Lenacapavir yaidhinishwa kama dawa mpya ya kukinga maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU)

Lenacapavir yaidhinishwa kama dawa mpya ya kukinga maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU)

#1
Fahamu Zaidi hapa Kuhusu Lenacapavir,Dawa mpya ambayo huweza kutumika kama Kinga ya VVU

Shirika la Chakula na Dawa la Marekani (FDA) limeiidhinisha sindano ya kampuni ya Gilead Sciences-Lenacapavir, kama dawa mpya ya kukinga maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) ambayo imechukuliwa kama matumaini makubwa katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI duniani.

Dawa hiyo hutolewa kwa sindano moja kila baada ya miezi sita na mara mbili kwa mwaka, jambo litakalopunguza mzigo wa kila siku wa kutumia dawa kama ilivyo kwa kinga nyingi za VVU zinazotumika hivi sasa.

Lenacapavir hufanya kazi kwa kuzuia sehemu ya protini ya virusi inayoitwa capsid, ambayo ni muhimu kwa virusi vya VVU kuweza kuishi na kujiiga ndani ya seli za mwili wa binadamu. 

Kwa kulenga capsid, Lenacapavir huzuia hatua mbalimbali za maisha ya virusi ikiwa ni pamoja na kuingia kwenye seli, kuiga muundo mpya, na kutoka nje ya seli ili kuambukiza zingine.

Tafiti zinaonesha kuwa Lenacapavir inaweza kutumika kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya VVU kwa watu walio katika hatari kubwa, ikiwa kama njia mpya ya PrEP (Pre-Exposure Prophylaxis).

FDA iliidhinisha matumizi ya Lenacapavir mwaka 2022 kwa wagonjwa waliokuwa na chaguzi chache za matibabu. Nchi mbalimbali barani Ulaya na Afrika pia zimeanza mchakato wa kuidhinisha na kuingiza dawa hiyo kwenye mifumo yao ya afya.

Hata hivyo Wizara ya Afya nchini Tanzania bado haijatoa tamko lolote juu ya uwepo wa dawa hizo na uthibitishwaji wake, hivyo wananchi wanapaswa kuendelea kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo.

REPLY HAPA


image quote pre code