Aepuka kucheka wala kutabasamu kwa Miaka 40 ili kuzuia ngozi kuwa na mikunjo na kuzeeka
Ili kuzuia ngozi kuwa na mikunjo(wrinkles) au makunyanzi na kuonekana kama Mzee mkazi wa Uingereza, Tess Christian, ameripotiwa kuepuka kutabasamu au kucheka kwa miaka 40, akidumisha muonekano huo tangu ujana wake. Sasa akiwa na umri wa miaka 60, anasifu mbinu hii ya "Mona Lisa" eti kama Sababu ya kumfanya asiwe na mistari kwenye ngozi ya uso wake na kuwa mwonekano nzuri kama binti mdogo.
Ingawa hadithi yake imezua udadisi unaoenea, madaktari wa ngozi bado wana shaka. Wanasema mambo kama vile jeni, utunzaji wa ngozi, na kinga dhidi ya jua yana jukumu kubwa zaidi katika mchakato wa kuzeeka kuliko kukaa tu bila kucheka.
Sources: BBC News, The Telegraph, Daily Mail



image quote pre code