, kama kwenye familia yenu kuna mtu mwenye tatizo kama hilo uwezekano wa wewe kupatwa pia ni mkubwa


- Kukutana na matatizo mbali mbali katika umri mdogo kama vile ajali,vifo n.k


- Mtu kuwa na matatizo mbali mbali kwenye ubongo wake kama vile sehemu ya mbele ya ubongo yaani frontal lobe kuwa less active n.k


- Kukutana na matukio magumu kwenye maisha yako kama vile; kufukuzwa kazi,kufeli mitihani kwa wanafunzi, matatizo ya ndoa,mahusiano n.k


- Matatizo mbali mbali ya kiafya kama vile; tatizo la kukosa usingizi(insomnia),kisukari,presha,asthma n.k


- Matumizi ya vilevi kama pombe,uvutaji wa sigara n.k 


MATIBABU YA TATIZO LA DEPRESSION


Kuna njia mbali mbali hutumika kumsaidia mtu mwenye tatizo la depression kama vile;


• Kufanya mazoezi ya mwili kila siku angalau kwa dakika 30 au nusu saa


• Kula vyakula vyenye virutubisho vyote


• Kuepuka unywaji wa pombe au uvutaji wa sigara


• Kujifunza kusema "HAPANA" kwa kila unachokiona kinaenda tofauti na ilivyo kawaida


• Pata msaada wa kisaikolojia yaani psychotherapy kama kuna huduma kama hiyo eneo ulilopo


• Pata muda wa kutosha wa kupumzika,kurefresh mind,kuongea na watu tofauti tofauti wala usikae peke yako, pamoja na muda wa Kulala


• IBADA, Tafiti zinaonyesha Ibada imeonekana kuwa tiba kuu ya tatizo hili,hivo kama ni mkristo au muislam nenda sehemu za ibada hudhuria sana kila kipindi,hali hiyo itaisha na kukujengea tumaini jipya la maisha


• Kwa upande wa Dawa, kuna dawa mbali mbali kama vile;


✓ Antidepressants mfano; Fluvoxamine(Luvox)


✓ Antiaxiety mfano; Diazepam


✓ Antipyschotic N.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comment

CHANZO CHA TATIZO LA KUTOKWA NA MBEGU ZA KIUME(SHAHAWA) UUME UKIWA HAUJASIMAMAAfyaclass Bongo Social •

 AFYA YA UZAZI KWA WANAUME

• • • • •

CHANZO CHA TATIZO LA KUTOKWA NA MBEGU ZA KIUME(SHAHAWA) UUME UKIWA HAUJASIMAMA


Tatizo la kutokwa na sperm/mbegu za kiume/semen au shahawa wakati hufanyi mapenzi au uume ukiwa haujasimama ni tatizo ambalo linatokea kwa baadhi ya wanaume. je chanzo cha tatizo hili ni nini?


Katika hali ya kawaida wanaume hutoa shahawa au maji maji kwenye uume wakati wanajiandaa kufanya tendo la ndoa, wakati wanafanya tendo la ndoa, wakati wapo kwenye hisia za kimapenzi, wakati wanapiga punyeto au masturbation n.k


Lakini kuna baadhi ya wanaume hupatwa na tatizo la kutokwa na maji maji kwenye uume(semen) kama yale wakati mtu akiwa katika hisia kali za kimapenzi au wengine humwaga kabsa shahawa wakati uume haujasimama, hawapo kwenye hisia za kimapenzi, wapo tu wamekaa katika hali isio na viashiria vyovyote vya kimapenzi.


CHANZO CHA TATIZO LA KUTOKWA NA MBEGU ZA KIUME(SHAHAWA) UUME UKIWA HAUJASIMAMA AU WAKATI HAUPO KWENYE HISIA ZOZOTE ZA KIMAPENZI


1. Wakati umelala, Wanaume wengi wakati wamelala huweza kuota ndoto ambazo hujulikana kama wet dreams au Nocturnal emissions, hali ambayo hupelekea kujiona wanafanya mapenzi kisha kumwaga shahawa, hii hutokea sana wavulana wakiwa katika kipindi cha ukuaji yaani Balehe au Puberty


MATIBABU

Katika hali ya kawaida huhitaji matibabu yoyote kama chanzo cha tatizo lako ni hiki hapa.


2. Matumizi ya baadhi ya dawa; dawa jamii ya ANTIDEPRESSANTS huweza kusababisha matatizo mbali mbali mwilini kama vile;

- mbegu za kiume kutoka nje ya uume au mwanaume kumwaga shahawa wakati hafanyi mapenzi wala hayupo kwenye mazingira hayo

- Mwanaume kukosa kabsa hamu ya tendo la ndoa

- Mwanaume kuchelewa sana kufika kileleni

- Mwanaume kuwa na tatizo la  upungufu wa nguvu za kiume,uume kushindwa kusimama au kwa kitaalam Erectile dysfunction

• Dawa zingine ni kama vile mood stabilizers au baadhi ya dawa za kutibu matatizo ya hormones mwilini

MATIBABU

Ukiona dalili hizi za kutoa shahawa wakati haupo kwenye mazingira ya kufanya tendo la ndoa halafu unatumia dawa katika makundi hayo hapo juu niliyoeleza,unashauriwa kuongea na daktari wako ili ikiwezekana ubadilishiwe dawa na kuacha dawa hizo.


3. Matatizo kwenye tezi la PROSTATE, Tezi la Prostate husaidia kutoa SEMEN ambazo ndizo hufanya kazi ya kusaidia kusafirisha mbegu za kiume kutoka kwenye uume,tezi hili huweza kukumbwa na matatizo mbali mbali kama vile;

- Kuvimba kwa tezi au kuongezeka ukubwa yaani Prostatitis kutokana na sababu mbali mbali kama vile maambukizi ya bacteria,matatizo kwenye mfumo wa kinga ya mwili,tatizo la kansa au Saratani n.k

Unashauriwa kuwahi hospitalini endapo utaona dalili hizi hapa chini;


• Kupatwa na maumivu ya mkojo wakati wa kukojoa

• Kutoa mkojo ambao umechanganyika na damu

• kutoa shahawa ambazo zimechanganyika na damu

• Kushindwa kufika kileleni kwa haraka,kushindwa kabsa kufika kileleni au kuwahi sana kuliko kawaida,uume kushindwa kusimama n.k

• Kupata maumivu makali wakati unafika kileleni


MATIBABU

Matatizo ya tezi la Prostate huhusisha tiba mbali mbali kulingana na chanzo chake kama vile huduma ya upasuaji na kuondolewa kwa tezi hilo pamoja na tiba zingine.


