Showing posts with label Bei Mpya za Mafuta. Show all posts
Showing posts with label Bei Mpya za Mafuta. Show all posts

Bei Mpya za Mafuta Mwezi Disemba, 2025 zatangazwa na EWURAAfyaclass Forum •

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza kupungua kwa bei za mafuta nchini, hatua inayotokana na kushuka kwa gharama za uagizaji mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam kwa wastani wa 2.4% kwa petroli na 3.6% kwa mafuta ya taa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa tarehe 3 Desemba 2025 na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt. James Mwainyekule, bei mpya za rejareja zimeanza kutumika rasmi Desemba.

Mabadiliko ya Bei za Mafuta

Petroli

• Dar es Salaam: Punguzo la Sh 2.38 – bei mpya Sh 2,610.10

• Tanga: Punguzo la Sh 2.26 – bei mpya Sh 2,616.13

• Mtwara: Punguzo la Sh 2.45 – bei mpya Sh 2,616.24


Dizeli

• Dar es Salaam: Sh 2,639.54

• Tanga: Sh 2,648.86

• Mtwara: Sh 2,654.32


Mafuta ya taa

• Dar es Salaam: Punguzo kubwa la Sh 120.48 – bei mpya Sh 2,513.87

• Tanga na Mtwara: Hakuna mabadiliko ya bei kutoka mwezi uliopita.


EWURA Yasisitiza Uzingatiaji wa Sheria kwa Vituo vya Mafuta

EWURA imewakumbusha wafanyabiashara wa mafuta kuhakikisha wanatoa stakabadhi za mauzo zinazobainisha:

  • Jina la kituo
  • Tarehe ya ununuzi
  • Aina ya mafuta
  • Bei kwa kila lita

Stakabadhi hizi ni muhimu kama uthibitisho endapo kutatokea changamoto kuhusu huduma iliyotolewa.

Kadhalika, vituo vyote vya mafuta vimetakiwa kuchapisha bei za bidhaa kwenye mabango yanayoonekana wazi, yakionyesha bei halisi, punguzo na vivutio vingine vya kibiashara.

EWURA imeonya kuwa ni kosa kisheria kutoweka bango la bei katika eneo la kituo, na kwamba adhabu kali zitatolewa kwa yeyote atakayekiuka masharti hayo.








0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD