Imani baada ya kutokuona Matokeo uliyoyatarajia

Nazungumzia Imani yako baada ya kutokuona Matokeo uliyoyatarajia, Hali yako ya Imani Ipoje? baada ya kutokupata au kutokuona kile ulichokitarajia? inapanda au kushuka zaidi?..

Imani ni nini? Waebrania 11:1 inasema "Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana".

Imani yako baada ya kutokuona matokeo uliyoyatarajia ipoje?;Hatua hii ni muhimu sana kwani Watu wengi hupoteza tumaini katika kipindi hiki,

Uliomba sawa,ulifunga sawa,ulifanya kwa Imani,ukatoa mpaka sadaka kwa Imani, halafu hukupata matokeo uliyoyatarajia?

ZINGATIA VITU HIVI MUHIMU SANA KWAKO,KWENYE IMANI YAKO KATIKA KIPINDI KAMA HIKI:

1.Imani yako inatakiwa Iongezeke Zaidi badala ya Kupungua

Mkumbuke Eliya katika 1Wafalme 18:42, Maombi ya Eliya katika Kilele cha Mlima Karmeli akiomba mvua inyeshe baada ya kuacha kunyesha kwa muda wa miaka 3 na Miezi 6.  Biblia inasema" Basi Ahabu akainuka ili ale na kunywa. Naye Eliya akapanda juu mpaka kilele cha Karmeli; akasujudu kifudifudi, akainama uso mpaka magotini.

Akamwambia mtumishi wake, Kwea sasa, utazame upande wa bahari. Akakwea, akatazama, na kusema, Hakuna kitu. Naye akanena, Enenda tena mara saba.

Ikawa mara ya saba akasema, Tazama, wingu linatoka katika bahari, nalo ni dogo kama mkono wa mtu. Akanena, Enenda, umwambie Ahabu, Tandika, ushuke, mvua isikuzuie".

Nini nataka kusema,Aliomba mara ya kwanza hakuna kitu,hakupata matokeo aliyotarajia,Akazidi kuomba,Mpaka mara ya 7,Matokeo yakaonekana.

Je,Umeomba mara moja hakuna kitu? Omba mpaka kitokee kitu,Imani yako isishuke mpaka upate matokeo.. Kati ya Kipindi ambacho Imani yako inatakiwa kuwa juu ni pamoja na kipindi hiki ambacho umeomba na hakuna kitu.

2.Jua Mungu bado yupo hata kama majibu hayajaonekana,

Kumbuka; Mungu hafanyi kazi kwa hisia Zetu,bali kwa kusudi lake, Ukisoma habari za Petro na Yohana na kiwete kwenye Matendo 3:1-13"Bibilia inatuambia Palikuwa na Mtu mmoja kiwete toka tumboni,alikuwa anaomba Sadaka kwenye Mlango wa hekalu uitwao Mzuri,watu wanapoingia kusali.

Pengine mtu huyu alishakata tamaa ya Uponyaji ndiyo mana badala ya kutafuta uponyaji hekaluni anaomba sadaka, Lakini Kusudi la Mungu alitakiwa apone siku Petro na Yohana Wanafika kusali ili kuonyesha uhakika wa nguvu za Yesu na Mpango wa Mungu kwa watu wote waliokuwa shuhuda. Siku anaponywa ilikuwa injili kubwa kwa watu wote,na Watu waliokuwa na Mashaka na Nguvu za Mungu,wakaona matendo makuu ya Mungu.

3.Imani ya Kweli haitegemei Mazingira,

Imani yako haipaswi kushuka kwa Sababu ya mazingira kutokuleta matokeo uliyoyataka, Kumbuka Mungu ndiye Mleta matokeo,Hivo usiweke Imani yako kwenye Matokeo,Weka Imani yako kwa Mungu mleta matokeo.

Na Mungu akubariki sana kwa kusoma Ujumbe huu,Like,Comment na Share kwa wengine....🙏🙏🙏🙏

...more

WEKA COMMENT HAPA(Reply)

"Karibu kutoa maoni yako. Kumbuka: Link zote za matangazo haziruhusiwi na zitafutwa kiotomatiki".