4. Tatizo la kwenye mfumo wa nerves au Nerves Injury

Endapo mwanaume kupatwa na jeraha au tatizo lolote linaloharibu nerves au mfumo wa fahamu huweza kupatwa na matatizo mengine mbali mbali kama vile;

- Hili la kutoa mbegu za kiume au kumwaga uume ukiwa haujasimama,ukiwa hufanyi mapenzi na wala huna hisia hizo kwa wakati huo

- Mabadiliko kwenye nguvu za kiume,uwezo wa uume kusimama, kushindwa kufika kileleni kabsa,kuchelewa au kuwahi kufika kileleni n.k

Tatizo la nerves kuharibiwa huweza kusababishwa na sababu mbali mbali ikiwemo maambukizi ya bacteria,umri mkubwa,magonjwa ya zinaa, upasuaji kwenye uti wa mgongo,kuumia kwa kupata ajali n.k


MATIBABU

Matibabu ya tatizo la kuharibika kwa nerves hutegemea na chanzo chake hivo lazima uongee na wataalam wa afya kwanza,kufanya vipimo kisha kujua chanzo chake na kuanza tiba


KUMWAGA SHAHAWA BAADA YA KUKOJOA

Hili si tatizo kwani wanaume wengi hupatwa na hii hali hasa mda mfupi tu kama ndyo wametoka kufanya mapenzi, kwani baadhi ya shahawa huweza kubaki kwenye njia ya mkojo yaani Urethra hivo hutolewa nje wakati wa kukojoa,

Japo huweza kuwa tatizo endapo hali hii hutokea kila mara, na kuhusishwa na matatizo mengine kama vile maambukizi ya bacteria,kuumia kwenye nerves, magonjwa ya zinaa N.k, Hivo kama ni tatizo la kujirudia kila mara muone daktari.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

CHANZO CHA DAMU KUCHAFUKAAfyaclass Bongo Social •

 DAMU

• • • • • •

CHANZO CHA DAMU KUCHAFUKA


Hivi kuchafuka kwa Damu ni kitu gani?


Bila shaka umewahi kusikia au hata wewe menyewe umeshawahi kuambiwa una tatizo la damu kuchafuka baada ya kuwa na dalili flani za kuumwa, je kuchafuka kwa damu ni kitu gani? au ina maana gani mtu akisema damu imechafuka?


Kuchafuka kwa damu ni kiswahili ambacho hutumika sana ila tafsri yake ni "SEPSIS or Blood Infection" Kwa lugha ya kitaalam zaidi, huku tukiwa na maana ya maambukizi kwenye damu ambapo kinga ya mwili wako huanza kuzalisha kemikali wakati ikipambana na mashambulizi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa kama vile Bacteria N.k


Tatizo hili hutokea zaidi kwa watu wenye kinga ndogo ya mwili kama vile: Wenye tatizo la Saratani,maambukizi ya ukimwi, wanaotumia dawa ambazo huweza kuleta athari kwenye mfumo wa kinga ya mwili n.k


Tafiti zinaonyesha pia Wenye ugonjwa wa Kisukari, waliofanyiwa upasuaji, wazee pamoja na wajawazito hupatwa sana na tatizo hili.


DALILI ZA KUCHAFUKA KWA DAMU


Baada ya mtu kupatwa na maambukizi ya vimelea vya magonjwa mbali mbali kwenye damu kama vile Bacteria na kinga ya mwili kuanza kupambana na mashambulizi hayo ndipo mtu huanza kupata dalili mbali mbali kama vile;


- Mwili kuanza kutoa jasho jingi sana kuliko kawaida


- Ngozi ya mwili kubadilika rangi yake ya asili


- Mtu kuanza kupatwa na uchovu wa mwili kupita kawaida


- Mtu kuanza kuhisi kichefuchefu pamoja na kutapika mara kwa mara


- Kupatwa na maumivu makali ya kichwa


- Kupatwa na tatizo la kuharisha


- Mapigo yako ya moyo kuanza kubadilika na kwenda mbio mara kwa mara


- Kuanza kukojoa mkojo mdogo kuliko kawaida


- Joto la mwili kuwa juu sana au mgonjwa kuwa na homa


- Kuanza kuhisi baridi kali mwilini N.k


ENDAPO HUKUPATA TIBA YOYOTE NINI HUTOKEA?


• Endapo tatizo hili likawa la mda mrefu na mtu hakupata tiba huweza kuleta madhara makubwa mwilini kama vile;


1. Matatizo ya moyo


2. Matatizo ya Ubongo


3. Matatizo ya Mapafu


4. Tatizo la Figo kufeli N.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

TATIZO LA NGOZI KUWA KAVU,KUPAUKA NA KUPASUKAAfyaclass Bongo Social •

 NGOZI

• • • • • •

TATIZO LA NGOZI KUWA KAVU,KUPAUKA NA KUPASUKA


Tatizo la ngozi kuwa kavu,kupauka na kupasuka huweza kuonekana maeneo mbali mbali ya mwili kama vile kwenye mikono,miguuni n.k, Hata hivo tatizo hili huweza kuwa la muda mfupi au muda mrefu kwa baadhi ya watu kulingana na hali ilivyo kama vile uwepo wa magonjwa ya ngozi,umri,hali ya hewa n.k


CHANZO CHA TATIZO LA NGOZI KUWA KAVU,KUPAUKA NA KUPASUKA


1. Hali ya hewa, baadhi ya watu huanza kupata tatizo hili la ngozi kuwa kavu,kupauka au kupasuka wakati wa Baridi sana na baadhi yao baada ya kuchomwa na jua kali au joto kali


Hapa asilimia kubwa ya watu wenye tatizo la ngozi kuwa kavu,kupauka au kupasuka wakati wa hali ya hewa kama vile; baridi kali huweza kupona tu kwa kutumia mafuta mbali mbali ya kulainisha ngozi ya mwili kwa kipindi hiki


2. Tatizo la ngozi ya mwili kuunguzwa na vyanzo mbali mbali vya joto kali kama vile moto wenyewe(wale wanaokaa sana jikoni),jua n.k


3. Tabia ya kuoga na maji ya moto kwa muda mrefu na mara kwa mara hasa kwa wale wanaopenda kuoga kwenye swimming pool za maji ya moto huweza kusababisha ukavu kwenye ngozi ya mwili


4. Kuwa na magonjwa mbali mbali ya ngozi kama vile Atopic dermatitis au Eczema


5. Matumizi ya baadhi ya sabuni za kuogea zenye kemikali kali huweza kuondoa layer ya mafuta kwenye ngozi na kuleta tatizo la ngozi kuwa kavu,kupauka na kupasuka pia.


