Ajali ya Shabiby Leo,Watu watano wafariki dunia papo hapo
Watu watano wamefariki dunia papo hapo na wengine zaidi ya 17 kujeruhiwa vibaya kufuatia ajali mbaya ya barabarani iliyohusisha basi la abiria la kampuni ya Shabiby na lori lililokuwa limebeba vinywaji baridi aina ya Pepsi.
Ajali hiyo imetokea katika Kijiji cha Tanangozi, Kata ya Mseke, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, baada ya magari hayo kugongana uso kwa uso.
Kwa mujibu wa taarifa za awali, lori hilo lilikuwa likitokea Mbeya kuelekea Dar es Salaam, huku basi la Shabiby likisafiri kutoka Dodoma kwenda Mbeya.
Majeruhi wamekimbizwa hospitalini kwa matibabu huku chanzo cha ajali hiyo kikiendelea kuchunguzwa na Jeshi la Polisi.





Post a Comment
"Karibu kutoa maoni yako. Kumbuka: Link zote za matangazo haziruhusiwi na zitafutwa kiotomatiki".