Bei ya Simu ya iPhone 17  Tanzania

Kwa mujibu wa vyanzo mbali mbali vya taarifa kampuni ya APPLE ilizindua rasmi simu mpya za mfululizo wa iPhone 17 mwezi Septemba 2025.

Japokuwa mabadiliko yake si makubwa sana ukilinganisha na iPhone 16, bado kuna maboresho kadhaa ambayo yanaweza kukuvutia kununua moja ya simu hizi mpya.

Hizi ndizo aina kuu za iPhone 17 pamoja na bei zake nchini Tanzania

Apple iPhone 17

Apple iPhone 17
Bei yake ni takribani shilingi milioni 3

Simu hii ina ukubwa wa inchi 6.3 ikiwa ni saizi ya wastani inayofaa watu wengi. Inakuja na RAM ya GB 8 pamoja na hifadhi ya GB 256 au 512.

Inatumia mfumo mpya wa iOS 26 na ina betri yenye uwezo wa mAh 3692. Kasi ya kuchaji ni hadi wati 25.

Kwa upande wa kamera, ina lenzi mbili zote zikiwa na uwezo wa 48MP kwa picha zenye ubora wa juu

Apple iPhone 17 Pro

Apple iPhone 17 Pro
Bei yake ni takribani shilingi milioni 4

Ina ukubwa sawa wa inchi 6.3 lakini ina nguvu zaidi kiutendaji. Inatumia chip aina ya Apple A19 Pro.

RAM yake ni GB 12 na ina betri ya mAh 3988. Pia inachaji hadi wati 25.

Tofauti kubwa ipo kwenye kamera ambapo ina kamera tatu za 48MP ikiwemo lenzi ya zoom inayosaidia kupiga picha za mbali kwa uwazi zaidi

Apple iPhone 17 Pro Max

Apple iPhone 17 Pro Max
Bei yake ni takribani shilingi milioni 4.5

Hii ndiyo simu kubwa zaidi kwenye mfululizo huu ikiwa na ukubwa wa inchi 6.9.

Ina betri kubwa zaidi inayofikia hadi mAh 5088 kwa baadhi ya matoleo. Pia ina RAM ya GB 12 na hifadhi kuanzia GB 256 hadi 1TB.

Utendaji wake ni wa juu sana kwa sababu ya chip ya A19 Pro na ina mfumo wa kamera tatu kama ilivyo kwa Pro

Apple iPhone Air

Apple iPhone Air
Bei yake ni takribani shilingi milioni 3.7

Toleo hili linajulikana kwa kuwa nyembamba zaidi kuliko zote.

Ina betri ndogo ya mAh 3149 na tofauti nyingine ni kwamba inatumia eSIM pekee badala ya laini za kawaida

NOTE:

Kwa ujumla iPhone 17 zimekuja na maboresho ya kawaida lakini bado zina ubora mkubwa kama ilivyo kawaida ya simu za Apple.

Kama unatafuta simu yenye bei nafuu unaweza kuchagua iPhone 17 ya kawaida, lakini kama unahitaji kamera bora na performance ya juu zaidi basi Pro au Pro Max zitakufaa zaidi.

WEKA COMMENT HAPA(Reply)

WEKA MAONI HAPA(Reply)