Mmiliki wa Super Feo,Omary Malukus Msigwa,alianza biashara na mtaji wa elfu 20
Anaitwa Omary Malukus Msigwa, anayefahamika zaidi kwa jina la Super Feo, ameendelea kuwa miongoni mwa wafanyabiashara waliovutia wengi kutokana na safari yake ya mafanikio kutoka maisha ya kawaida hadi kuwa miongoni mwa matajiri wakubwa nchini.
Super Feo ambaye ni mmiliki wa kampuni ya usafirishaji ya Super Feo Express, anatajwa kuanza biashara akiwa na mtaji mdogo wa takribani shilingi 20,000 pekee. Kupitia juhudi, uvumilivu na biashara mbalimbali, ameweza kujenga himaya kubwa inayojumuisha mabasi ya abiria, malori, kiwanda cha unga pamoja na shule.
Safari yake imekuwa chanzo cha hamasa kwa vijana wengi wanaotafuta mafanikio kupitia biashara, huku wengi wakiamini kuwa nidhamu ya kazi na kutokata tamaa ni sehemu ya siri ya mafanikio yake.
Leo hii jina la Super Feo limeendelea kutambulika ndani na nje ya sekta ya usafirishaji kutokana na ukuaji mkubwa wa biashara zake na mchango wake kwenye ajira.
Vijana tusiogope kuanza na tulicho nacho mkononi...


.jpeg)



Post a Comment
Related Discussions...