Hiki sio Cheti Chetu,Picha hii imehaririwa kidijitali na si cheti halisi kilichotolewa-UDSM
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimejitokeza hadharani kukanusha picha inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha kile kinachodaiwa kuwa ni cheti cha chuo hicho kikitumika kufungia maandazi, kikisema picha hiyo imehaririwa kidijitali na si cheti halisi kilichotolewa na taasisi hiyo.
Kupitia taarifa yake, UDSM imesema nyaraka hiyo imeundwa kwa lengo la kupotosha umma na kuchafua taswira ya chuo hicho, huku ikieleza kuwa vyeti vyake halisi vina alama maalum za usalama, mpangilio rasmi unaotambulika pamoja na utaratibu maalum wa saini za wahusika.
Chuo hicho pia kimebainisha kuwa saini ya Msajili inayoonekana kwenye picha hiyo si sehemu ya muundo wa vyeti vya kweli vya UDSM.
Aidha, UDSM imesisitiza kuwa vyeti vya taaluma ni matokeo ya juhudi na mafanikio ya muda mrefu ya wahitimu, hivyo vinapaswa kuheshimiwa na kuthaminiwa.
Chuo hicho kimelaani matumizi mabaya ya teknolojia za kidijitali na zana za Akili Mnemba (AI) katika kueneza taarifa za uongo, huku kikitoa wito kwa wananchi kupuuza na kutosambaza picha hiyo ya kughushi.





Post a Comment
Karibu Afyaclass Bongo Social,Share mawazo yako hapa au chochote kuhusiana na Makala husika,Karibu Sana Mdau Wetu Muhimu.