Showing posts with label Dawa ya red eyes. Show all posts
Showing posts with label Dawa ya red eyes. Show all posts

Red Eyes yapofusha Saba Dar wakati wakiitibuAfyaclass Forum •

Red Eyes yapofusha Saba Dar wakati wakiitibu

 Idadi inafanya jumla ya wagonjwa waliougua macho mekundu na kupata  madhara  kwa Tanzania Bara na Zanzibar kufikia 14.

Wizara ya Afya imesema watu saba jijini Dar es Salaam wamepata upofu kutokana na kutibu ugonjwa wa macho mekundu kwa njia za kienyeji, huku wawili kati yao vioo vya jicho vikitoboka.

Ugonjwa huo wa maambukizi kwenye ngozi ya juu ya gololi la jicho unaoitwa Conjunctivitis, maarufu Red eyes umesambaa mikoa 26 nchini.

Februari 7, 2024, mratibu wa huduma za afya msingi na matibabu ya macho Zanzibar, Dk Rajab Muhammed Hilali alitoa takwimu za watu saba kupata upofu baada ya matumizi ya dawa za kienyeji kutibu ugonjwa huo.

Athari za kutibu ugonjwa wa macho kwa njia asili

Idadi hiyo inafanya jumla ya wagonjwa waliopata madhara hasi kwa Tanzania Bara na Zanzibar kufikia 14.

Ugonjwa huo ulioripotiwa kwa mara ya kwanza Januari 13, 2024 athari zake hasi ni vidonda kwenye kioo cha jicho vinavyoweza kusababisha kovu kwenye jicho litakalomfanya mgonjwa apate uoni hafifu au kupoteze uwezo wa kuona kabisa.

Akizungumza na Mwananchi Digital, leo Jumapili Februari 18, 2024, Mkurugenzi wa Tiba, Wizara ya Afya, Profesa Paschal Ruggajo amesema hadi Februari 15, watu saba walitolewa taarifa ya kupata madhara kwenye vioo vya jicho.

“Watano wamepata vidonda kwenye kioo cha jicho na wawili walikutwa vioo vya jicho vimetoboka. Wagonjwa wote walionwa kwenye vituo vya tiba vilivyopo Dar es Salaam na umri wao ni kati ya miaka 21 hadi 42.

“Baadhi ya vitu vilivyotumika na waathirika hao ni pamoja na maji ya chumvi, tangawizi, maji ya majani ya mbaazi, vitunguu swaumu, chai ya rangi, vicks na dawa zenye viambata vya steroids,” amesema Ruggajo.

Profesa Ruggajo amesema wizara imeendelea kufuatilia mwenendo wa maambukizi na kutoa elimu kwa jamii kuhusu namna bora ya kujikinga na ugonjwa huo.

Amesema hadi Februari 15 2024, jumla ya wagonjwa 14,641 wametolewa taarifa, walioonwa katika vituo vya kutolea huduma za afya kwenye mikoa 26.

Dar es Salaam inaongoza kwa idadi ya wagonjwa 6,940, Pwani (4,480), Morogoro (630) na Dodoma (550).

Profesa Ruggajo amesema wizara inaendelea na hatua mbalimbali za kinga na udhibiti wa ugonjwa huo, ikiwamo utoaji wa elimu kwa kutumia wataalamu wa afya kupitia vyombo vya habari.

“Elimu inatolewa maeneo yenye mikusanyiko hususani shule, magereza na vyuo, nyumba za ibada, usambazaji wa vipeperushi na utoaji wa huduma za afya kwa wagonjwa kupitia vituo vyetu vya tiba na mitandao ya kijamii,” amesema.

Amesema wizara pia inaendelea kuratibu na kusimamia huduma mkoba za macho kwenye maeneo mbalimbali nchini na kubaini wagonjwa wenye shida ya macho mekundu na kuwapatia elimu.

“Hadi sasa vipindi vya kwenye runinga zaidi ya 20 vimetolewa na wataalamu wetu wa afya, redio za kijamii zaidi ya 25 kwenye mikoa mbalimbali, ikiwemo ambayo haina wagonjwa,” amesema.

Amesema wanafunzi wa shule za msingi na sekondari zaidi ya 25,000 wamefikiwa kwenye shule zao pamoja na walimu wao.

