Afyaclass Bongo Social Tamko Kali latolewa na Raisi wa Israel baada ya Shambulio La Iran Kulenga Hospitali



Rais wa Israel, Isaac Herzog, ametoa tamko lenye hisia kali na ujumbe mzito wa mshikamano baada ya Kituo cha Matibabu cha Soroka mjini Be’er Sheba kulengwa katika shambulio la makombora lililotekelezwa na Iran mapema asubuhi ya leo. 

Akiandika kupitia mitandao ya kijamii, Rais Herzog alieleza kwa majonzi jinsi shambulio hilo lilivyolenga moja kwa moja raia wa kawaida, wakiwemo watoto wachanga, akina mama, wazee na wahudumu wa afya, huku akitaja hospitali hiyo kama “beacon ya matumaini na maelewano” kati ya Wayahudi, Waarabu na hata Wapalestina kutoka Ukingo wa Magharibi na Gaza.

Katika ujumbe wake wa kina, Rais Herzog alieleza:
“Mtoto mchanga akiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi. Mama yake akiwa kando yake, akimlinda kwa machozi na maombi. Daktari akiharakisha kati ya vitanda, akijaribu kuokoa maisha. Mkazi mzee akiwa katika nyumba ya uangalizi ya karibu, hawa si wapiganaji, hawa si malengo ya kijeshi, hawa ni raia. Wao ndio walengwa wa shambulio hili la Iran dhidi ya watu wasio na hatia.”

You, Mehreen and others

WEKA MAONI HAPA(Reply)

Notification
Karibu Afyaclass Bongo Social Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Bongo Social ASANTE.
UNDERSTOOD