Msanii Mkongwe wa Filamu Tanzania Hashim Kambi Afariki Dunia
Tasnia ya filamu nchini Tanzania imepata pigo baada ya taarifa kuthibitisha kifo cha msanii mkongwe Hashim Kambi aliyefariki dunia leo tarehe 27 Aprili 2026.
Taarifa hizo zimethibitishwa na msemaji wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Coletha Raymond, kupitia mahojiano yake na vyombo vya habari.
Kwa mujibu wa Coletha, marehemu alikuwa ametokea mkoani Tabora kwa shughuli za kikazi, na baada ya kurejea aliendelea moja kwa moja kwenye kazi nyingine eneo la Pilipili. Akiwa huko, alidaiwa kuanza kujisikia vibaya kabla ya kukimbizwa hospitalini, ambapo baadaye alifariki dunia.
Imeelezwa kuwa marehemu alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya presha pamoja na kisukari kwa kipindi fulani.
Shirikisho la Filamu Tanzania limeeleza kuwa linaendelea na vikao vya ndani ili kupanga taratibu zote zinazohusu mazishi pamoja na kutoa taarifa rasmi zaidi kwa umma.
Kifo cha Hashim Kambi ni pigo kubwa kwa wadau wa sanaa na mashabiki wa filamu nchini, kutokana na mchango wake mkubwa alioutoa katika kukuza tasnia hiyo kwa miaka mingi.
Tunatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na wadau wote wa sanaa nchini.
You, Mehreen and others


.jpg)