Watu 15 Wafariki Baada ya Mgodi wa Dhahabu Kuporomoka Kenya

Watu 15 wamefariki dunia baada ya mgodi wa dhahabu kuporomoka katika eneo la Ramos, lililopo Kacheliba Constituency, kaunti ya West Pokot nchini Kenya.

Waathirika hao walikuwa miongoni mwa wachimbaji kadhaa waliokuwa wakifanya kazi ndani ya mgodi huo jioni ya Alhamisi kabla ya shimo hilo kuporomoka ghafla na kuwafunika chini ya vifusi.

Operesheni za uokoaji zimeendelea hadi Ijumaa zikihusisha maafisa wa Kenya Red Cross, wakazi wa eneo hilo pamoja na vyombo vya usalama huku juhudi zikifanyika kuhakikisha watu wote waliokuwa ndani ya mgodi huo wanapatikana.

Mamlaka nchini Kenya zimeanza uchunguzi wa tukio hilo huku hofu ikitanda kuwa huenda idadi ya waliofariki ikaongezeka kutokana na baadhi ya wachimbaji kuendelea kutafutwa chini ya vifusi.

Matukio ya migodi kuporomoka yamekuwa yakiripotiwa mara kwa mara katika baadhi ya maeneo ya uchimbaji madini nchini Kenya kutokana na changamoto za usalama na miundombinu mibovu kwenye maeneo hayo.

WEKA COMMENT HAPA(Reply)

"Karibu kutoa maoni yako. Kumbuka: Link zote za matangazo haziruhusiwi na zitafutwa kiotomatiki".