Mashabiki Wamgeuka Mbappe Real Madrid, Kura Za Mtandaoni Zafika Milioni 50
Hali ndani ya klabu ya Real Madrid inaelezwa kuwa ya sintofahamu kufuatia presha kubwa kutoka kwa mashabiki wanaomlaumu straika nyota Kylian Mbappe kwa kile wanachodai kuwa kushuka kwa kiwango cha timu hiyo.
Licha ya Real Madrid kuwa moja ya vilabu vikubwa duniani vilivyojaa historia ya mafanikio, mataji pamoja na kupita kwa mastaa wengi maarufu, taarifa mbalimbali zinaonyesha kuwa kwa sasa kuna hali ya kutokuelewana ndani ya kikosi hicho huku mashabiki wakionyesha hasira zao waziwazi mitandaoni.
Mashabiki hao wameanzisha kampeni pamoja na kura za mtandaoni wakitaka Mbappe aondoke klabuni hapo, huku ripoti zikidai kuwa kura hizo zimefikia zaidi ya milioni 50, jambo linaloonyesha ukubwa wa presha anayokumbana nayo nyota huyo wa Ufaransa.
Mbali na hilo, taarifa nyingine zimeeleza kuwepo kwa mgogoro mkubwa kati ya viungo wawili wa timu hiyo, Federico Valverde na Aurelien Tchouameni, ambapo inadaiwa wawili hao walihusikana kwenye ugomvi mzito hadi kufikia kuumizana.
Hata hivyo, bado hakuna taarifa rasmi kutoka Real Madrid kuhusu madai hayo yanayoendelea kusambaa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo mbalimbali vya habari.
Swali kubwa linalobaki kwa sasa ni kama presha ya mashabiki itaweza kushawishi uamuzi wa baadaye kuhusu mustakabali wa Mbappe ndani ya Real Madrid.





Post a Comment
"Karibu kutoa maoni yako. Kumbuka: Link zote za matangazo haziruhusiwi na zitafutwa kiotomatiki".