DALILI ZA TATIZO HILI LA NGOZI KUWA KAVU,KUPAUKA NA KUPASUKA NI PAMOJA NA;


- Mtu kuhisi ngozi kukakamaa isivyo kawaida hasa baada ya kutoka kuoga


- Ngozi ya mwili kuaza kuwa na mikwaruzo hasa maeneo ya miguuni na kwenye mikono


- Ngozi ya mwili kuanza kuwasha mara kwa mara


- Ngozi ya mwili kuanza kutoka magamba kidogo kidogo pamoja na unga mweupe


- Ngozi ya mwili kuwa na kreki hasa maeneo ya miguuni na mikononi


- Ngozi ya mwili kuanza kubadilika rangi na kuwa kijivu,dhambarau au nyekundu zaidi


- Na kwa baadhi ya watu ngozi ya mwili hupasuka au kuwa na kreki hadi kupelekea damu kuvuja


- Ngozi ya mwili kuchubuka yenyewe


UKIONA DALILI HIZI HAPA CHINI MUONE DAKTARI MAPEMA ZAIDI


• Ngozi kuwa kavu hadi kuwa nyekundu au kuvuja damu


• Ngozi kuwa kavu na kuwasha hadi kupelekea mtu kushindwa kulala usiku


• Ngozi ya mwili kuchubuka kwa kiwango kikubwa zaidi


• Kuanza kupata vidonda kwenye ngozi yako

N.k


WATU AMBAO WAPO KWENYE HATARI YA KUPATWA NA TATIZO HILI NI PAMOJA NA;


✓ Wenye umri wa kuanzia miaka 40 na kuendelea


✓ Wanaoshi maeneo yenye baridi sana pamoja na hali ya hewa kavu


✓ Wanaofanya kazi ambazo huhitaji kushika maji mara kwa mara


✓ Wanaopenda kuoga kwenye swimming pool za maji ya moto N.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

MADHARA YA KUFANYA MAPENZI NA MWANAMKE ALIYOPO KWENYE HEDHIAfyaclass Bongo Social •

 HEDHI

• • • • •

MADHARA YA KUFANYA MAPENZI NA MWANAMKE ALIYOPO KWENYE HEDHI


Mbali na kwamba kufanya mapenzi wakati wa hedhi ni sawa na kufanya mapenzi kwenye mazingira machafu na hatarishi mno,Pia kuna magonjwa mengi ambayo wahusika wote wawili huweza kuyapata yaani Mwanaume na Mwanamke.


1. MADHARA KWA MWANAMKE


- Kuongezeka kwa damu ambayo hutoka wakati wa period(hedhi) na kuanza kutoka nyingi


- Kuwa katika hatari ya kupata maambukizi kwenye via vya uzazi yaani PID ikiwa ni pamoja na kwenye shingo ya kizazi n.k


- Kuwa katika hatari ya kupatwa na magonjwa ya Zinaa ikiwa ni pamoja na maambukizi ya UKIMWI


- Kupata maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi na wakati wa tendo la ndoa


- Kuwa katika hatari ya kupatwa na Ugonjwa wa Homa ya Ini(Hepatitis)


- Kuwa na tatizo la kupatwa na hofu pamoja na wasiwasi mara kwa mara


- Uwezekano wa kubeba mimba ambayo haitarajiwi upo japo ni mdogo sana


- Mirija ya uzazi kuziba pamoja na kupatwa na tatizo la kushindwa kubeba mimba


- Kupatwa na tatizo la kuvimba kwa kuta za ndani ya uke

N.k



2. MADHARA KWA MWANAUME


- Mwanaume kupatwa na maambukizi kwenye mfumo mzima wa mkojo ikiwa ni pamoja  na njia ya mkojo,Kibofu cha mkojo,Figo n.k


- Mwanaume kupatwa na tatizo la kuziba kwa Njia ya Mkojo


- Mwanaume kupatwa na matatizo kwenye tezi dume(Prostate gland)


- Mwanaume Kutokufurahia tendo la ndoa,kwani limefanyika kwenye mazingira machafu sana,mazingira ya damu,maji maji,harufu,N.k


Lakini pia kufanya mapenzi mwanamke akiwa kwenye hedhi huweza kuleta matatizo ya uzazi kwa wote wawili(mwanamke na mwanaume)


Epuka kufanya mapenzi kipindi cha hedhi au Period kwani sio salama kwa afya yako


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comment

DALILI ZA TATIZO LA DAMU KUGANDAAfyaclass Bongo Social •

DAMU KUGANDA

• • • • • •

DALILI ZA TATIZO LA DAMU KUGANDA


Dalili za tatizo la damu kuganda huweza kuonekana kwenye maeneo mbali mbali ya mwili kama vile mikononi,miguuni, kwenye mapafu, kwenye moyo n.k

 

Wakati damu imeganda(Blood clots) kwenye mishipa ya vein miguuni au mikononi hali ambayo hujulikana kwa kitaalam kama deep vein thrombosis (DVT) ni hatari kwani clots za damu huweza kusafiri moja kwa moja kwenda kwenye moyo au mapafu.


Na sana sana damu kuganda maeneo kama haya hutokana na mtu kukaa sehemu moja kwa muda mrefu,kutokutembea kwa sababu mbali mbali kama vile ugonjwa wa miguu, upasuaji n.k


DALILI ZA TATIZO LA DAMU KUGANDA


1). Miguuni au Mikononi


- Mikono au miguu kuvimba na hii huanza kuonekana pale tu damu inapoanza kuganda


- Rangi ya ngozi mikononi au miguuni kubadilika na kuwa Nyekundu zaidi au Blue, na baadhi ya watu huanza kupatwa na miwasho ya ngozi maeneo haya


- Maumivu ya miguu au mikono ambayo huongezeka kadri siku zinavyosogea mbele


- Ngozi ya sehemu ambapo damu imeganda au tatizo la deep vein thrombosis (DVT)  limetokea huwa ya moto zaidi kuliko sehemu zingine


- Misuli ya miguu kuanza kukakamaa(lower leg muscle cramps)


- Uvimbe miguuni ambao huambatana na maumivu ya miguu n.k


2). Mapafu


Kama zile clots za damu baada ya kuganda zimefika kwenye mapafu hali ambayo hujulikana kama pulmonary embolism ni hatari sana kwa mgonjwa,  na mgonjwa huweza kuanza kupata dalili hizi hapa;


- Kupata shida sana ya kupumua au kukosa hewa


- Mgonjwa kuanza kukohoa sana, wengine hukohoa hadi damu


- Kuanza kupata maumivu makali ya kifua wakati wa kupumua


- Kupatwa na kizunguzungu kikali


- Kutokwa na jasho sana mwilini n.k


3). Moyo


- Mgonjwa kupata maumivu makali ya kifua pamoja na mikono


- Mgonjwa kutokwa sana na jasho mwilini


- Kupata shida wakati wa kupumua au kupumua kwa shida


- Kuwa katika hatari ya kupatwa na ugonjwa wa shambulio la moyo yaani Heart attack

 N.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comment

CHANZO CHA MAUMIVU MAKALI SANA YA TUMBO WAKATI WA HEDHI(dysmenorrhea)Afyaclass Bongo Social •

HEDHI

• • • • • 

CHANZO CHA MAUMIVU MAKALI SANA YA TUMBO WAKATI WA HEDHI(dysmenorrhea)


Wanawake wengi husumbuliwa na tatizo la maumivu makali sana ya tumbo wakati wa hedhi hadi wengine kufikia hatua ya kushindwa kufanya chochote na kulazwa hospitalini, Je chanzo cha tatizo hili ni nini? Endelea kusoma makala hili ili ujifunze zaidi.


 Kwanza kabsa tuanze na dalili za tatizo la maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi.


Dalili za maumivu ya tumbo wakati wa Hedhi ni pamoja na:


✓ Mwanamke Kupata maumivu makali ya tumbo mithili ya mtu anakuminya,kukugandamiza au kukatwa na kitu kikali chini ya kitovu chako


✓ Maumivu ambayo huanza siku 1 hadi 3 kabla ya kipindi chako cha hedhi, hufikia masaa 24 baada ya kuanza kwa kipindi chako na hupungua kwa siku 2 hadi 3


 ✓ Maumivu ambayo husambaa nyuma ya mgongo,kiunoni na kwenye mapaja


 ✓ Wanawake wengine pia hupatwa na tatizo la:


 i). Kichefuchefu na kutapika


 ii). Maumivu ya kichwa


iii). Kizunguzungu 


iv). Kuharisha n.k


 CHANZO CHA MAUMIVU MAKALI SANA YA TUMBO WAKATI WA HEDHI(wanawake)

 

 Wakati wa hedhi, tumbo la uzazi yaani UTERUS hugandamizwa zaidi na kusinyaa(contract) mithili ya kukamuliwa ili kutoa nje uchafu ambao hauhitajiki tena, sasa wakati mchakato huu unafanyika ndipo tatizo la kupata maumivu ya tumbo huanzia hapo.


Dutu zinazofanana na vichocheo au homoni za prostaglandini ndizo zinazohusika na kusababisha maumivu,mgandamizo na uchochezi zaidi ili kutoa uchafu ambao hauhitajiki tena ndani ya mji wa mimba.


Sasa basi uzalishwaji wa vichocheo hivi vya Prostaglandins ambavyo huhusika katika mchakato mzima wa kuleta maumivu na mgandamizo ndani ya kuta na misuli ya mji wa mimba(uterus) hutofautiana kiwango kati ya Mwanamke mmoja na mwingine.


Endapo Prostaglandins zimezalishwa kwa kiwango kidogo sana mwanamke hupata maumivu kidogo lakini endapo zimezalishwa kwa kiwango kikubwa sana mwilini na mwanamke hupatwa na maumivu makali zaidi.


Na zipo sababu mbali mbali za kutokea kwa mabadiliko hayo na mwanamke kupata maumivu makali sana ya tumbo wakati wa hedhi,na sababu hizo ni kama vile;

 

1. Tatizo la Endometriosis, ambapo kuta za ndani ya mji wa mimba huvimba hali ambayo hupelekea kuta hizo kutokeza kwa nje hasa kwenye maeneo kama vile; kwenye mirija ya uzazi yaani Fallopian tubes, kwenye vifuko vya mayai yaani Ovaries, au kwenye tishu zinazofunika mfupa wa nyonga yaani Pelvis.


 2. Tatizo la Uvimbe kwenye kizazi(Fibroids),  Uvimbe kwenye kizazi huweza kusababisha tatizo la maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi.


 3. Tatizo la Adenomyosis, ambapo Tishu zinazofunika tumbo lako la uzazi yaani uterus huanza kukua ndani ya kuta za misuli ya uterasi.


4. Ugonjwa wa PID(pelvic inflammatory disease) ukiwa na maana ya maambukizi ya bacteria kwenye Via vya Uzazi vya Mwanamke

 

wanawake wenye PID huweza kukumbwa pia na tatizo la maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi hadi wengine kushindwa kufanya chochote na kulazwa hospitalini.


 5. Tatizo la Cervical Stenosis, Kwa wanawake wengine, mlango wa kizazi yaani CERVIX huwa ni mdogo sana hali ambayo husababisha shinikizo zaidi na mgandamizo mkubwa wakati uchafu(Hedhi) ukitolewa nje kutoka kwenye kizazi. Shinikizo hili huongeza maumivu zaidi ya tumbo wakati wa hedhi

 

WANAWAKE AMBAO WAPO KWENYE HATARI ZAIDI YA KUPATA MAUMIVU MAKALI YA TUMBO WAKATI WA HEDHI NI PAMOJA NA;

 

 • Wanawake wenye umri mdogo chini ya miaka 30


 • Wanawake wanaoshambuliwa na magonjwa kama PID mara kwa mara


• Wanawake wanaowahi kubalehe au wanaobalehe mapema, kati ya umri wa miaka 11 au chini


• Wanawake wanaovuja damu nyingi wakati wa hedhi

 

 • Wanawake wenye mzunguko wa hedhi usio na tarehe maalumu(wenye kubadilika badilika) yaani irregular menstrual cycle


• Wanawake waliopo kwenye familia ambazo zina historia ya watoto wa kike kupata maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi (dysmenorrhea)


 • Wanawake wanaovuta sigara n.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comment

CHANZO CHA TATIZO LA KUVUJA JASHO KUPITA KIASI KWENYE KWAPAAfyaclass Bongo Social •

 JASHO

• • • • •

CHANZO CHA TATIZO LA KUVUJA JASHO KUPITA KIASI KWENYE KWAPA


Katika hali ya kawaida kuvuja jasho ni mojawapo ya mifumo ya mwili katika kutoa taka mwili nje na kukufanya uwe na afya zaidi, jasho huweza kutoka kwenye maeneo mbali mbali ya ngozi yako kama vile; Usoni, kwenye kwapa, tumboni,kwenye mikunjo ya miguuni,mikononi,shingoni au mwili mzima.


