Gaza: Watoto 57 wameripotiwa kufariki dunia kutokana na utapiamlo, yasema WHO

Gaza: Watoto 57 wameripotiwa kufariki dunia kutokana na utapiamlo, yasema WHO

#1

Gaza: Watoto 57 wameripotiwa kufariki dunia kutokana na utapiamlo, yasema WHO



Gaza: Watu wamenaswa katika mzunguko wa ukosefu wa chakula cha mseto, na kusababisha utapiamlo na magonjwa.

Huko Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa na Israeli, watoto wenye utapiamlo kutokana na njaa wanafariki dunia huku wale wanaonusurika wakikabiliwa na matatizo makubwa ya kiafya, imesema taarifa iliyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO.

Tangu kuanza kwa kizuizi cha misaada tarehe 2 Machi, watoto 57 wameripotiwa kupoteza maisha kutokana na athari za utapiamlo, kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Palestina Ikiwa hali itaendelea, karibu watoto 71,000 walio na umri wa chini ya umri wa miaka 5 wanatarajiwa kuathirika na utapiamlo mkali katika kipindi cha miezi 11 ijayo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, Mwakilishi wa WHO kutoka eneo linalokaliwa la Palestina, Dkt. Rik Peeperkorn, amesema kuwa marufuku kamili ya misaada iliyowekwa na Israel imeliacha shirika hilo na vifaa vichahe vya kutibu watoto 500 tu walio na utapiamlo mkali sehemu ndogo sana ikilinganishwa na hitaji halisi. Watu wamekwama kwenye mzunguko huu ambapo ukosefu wa chakula bora, utapiamlo na magonjwa vinachocheana,” ameonya.

Kauli ya Dkt. Peeperkorn imekuja kufuatia kuchapishwa kwa uchambuzi mpya wa kiwango cha tahadhari ya uhakika wa chakula kinachoungwa mkono na Umoja wa Mataifa, au IPC, kinachoonesha kuwa mtu mmoja kati ya watano Gaza, yaani watu 500,000 wanakabiliwa na njaa kali, huku watu wote milioni 2.1 wa Ukanda huo wakikumbwa na uhaba mkubwa wa chakula.

Janga la njaa linaongezeka

Hili ni moja ya Janga kubwa la njaa duniani, likijitokeza kwa wakati halisi,” amesema Dkt. Peeperkorn.


Watoto waliopoteza makazi yao wakiwa katika mji wa Gaza.

Ameelezea ziara yake ya hivi karibuni katika hospitali ya Kamal Adwan kaskazini mwa Gaza, ambapo kila siku watoto zaidi ya 300 hupimwa katika kituo cha lishe kinachoungwa mkono na WHO. Wakati wa ziara hiyo, hospitali iliripoti zaidi ya asilimia 11 ya visa vya utapiamlo mkali wa kiwango cha dunia.

Akielezea hali ya watoto waliothirika, amesema, “Nimemuona wodini… Mtoto mwenye umri wa miaka mitano, na nilifikiri ana umri wa miaka miwili na nusu.”

WHO inaunga mkono vituo 16 vya matibabu ya utapiamlo vya wagonjwa wa nje na vituo 3  vya wagonjwa wa kulazwa katika eneo hilo kwa kuwapa vifaa vya kuokoa maisha, lakini kusitishwa kwa misaada na kupungua kwa upatikanaji wa msaada wa kibinadamu kunatishia uwezo wa shirika hilo kuendeleza shughuli hizo.

Dkt. Peeperkorn amesisitiza madhara ya muda mrefu ya utapiamlo ambayo “yanaweza kudumu maisha yote, yakiwemo kudumaa kwa ukuaji, matatizo ya kiakili na kiafya.

Ameonya kuwa Bila chakula chenye virutubisho vya kutosha, maji safi, na huduma za afya, kizazi kizima kitaathirika milele”.

Mwakilishi huyo wa WHO amesema kuwa shirika hilo linaendelea kuwasiliana mara kwa mara na mamlaka za Israel juu ya umuhimu wa kuingiza misaada Gaza. Takribani malori 31 ya WHO yamesimama katika eneo la Al-Arish nchini Misri, karibu na mpaka wa Rafah, na misaada mingine iko Ukingo wa Magharibi, tayari kusafirishwa “siku yoyote itakaporuhusiwa”.

Huduma za afya si lengwa

Akizungumzia mashambulizi dhidi ya vituo vya afya, Dkt. Peeperkorn amesema kuwa kitengo cha kutibu majeraha ya moto cha Hospitali ya Nasser mjini Khan Younis kilishambuliwa kwa bomu leo Jumanne, na kusababisha vifo vya watu wawili na kujeruhi wengine 12. Shambulio hilo lilipunguza vitanda 18 vya hospitali katika idara ya upasuaji, ikiwemo vitanda vinane vya wagonjwa mahututi.

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa mwandishi mmoja wa habari wa Palestina aliuawa katika shambulio hilo wakati akipata matibabu ya majeraha aliyopata kwenye shambulio la awali.

“Huduma za afya si lengwa,” amehitimisha Dkt. Peeperkorn. Amesisitiza wito wa kulindwa kwa vituo vya afya, kusitishwa mara moja kwa kizuizi cha misaada, kuachiliwa kwa mateka wote wanaoshikiliwa na makundi yenye silaha ya Kipalestina, na kutekelezwa kwa usitishaji wa mapigano “unaopaswa kuleta amani ya kudumu.”

♦ Via UN

Reply


image quote pre code
مشاركة: