Mmoja wa waigizaji kipenzi wa filamu za Kibabe ni Billy Drago

Mmoja wa waigizaji kipenzi wa filamu za Kibabe ni Billy Drago

#1

FILAMU za  ubabe haziwezi kunoga kama hakuna mwigizaji mahiri anayekuwa akitoa upinzani mkali kwa kinara mkuu yaani ‘steringi’ japo huwa hauawi. Hii ndio hufanya mashabiki kuwapenda waigizaji wanaocheza nafasi za ukatili katika filamu zao.

Mmoja wa waigizaji kipenzi wa filamu za aina hiyo ni Billy Drago ambaye katika filamu zake nyingi huigiza kama mtumiaji dawa za kulevya na mfanyabiashara wa dawa hizo ambaye huua huku akitabasamu, lakini sura yake pia imekaa kikatili katili na ki- ‘tejateja’. 

Huigiza nafasi ya ukatili na kwa kweli huwa ni katili hasa katika filamu zake. Agalia filamu Delta Force 2: The Colombian Connection alivyofanya unyama katika mapambano yake na Chuck Norris ambapo katika filamu hiyo ameigiza kama mmiliki na mfanyabiashara mkubwa wa dawa za kulevya.

Humo anamuua kinyama kibarua wake mmoja wa mashamba ya dawa za kulevya. Kisa?Mke wake alikwenda kumfariji, mkewe huyo alipotaka kulipa kisasi(mwishoni mwa filamu), anaishia kuchomwa jambia.

Mwangalie Billy Drago  alivyompeleka ‘mbaya’ Cynthia Rothrock katika filamu ya Lady Dragon, unapomkosea adhabu yake ni wee kujikata kidole mbele yake na bado atakwambia haitoshi! Huyu ndiye Billy Drago mwigizaji aliyetokea kupendwa katika filamu za ‘action’.

Ugizaji wake huo wa kikatili huku akiwa na uso wa tabasamu na masikhara wakati anafanya kweli ni staili iliwafanya mashabiki wengi kumpenda na kutaka kumuona katika kila filamu zake alizoigiza. 

Jina lake halisi ni  William Eugene Burrows, alizaliwa  Septemba 18, 1949, huko Hugoton, Kansas, Marekani na kuanza uigizaji mwaka 1979, alifariki dunia Juni 24, 2019. Isome zaidi katika gazeti mtandao la SpotiLeo la leo Novemba 10, 2025.

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code
مشاركة: