Showing posts with label Cheti cha kuzaliwa cha mtoto. Show all posts
Showing posts with label Cheti cha kuzaliwa cha mtoto. Show all posts

Cheti cha kuzaliwa cha mtoto,Maombi ya CHETI cha KuzaliwaAfyaclass Forum •

Cheti cha kuzaliwa cha mtoto,Maombi ya CHETI cha Kuzaliwa

Maelezo ya RITA juu ya Cheti cha Kuzaliwa na Upatikanaji wake.

Maombi ya Cheti cha Kuzaliwa

Usajili wa kuzaliwa unaweza kufanywa katika:

i.Katika kituo cha tiba au ngazi ya kitongoji kwa watoto wachanga (ndani ya siku 90)

ii.Katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya (usajili wa kuchelewa)

iii.Kwa mtandao (usajili wa kuchelewa, kubadilisha cheti cha zamani kuwa kipya)

Mtoto anasajiliwa mara tu baada ya kuzaliwa katika kituo cha tiba ambapo tukio la kizazi limetokea au katika Ofisi ya Mtendaji wa Kata kwa vizazi vya nyumbani. Ikiwa kwa sababu fulani mtu anakosa kusajili mahali hapo, mtoto anaweza kusajiliwa wakati wa chanjo ndani ya siku 90. Aidha, tukio la kuzaliwa linaweza kusajiliwa kama usajili wa kuchelewa katika Ofisi ya Katibu wa Wilaya kwa kupitia mtandao.

Mahitaji ya jumla kwa maombi ya cheti cha kuzaliwa:

Mwombaji lazima aambatishe baadhi ya hati mbili kati ya zifuatazo:

  • Kadi ya Kliniki ya Mama
  • Kadi ya Kliniki ya Mtoto
  • Tangazo la kuzaliwa
  • Cheti cha Ubatizo cha Mtoto (kwa wale walio batizwa wakiwa na umri mdogo)
  • Cheti cha Kumaliza elimu (Shule za Msingi au Sekondari - O Level)
  • Pasi ya kusafiria
  • Kadi ya mpiga kura
  • Cheti cha ubatizo

Pamoja na mojawapo ya haya:

  • Kitambulisho cha Kitaifa cha mzazi/mlezi
  • Hati ya kusafiria ya mzazi
  • Utambulisho kutoka Mtendaji wa Kata

N.B: Uhitaji wa kuweka vitambulisho vya wazazi vitatumika ikiwa wazazi wapo hai.

USAJILI UNAVYOFANYIKA KWA WATOTO WACHANGA
Mwombaji (Mzazi/mlezi) atasajili tukio hili kwenye dawati la Usajili katika Kituo cha tiba kizazi kilipotokea wakati mtoto anapozaliwa au wakati wa kupata chanjo. Pia Usajili unaweza kufanyika katika ofisi ya kata kwa vizazi vya nyumbani.

Soma Zaidi kwenye Ukurasa Wao: https://www.rita.go.tz/page.php?p=9

0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD