Fahamu Mambo Nane(8) ya kuacha ili usipate tatizo la Upungufu wa Nguvu za Kiume

Karibu tena Kwenye Page yetu ya Afyaclass, Leo nmekutajia mambo makuu(8) unayopaswa kuacha kabsa ili usije ukaingia kwenye tatizo la Upungufu wa nguvu za kiume, Tatizo ambalo huwasumbua wengi kwa hivi Sasa;

kuna mambo muhimu ya kuyaacha Kabsa au kuyaepuka au kuyapunguza kwa sababu yanaathiri moja kwa moja nguvu za Kiume.

Tuanze na Jambo la Kwanza;

1. Uvutaji sigara

Kwa nini uache:

Sigara huharibu mishipa ya damu na kupunguza mtiririko wa damu kwenda kwenye uume.

Inaathirije:

Uume unahitaji damu ya kutosha ili usimame. Sigara husababisha mishipa kubana au kwa kitaalama "vasoconstriction", hivyo kusababisha kushindwa kusimamisha uume au kusimama kwa muda mfupi.

2. Matumizi ya Pombe

Kwa nini uache:

Unywaji mwingi wa pombe hupunguza uwezo wa mfumo wa neva kufanya kazi vizuri.

Inaathirije:

  • Hupunguza hamu ya tendo la ndoa
  • Huathiri homoni za kiume (testosterone) na
  • kupunguza nguvu ya kusimamisha uume

3.Kupiga Punyeto

Hapa ndipo tatizo linaweza kuanza.

Inaathirije:

Kupunguza hamu ya tendo la ndoa na mwenza halisi,

Kuchoka kwa mfumo wa neva na mwili,Kuharibifu vishipa vidogo vidogo vya damu vyote hivi huweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume au

Uume kushindwa kusimama vizuri wakati wa tendo la ndoa.

4. Lishe duni (vyakula vya mafuta mengi na sukari nyingi)

Kwa nini uache:

Lishe mbaya huongeza hatari ya magonjwa kama

  • Kusuakri,
  • Shinikizo la Damu

Inaathirije:

Magonjwa haya huharibu mishipa ya damu na neva zinazohusika na kusimamisha uume.

5. Kukaa bila kufanya mazoezi

Kwa nini uache uvivu:

Kutofanya mazoezi hupelekea uzito kupita kiasi na mzunguko mbaya wa damu.

Inaathirije:

Damu haizunguki vizuri mwilini,

Hupunguza stamina na nguvu za mwili,

Huongeza hatari ya kupata Nguvu za kiume

6. Msongo wa mawazo (stress)

Kwa nini udhibiti:

Stress huathiri akili na homoni.

Inaathirije:

Huzuia ishara za neva zinazochochea uume kusimama,

Hupunguza hamu ya tendo la ndoa,

Husababisha tatizo la kisaikolojia hata kama mwili uko sawa

7. Kutotumia dawa kiholela

Kwa nini uache matumizi holela:

Kutumia Baadhi ya dawa bila ushauri wa daktari huathiri nguvu za kiume.

Dawa za kinyeji pia kama,Vumbi la 'Congo n.k,Usitumie Vitu hivi bila Ushauri wa Daktari

Inaathirije:

  • Hushusha libido au hamu ya kufanya tendo la ndoa
  • Huathiri mfumo wa neva na mishipa ya damu
  • Huchangia kushindwa kusimamisha uume

8. Kukosa usingizi wa kutosha

Kwa nini ubadilishe hili:

Usingizi mdogo huathiri uzalishaji wa homoni.

Inaathirije:

Hupunguza testosterone,

Huathiri nguvu za mwili na hamu ya tendo la ndoa

NB:Kuacha au kupunguza mambo haya kunaweza kusaidia sana kurejesha nguvu za kiume. Mara nyingi, mabadiliko ya mtindo wa maisha yanaweza kuwa tiba kubwa kuliko dawa.

Je,Unatatizo lolote na hujapata Tiba bado? kwa Ushauri Zaidi na Tiba tuwasiliane +255758286584.

WEKA COMMENT HAPA(Reply)

WEKA MAONI HAPA(Reply)