Na kutokwa na jasho mwilini kwa kawaida huweza kusababishwa na hali mbali mbali kama vile; jua kali,joto kali,mtu kufanya mazoezi mbali mbali n.k


Lakini endapo unatoa jasho jingi sana kwenye maeneo kama KWAPANI bila kuwa na chanzo chochote cha joto huweza kuwa ni tatizo ambalo huhitaji Tiba.


Kuna baadhi ya Watu husumbuliwa na tatizo la kuvuja jasho jingi sana kwapani bila kujali kuna baridi au joto,bila kujali wapo kwenye jua au kivulini,bila kujali wamevaa nguo nyingi nzito au hawajavaa, je nini huweza kuwa chanzo cha tatizo hili?


HIZI HAPA NI BAADHI YA SABABU ZA MTU KUVUJA JASHO JINGI KWAPANI


1. Mtu kuwa na tatizo la Shambulio la moyo yaani Heart attack


2. Mtu kuwa na tatizo la kisukari ikiwa ni pamoja na sukari kuwa chini sana kwenye damu yaani Low Blood sugar


3. Mtu kuwa na maambukizi ya magonjwa mbali mbali kama vile FANGASI wa kwapani n.k


4. Mtu kuwa na Matatizo mbali mbali katika mfumo wa fahamu au Nerves system


5. Dalili za mwanamke kufikia kwenye kipindi cha Ukomo wa Hedhi yaani Menopausal hot flashes


6. Mtu kuwa na matatizo ya baadhi ya Kansa au Saratani kama vile Kansa ya ngozi n.k


7. Mtu kuwa na matatizo kwenye Tezi la THYROID n.k


Hizo hapo juu ni baadhi ya Sababu ambazo huweza kuchangia mtu kuwa na tatizo la kuvuja jasho kwapani kupita kiasi, Hivo ukiona hivo wasiliana na Wataalam wa afya kwa ajili ya kupata matibabu.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

PREDNISOLONE TABLETS ZINAFANYAJE KAZI NA SIDE EFFECTS ZAKE NI ZIPI?Afyaclass Bongo Social •

 DAWA

• • • • • •

PREDNISOLONE TABLETS ZINAFANYAJE KAZI NA SIDE EFFECTS ZAKE NI ZIPI?


Matumizi ya dawa aina ya Prednisolone yameongezeka sana kwa hivi sasa, Dawa hizi ni jamii ya STEROIDS ambazo hutumika kutibu matatizo mbali mbali kwa binadamu kama vile;


• Aina mbali mbali za Allergies(mzio)


• Vimbe mbali mbali mwilini yaani Inflammatory conditions


• Magonjwa ya mfumo wa kinga ya mwili yaani Autoimmune diseases


• Aina mbali mbali za kansa au saratani


• Tatizo la Adrenocortical insufficiency


• Kiwango kikubwa cha Calcium kwenye Damu


• Ugonjwa wa Rheumatoid arthritis


• Magonjwa ya ngozi kama vile Dermatitis


• uvimbe kwenye macho


• Tatizo la Multiple Sclerosis,Asthma


• Pamoja na magonjwa mengine mengi


MATUMIZI:


- Dawa hizi za Prednisolone zipo katika mifumo mikuu minne(4) yaani;


1. Kuna Prednisolone ya VIDONGE vya kunywa Mdomoni(Prednisolone Tablets)


2. Kuna Prednisolone ya SINDANO(Prednisolone Intravenous{IV} Injection)


3. Kuna Prednisolone CREAM ya kupaka kwenye ngozi(Prednisolone Topical Cream)


4. Na kuna Prednisolone MATONE YA MACHO yaani(Eye drops)


SIDE EFFECTS ZA DAWA YA PREDNISOLONE


- Aina hii ya dawa huweza kuleta maudhi mbali mbali kwa mgonjwa baada ya matumizi kama vile;


✓ Kuleta kichefuchefu


✓ Kusababisha mwili kuchoka kuliko kawaida


✓ Matatizo ya Figo kwa baadhi ya wagonjwa kama ikitumiwa kwa muda mrefu


✓ Matatizo ya akili japo ni kwa asilimia 5% ya wagonjwa


✓ Matatizo ya mifupa ikiwa ni pamoja na mifupa kukosa nguvu n.k


✓ Mgonjwa kushambuliwa kwa urahisi na magonjwa kama Yeast infection(Fangasi,Uti,Pid N.k) kutokana na shida ya kushuka kwa kinga ya mwili


✓ Kupatwa na tatizo la Kiungulia yaani Heartburn


✓ Kupatwa na Maumivu makali ya kichwa


✓ Kupatwa na tatizo la kizunguzungu kikali


✓ Mzunguko wa hedhi kubadilika kabsa kwa Wanawake


✓ Kupatwa na tatizo la kukosa usingizi


✓ Kuvuja jasho kupita kawaida


✓ Ngozi kuanza kuwa na chunusi,vijibu vidogo N.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

CHANZO CHA TATIZO LA KUISHIWA NGUVU MWILINI PAMOJA NA TIBA YAKEAfyaclass Bongo Social •

MAGONJWA

• • • • • •

CHANZO CHA TATIZO LA KUISHIWA NGUVU MWILINI PAMOJA NA TIBA YAKE


Tatizo hili huwapata watu wengi kwa hivi sasa,hadi wengine kufikia hatua ya kudondoka gafla,au kushindwa kufanya kazi za kawaida,mfano kwa wafanyakazi wa ndani n.k


Tatizo la kuishiwa na nguvu mwilini huweza kumpata mtu yoyote bila kujali umri wake wala jinsia yake. Tatizo hili huweza kuwa la kujirudia mara kwa mara ndani ya muda mfupi kisha kutulia kulingana na chanzo husika cha tatizo hili.


BAADHI YA SABABU AMBAZO HUWEZA KUCHANGIA MTU KUPATWA NA TATIZO LA KUISHIWA NGUVU MWILINI NI PAMOJA NA;


1. Mtu kupatwa na magonjwa mbali mbali kama vile;


• Ugonjwa wa Malaria,UTI,PID n.k


• Magonjwa mbali mbali ya Moyo ikiwa ni pamoja na mishipa ndani ya moyo kuziba, shambulio la moyo yaani Heart attack n.k


• Aina mbali mbali za kansa au saratani


• Magonjwa ya mfumo wa upumuaji pamoja na mapafu kama vile; pneumonia n.k


• Mtu kupatwa na tatizo la STROKE(kiharusi), Mishipa ya damu kichwani kupasuka na kuanza kuvuja damu kwenye Ubongo


• Kuwa na tatizo la Presha au shinikizo la Damu


• Magonjwa ya mfumo wa kinga ya mwili yaani Autoimmune diseases kama vile; LUPUS, MULTIPLE SCLEROSIS n.k


• Kuwa na tatizo la kuishiwa na damu mwilini yaani ANEMIA


2. Sababu zingine ni kama vile;


• Mtu kupatwa na tatizo la kuishiwa na Maji mwilini


• Dalili za tatizo la msongo wa mawazo,sonona au Hofu kuu


• Madhara ya Baadhi ya Dawa, ikiwa ni pamoja na mtu kuoverdose dawa au kutumia dawa zisizosahihi kulingana na tatizo lake


• Ulaji wa vyakula vingi ambavyo husababisha kuongezeka kwa kiasi kikubwa cha Insulin mwilini hali ambayo hupelekea kushuka kwa SUKARI mwilini kwa kasi zaidi, tatizo ambalo hupelekea mtu kuanza kuishiwa na nguvu mwilini


• Ulaji wa nyama kwa wingi zaidi kuliko vyakula vingine, hali ambayo hupelekea uzito wa mwili kuongezeka sana, lakini kuishiwa na nguvu mwilini


• Mtu kupatwa na tatizo la kutokupata usingizi wa kutosha kila siku


• Mwili kukosa kabsa mazoezi hasa kwa watu ambao hufanya kazi za kukaa kwa muda mrefu

N.k


KUMBUKA; Tatizo la kuishiwa nguvu mwilini husababishwa na sababu nyingi sana,hivo kujua chanzo na kupata tiba sahihi lazima uongee na wataalam wa afya kwanza.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

MADHARA YA DAWA ZA KUREFUSHA MAISHA(ARV'S) NA JINSI YA KUKABILIANA NAYO(Ukimwi)Afyaclass Bongo Social •

ARV's

• • • • •

MADHARA YA DAWA ZA KUREFUSHA MAISHA(ARV'S) NA JINSI YA KUKABILIANA NAYO(Ukimwi)


 Hapa kuna athari mbali mbali zinazotokana na matumizi ya dawa za kurefusha maisha(ARV'S) kwa Wagonjwa wa UKIMWI na vidokezo vya jinsi ya kuzidhibiti Madhara hayo.


 • Kupoteza hamu ya kula


 Mifano ya dawa ambazo zinaweza kusababisha ni pamoja na:


- abacavir (Ziagen)


 - zidovudine


✓ Nini kinaweza kusaidia kudhibiti hali hii:


 Kula chakula kidogo kidogo mara kwa mara kwa siku badala ya kula chakula kingi kwa mara moja.


 Kula vyakula vilaini au chakula chenye virutubisho vya lishe ili kuhakikisha mwili unapata vitamini na madini ya kutosha.


 Uliza mtoa huduma wa afya au daktari wako juu ya kuchukua dawa za kuongeza hamu ya kula.


 • Lipodystrophy


 Lipodystrophy ni hali inayosababisha watu kupoteza au kupata mafuta katika sehemu fulani za mwili.  Hii inaweza kuwafanya watu wengine wajisikie wasiwasi au hofu kubwa kila mara.


 Mifano ya dawa ambazo zinaweza kusababisha madhara haya ni pamoja na: Mchanganyiko wa dawa kutoka kwa kichocheo cha nucleoside / nucleotide reverse transcriptase (NRTI) pamoja na dawa jamii ya kizuizi cha protease.


 NRTI ni pamoja na:


 - abacavir


 - stavudine


 - didanosini


 - zidovudine


- lamivudine


- emtricitabine


 - tenofovir


 Vizuizi vya Protease ni pamoja na:


- atazanavir


 - darunavir


 - fosamprenavir


 - indinavir


 - lopinavir


 - nelfinavir


- ritonavir


- saquinavir


- tipranavir


 ✓ Nini kinaweza kusaidia kudhibiti hali hii:


 Mazoezi yanaweza kusaidia kupunguza mafuta mwilini kutoka kwa mwili mzima, pamoja na maeneo ambayo mafuta yamejijengea.


 Dawa ya sindano inayoitwa tesamorelin (Egrifta) inaweza kusaidia kupunguza mafuta mengi ya tumbo kwa watu wanaotumia dawa za VVU.  Walakini, wakati watu wanaacha kuchukua tesamorelin, mafuta ya tumbo yanaweza kurudi.


 Liposuction inaweza kuondoa mafuta katika maeneo ambayo yamejikusanya.


 Ikiwa kupoteza uzito kunatokea, mtoa huduma ya afya anaweza kutoa habari juu ya sindano za asidi ya polylactic n.k


 Watu wenye ugonjwa wa sukari na VVU wanaweza kufikiria kuuliza mtoa huduma wao wa afya juu ya kuchukua metformin.  Dawa hii ya kisukari inaweza kusaidia kupunguza mafuta ya tumbo yanayosababishwa na lipodystrophy.


 • Kuhara


 Mifano ya dawa ambazo zinaweza kusababisha tatizo hili ni pamoja na:


- vizuizi vya protease


- vizuizi vya nucleoside / nucleotide reverse transcriptase (NRTIs)


 - delavirdine


 - raltegravir


- elvitegravir / cobicistat


 ✓ Nini kinaweza kusaidia kudhibiti hali hii:


 Epuka Kula vyakula vyenye mafuta mengi, vikali au vyenye viungo vingi/vyenye pilipili nyingi, na vya maziwa, pamoja na vyakula vya kukaanga na bidhaa zilizo na maziwa.


 Kula vyakula vichache vilivyo na nyuzi nyingi au fibers, kama mboga za majani matunda kama machungwa,maembe n.k, nafaka na karanga.


 Uliza mtoa huduma ya afya juu ya faida za kuchukua dawa za kukabiliana na kuharisha, kama vile loperamide (Imodium).


 • Uchovu


 Uchovu ni mojawapo ya athari za matibabu ya baadhi ya dawa za VVU.


 Mifano ya dawa ambazo zinaweza kusababisha shida hii ni pamoja na:


 - zidovudine


 - efavirenz


 ✓ Nini kinaweza kusaidia kudhibiti hali hii:


 Kula vyakula vyenye virutubisho kamili na vya kuongeza nguvu.


