Afyaclass Bongo Social Watu 20 wamepoteza maisha na wengine 70 kujeruhiwa kwa mafuriko Manyara,Rais. Samia Suluhu Hassan, ametoa salamu za pole

”Kwa masikitiko makubwa tumepokea taarifa za kutokea kwa mvua kubwa katika mkoa wa Manyara na kuleta madhara makubwa katika kijiji cha Katesh,mimi na wenzangu tunatoa pole sana.”

Amesema ametoa maelekezo nguvu zote za serikali zielekezwe huko kwenye shughuli za uokoaji ili kuzuia maafa zaidi kutokea.

”Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama tayari nimevielekeza vifike huko, wizara ya afya kushughulikia majeruhi,lakini pia wizara ya madini kuona kinachorokea katika sehemu ambayo milima imeonesha kutetemeka, imeonesha kuporomoka” alisema Rais Samia.

Watu 20 wamepoteza maisha na wengine 70 kujeruhiwa kutokana na mafuriko katika eneo la Katesh na Gendabi wilayani Hanang mkoani Manyara, Gazeti la Mwananchi limeripoti.

Taarifa za awali zinasema kuporomoka kwa sehemu ya Mlima Hanang ndio chanzo cha mafuriko hayo.

Mvua iliyonyesha usiku wa kuamkia leo jumapili imesababisha mafuriko ya tope katika eneo hilo.

Via: Bbc

You, Mehreen and others
Hashtag:

WEKA MAONI HAPA(Reply)

Notification
Karibu Afyaclass Bongo Social Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Bongo Social ASANTE.
UNDERSTOOD