Msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop nchini, Prof Jay, amepokea msaada wa Shilingi milioni 30 kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ikiwa ni sehemu ya kumwezesha kuendelea na maisha yake baada ya kutoka kwenye changamoto ya afya iliyokuwa ikimkabili.
Fedha hizo zilikabidhiwa leo Mei 10, 2026 na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma, aliyemtembelea Prof Jay akiwa ameambatana na Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Nurdin Bilal Juma (Shetta).
Katika ziara hiyo, ujumbe huo ulimfikishia Prof Jay salamu maalum kutoka kwa Rais Samia, huku ukieleza kuwa Serikali inaendelea kuthamini mchango wake mkubwa katika tasnia ya muziki na jamii kwa ujumla.
Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, Prof Jay amemshukuru Rais Samia kwa moyo wake wa upendo na namna alivyoendelea kumuunga mkono tangu alipokuwa akisumbuliwa na maradhi hadi aliporejea katika hali yake. Aidha, amewashukuru Watanzania waliokuwa wakimuombea na kumpa faraja katika kipindi chote cha changamoto alizopitia.
_____________________
#7mediaupdates

_1.jpeg)



Post a Comment
"Karibu kutoa maoni yako. Kumbuka: Link zote za matangazo haziruhusiwi na zitafutwa kiotomatiki".