 Fanya mazoezi mara kwa mara angalau kwa dakika 30 au nusu saa kila siku.


 Epuka kuvuta sigara na kunywa pombe.


 Zingatia ratiba ya kulala na epuka kufanya vitu vinavyochangia kukosa usingizi.


 • Viwango vya juu kuliko kawaida vya cholesterol na triglycerides


 Mifano ya dawa ambazo zinaweza kusababisha tatizo hili ni pamoja na:


 - stavudine


 - didanosini


 - zidovudine


 - efavirenz


 - lopinavir / ritonavir


 - fosamprenavir


 - saquinavir


 - indinavir


- tipranavir / ritonavir


- elvitegravir / cobicistat


✓ Nini kinaweza kusaidia kudhibiti hali hii:


 Epuka kuvuta sigara.


 Fanya mazoezi mara kwa mara


 Punguza kiwango cha mafuta kwenye lishe.  Ongea na mtaalam wa lishe kuhusu njia salama zaidi ya kufanya hivyo.


 Kula samaki na vyakula vingine vyenye asidi ya mafuta ya omega-3.  Hizi ni pamoja na walnuts, mbegu za kitani, na mafuta ya canola.


 Fanya vipimo vya damu kuangalia viwango vya cholesterol na triglyceride mara nyingi kama mtoaji wa huduma ya afya anavyopendekeza.


 Chukua statins au dawa zingine ambazo hupunguza cholesterol ikiwa imeamriwa na mtoa huduma ya afya.


Kumbuka, watu walio na VVU wanapaswa kuongea kwanza na mtoa huduma wao wa afya au daktari kabla ya kujaribu Njia yoyote kati ya hizi.  Mtoa huduma ya afya ndiye atakayeamua  chaguo salama kwako kulingana na tatizo lako pamoja na hali yako.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

CHANZO CHA TATIZO LA MTOTO KUKOHOA MFULULIZOAfyaclass Bongo Social •

  KIKOHOZI

• • • • •

CHANZO CHA TATIZO LA MTOTO KUKOHOA MFULULIZO


Tatizo hili la mtoto kukohoa mfululizo huweza kuambatana na matatizo mengine kama vile kuharisha,kutapika,homa n.k


Je nini chanzo cha shida hii kwa watoto? na kitu gani cha kufanya ikiwa mtoto wako ana shida hii? soma hapa kwenye makala hii..!!


CHANZO CHA TATIZO LA MTOTO KUKOHOA MFULULIZO


Zipo sababu mbali mbali ambazo huweza kuchangia uwepo wa shida hii kwa watoto kama vile;


1. Maambukizi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa kama bacteria,fangasi,au virusi kwenye mfumo mzima wa koo la hewa.


2. Mtoto kuwa na Tatizo la acid kupanda kutoka tumboni yaani kwa kitaalam ACID REFLUX huweza kusababisha mtoto kuanza kukohoa mfululizo, kutapika mara kwa mara,kupatwa na kiungulia n.k


3. Mtoto kuwa na ugonjwa wa asthma


4. Mtoto kuwa na tatizo la Allergies(mzio) juu ya vitu mbali mbali kama vumbi, marashi, n.k


Hali hii huweza kuambatana na kikohozi cha mfululizo, kuwashwa kooni, kutokwa na machozi, kuanza kupata upele kwenye ngozi au rashes, pua kuvimba n.k


5. Mtoto kuwa na ugonjwa wa Kifaduro ambapo kwa kitaalam hujulikana kama whooping cough au Pertussis.


6. Pamoja na sababu zingine kama vile; matatizo ya kurithi baadhi ya vinasaba vya tatizo hili katika ukoo au familia flani n.k


UKIONA MTOTO ANA DALILI KAMA HIZI HAPA CHINI AWAHI HOSPITALINI


- Kikohozi ambacho kinaambatana na tatizo la kushindwa kupumua au kukosa pumnzi


- Kikohozi ambacho kinaambatana na tatizo la kupaliwa kila mara


- Kikohozi ambacho kinaambatana na tatizo la mtoto kutapika mfululizo


- Kikohozi ambacho kinaambatana na tatizo la uchovu wa mwili kupita kiasi,mwili kukosa nguvu n.k


- Kikohozi ambacho kinaambatana na shida ya kubadilika rangi kwa ngozi kwenye lips za mdomo pamoja na kucha kuwa Blue


Mtoto anatakiwa kwenda hospital kwa ajili ya vipimo ili kupata tiba sahihi kulingana na chanzo cha tatizo lake.


KIKOHOZI HIKI HUWEZA KUAMBATANA NA SHIDA ZINGINE KAMA VILE:


✓ mtoto kupiga chafya mara kwa mara


✓ mtoto kuchoka sana


✓ mtoto kuvimba pua


✓ mtoto kuwa na homa


✓ mtoto kukosa kabsa hamu ya kula chakula


✓ mtoto kuharisha


✓ mtoto kutapika

N.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comment

Mtoto kukojoa kwa shida au kushindwa kukojoaAfyaclass Bongo Social •

 MTOTO

• • • •

Mtoto kukojoa kwa shida au kushindwa kukojoa


Kwa namna moja au nyingine tatizo hili la mtoto kushindwa kukojoa au kupata shida sana wakati wa kukojoa huweza kutokea bila kujali umri wa mtoto wala jinsia yake.


HIZI HAPA CHINI NI BAADHI YA SABABU AMBAZO HUWEZA KUCHANGIA UWEPO WA TATIZO HILO KWA MTOTO


1. Maambukizi ya magonjwa kwenye mfumo mzima wa mkojo yaani UTI n.k


2. Kuwepo kwa tatizo la kupata choo kigumu sana kwa mtoto yaani Constipation


3. Mtoto kupatwa na hofu kuu pamoja na wasi wasi kutokana na hali anayopitia kwa wakati huo pamoja na mazingira aliyopo


4. Matumizi ya vinywaji vyenye kiwango kikubwa cha Caffeine mara kwa mara


5. Matatizo kwenye mfumo wa fahamu ikiwa ni pamoja na magonjwa(nerves diseases), Kuumia uti wa mgongo n.k


6. Kuwa na tatizo la kukuwa kwa tezi la Prostate


7. Upasuaji unaohusisha mfumo mzima wa mkojo


8. Matumizi ya baadhi ya Dawa


9. Kuwa na tatizo la mawe kwenye figo yaani Kidney stones


10. Kuwa na tatizo la Rectocele


11. Mrija wa mkojo kuwa mwembamba kuliko kawaida(Urethral stricture) au kuziba kabsa. N.k


Ni vigumu sana kugundua chanzo cha tatizo hili kwa mtoto wako kama huna utaalam huo,hivo ni muhimu sana kuongea na wataalam wa afya ili kujua chanzo cha shida hiyo pamoja na kupata vipimo na Tiba kwa mtoto wako.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comment

TATIZO LA KICHWA CHA UUME KUWA CHEKUNDU,KUWASHA AU KUVIMBAAfyaclass Bongo Social •

TATIZO LA KICHWA CHA UUME KUWA CHEKUNDU,KUWASHA AU KUVIMBA


Tatizo hili la kichwa cha uumwe kuwasha,kuvimba au kuwa chekundu kwa kitaalam hujulikana kama Balanitis.


Tatizo hili hutokea kwa asilimia 10% ya wanaume katika maisha yao, huku idadi kubwa ikiwa ni wale ambao hawajatahiriwa pamoja na wale wenye umri mdogo wa chini ya miaka 4. Japo pia hata wengine hupatwa na tatizo hili.


DALILI ZA TATIZO HILI


Tatizo hili huweza kuambatana na Dalili mbali mbali kama vile;


- Kupata maumivu


- Kichwa cha uume kuwasha sana


- Kichwa cha uume kubadilika rangi na kuwa chekundu


- Kichwa cha uume kuvimba


- Mara chache kupata maumivu wakati wa kukojoa kama vile mtu mwenye shida ya UTI


- Kupata vidonda kwenye kichwa cha uume


- Kutoa harufu mbaya kwenye uume


- Kutoa uchafu mweupe chini au kuzunguka ngozi ya uume

N.k


CHANZO CHA TATIZO HILI


Zipo sababu mbali mbali ambazo huchangia uwepo wa tatizo hili kama vile;


1. Mwanaume kutojisafisha vizuri sehemu za siri au uchafu(poor hygiene)


2. Mwanaume kutokutahiriwa


3. Kupata maambukizi ya fangasi sehemu za siri yaani Candidiasis or Genital Yeast Infection


4. Kupatwa na magonjwa mbali mbali ya Zinaa(STD's)


5. Kuwa na tatizo la Scabies


6. Kuwa na tatizo la Allergy ya vitu mbali mbali kama vile sabuni,mafuta,maji n.k


7. Kuwa na magonjwa mengine ya ngozi kama vile Psonosis au Eczema N.K


WANAUME AMBAO WAPO KWENYE HATARI YA KUPATWA NA TATIZO HILI NI PAMOJA NA;


• Wanaume wachafu


• Wanaume ambao hawajatahiriwa


• Wanaume wenye tatizo la sukari, kwani kuongezeka kwa sukari kwenye ngozi huhamasisha bacteria pamoja na fangasi wazaliane kwa haraka na wafanye mashambulizi kwa kasi zaidi


• Wanaume wanene kupita kiasi


• Wanaume wanaopatwa na magonjwa ya zinaa mara kwa mara


• Wanaume wenye tatizo la allergy ya vitu mbali mbali

N.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

MSONGO WA MAWAZO HUSABABISHWA NA NINI?Afyaclass Bongo Social •

MSONGO WA MAWAZO

• • • • • • •

MSONGO WA MAWAZO HUSABABISHWA NA NINI?


Tatizo la msongo wa mawazo huweza kumpata mtu yoyote kulingana na hali anayopitia au mazingira aliyopo kwa wakati huo, katika makala hii tunachambua baadhi ya sababu au vyanzo vya kusababisha tatizo la msongo wa mawazo kwa watu, na dalili za mtu mwenye msongo wa mawazo.


✓ Je tatizo la msongo wa mawazo huweza kusababishwa na nini?


✓ Je utamjuaje mtu mwenye tatizo la msongo wa mawazo?


BAADHI YA SABABU KUU ZA KULETA TATIZO LA MSONGO WA MAWAZO KWA WATU NI PAMOJA NA;


1. Mtu kupitia hali ngumu ya maisha ikiwemo kuwa na kipato kidogo sana au kuporomoka kiuchumi kwa gafla


2. Mtu kufukuzwa kazi au kusimamishwa kazi ambayo alikuwa anaitegemea kwenye maisha yake


3. Mwanafunzi kufeli mtihani,kudisco kwa wanachuo, au kufukuzwa shule kwa sababu mbali mbali kama vile; kubeba ujauzito wakati akiwa shuleni n.k


4. Matatizo kwenye mahusiano ya kimapenzi ikiwa ni pamoja na; kuachwa, kupigwa, kusalitiwa n.k


5. Matatizo na migogoro ndani ya ndoa


6. Kutokuelewana kati ya wanandugu wa karibu sana kwenye familia


7. Kubanwa na shughuli nyingi sana huweza kukuletea tatizo la msongo wa mawazo pia


8. Mama kuzaa mtoto mwenye matatizo kama vile magonjwa flani,udhaifu au ulemavu flani huweza kusababisha tatizo la msongo wa mawazo kwa mama na familia kwa ujumla


9. Kuwa na tabia ya kutamani vitu ambavyo huna uwezo navyo


10. Kutaka kila kitu kifanyike kwa usahihi unaotaka wewe bila kuwa na kasoro au makosa yoyote n.k


BAADHI YA DALILI ZA MTU MWENYE TATIZO LA MSONGO WA MAWAZO


- Mtu kufanya kitu kimoja kwa muda mrefu sana kuliko kawaida,mfano; mtu anaweza kufanya kazi ya kufagia chumba kimoja tu kwa zaidi ya masaa mawili


- Mtu Kuwa na tatizo la kukosa usingizi


- Mtu kuomba msamaha kila mara hata kwa vitu ambavyo kwa hali ya kawaida sio makosa


- Mtu kuanza kuongea mwenyewe


- Mtu kuwa na wasiwasi pamoja na hofu kubwa


- Mtu kukasirika kwa haraka zaidi kwa vitu vidogo sana,tabia ambayo hakuwa nayo hapo kabla


- Mtu kuhisi uchungu pamoja na kuonewa kila mara


- Mtu kujiona hawezi kufanya chochote


- Mtu kuanza kukaa peke yake na kusononeka muda wote,tabia ambayo hakuwa nayo hapo kabla


- Mtu kuanza kuongea maneno ya kukata tamaa ya maisha,kutaka kujidhuru au kujiua N.k


Mtu mwenye dalili kama hizi anahitaji msaada wa haraka zaidi ili asijepatwa na madhara makubwa zaidi.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Bongo Social Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Bongo Social ASANTE.
UNDERSTOOD