Profesa Ruggajo amesema wanaendelea kutoa elimu kuhusu madhara ya kutofuata kanuni zilizotolewa, baada ya kupata taarifa ya wagonjwa kutumia tiba zisizo rasmi na kupata madhara.

Kutokana na hilo, amesema wizara iliandaa video na kuirusha kwenye vyombo mbalimbali vya kuelimisha.

Akizungumza na Mwananchi Februari 8, 2024, Meneja Mpango wa Taifa wa Huduma za Macho, Wizara ya Afya, Dk Bernadetha Shilio alisema baadhi ya wagonjwa wanaopokewa kioo cha jicho kinabainika kumeharibika.

Amesema wagonjwa wa aina hiyo wanapotibiwa bado kunakuwa na kovu lenye rangi nyeupe kama karatasi ambalo likibaki hivyo moja kwa moja hupata ulemavu wa kutoona.

Matibabu sahihi:

Wizara inaelekeza hatua za kuchukua kwa kuosha uso kwa maji safi na sabuni mara kwa mara.

Tumia dawa ya paracetamol kumeza kwa ajili ya kupunguza maumivu

Nenda kituo cha tiba kwa ajili ya uchunguzi, kama hupati nafuu.

Hakikisha mikono na uso inakuwa safi muda wote.

Jizuie kugusa macho yako kadri uwezavyo.

Tumia vipukusi (vitakasa mikono) mara kwa mara.

Epuka kushikana mikono au kugusa vitu vinavyoguswa na wengi.

 Tumia taulo au leso za karatasi kufuta tongotongo au machozi.

Nenda kituo cha kutolea huduma mara upatapo dalili.

Kumbuka kufua mashuka na mataulo kila siku.

Via:Mwananchi

Soma Zaidi kuhusu Red eyes;

Red Eyes yapofusha Saba Dar wakati wakiitibu
0 Comment

Mkojo,Chumvi, kitunguu saumu sio dawa ya kutibu ‘red eyesAfyaclass Forum •

Mkojo,Chumvi, kitunguu saumu sio dawa ya kutibu ‘red eyes’

Wataalamu wasema zinachangia kuongeza maumivu, waonya zaweza kusababisha uoni hafifu na upofu.

Wataalamu wa afya na madaktari bingwa wa macho wamesema wanapokea idadi kubwa ya wagonjwa wakiwa katika hali ya ugonjwa mkali, kutokana na matumizi ya njia mbadala kutibu macho, ikiwamo matumizi ya mkojo na chumvi.

Hali hiyo imebainika siku 15 tangu kutangazwa kuibuka ugonjwa huo ujulikanao viral keratoconjunctivitis (red eyes) Januari 13, 2024 mkoani Dar es Salaam.

Wataalamu waliozungumza na Mwananchi Digital jana Januari 28, 2024 wameeleza wagonjwa wanaotumia chumvi, mkojo, chai ya rangi na kitunguu saumu kama tiba, macho yao huvimba na kuuma zaidi pamoja na kupatwa homa. Athari hasi zaidi zinazotajwa ni kusababisha vidonda kwenye kioo cha jicho.

Tiba hizo mbadala zinaelezwa zinaweza kusababisha kovu kwenye jicho litakalomfanya mgonjwa apate uoni hafifu au kupoteze uwezo wa kuona kabisa.

Daktari bingwa na mkuu wa kitengo cha macho kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Sarah Mrema ameisema idadi ya wagonjwa wanaohudhuria hospitalini hapo kutibiwa macho imekuwa ikiongezeka na kupungua.

Amesema wamekuwa wakipokea wagonjwa wakiwa tayari walianza kutumia tiba za majani ya chai, vitunguu saumu na chai ya rangi.

“Si kwamba wanapona wakitumia tiba mbadala, maumivu yanazidi, wakija hapa wanakuwa na maumivu makali. Ukihoji anakwambia alitumia mkojo, chumvi na njia nyingine nyingi. Unampa dawa anatumia, kisha anapona,” amesema Dk Sarah.

Kwa mujibu wa Dk Sarah, takwimu za hospitali hiyo zinaonyesha tangu Desemba 22, 2023 wagonjwa 105 walifika kutibiwa na kuna siku orodha ya wagonjwa inapanda na siku nyingine inapungua.

Daktari bingwa wa macho katika Hospitali ya Muhimbili-Upanga, Neema Moshi amesema unapotumia vitu vikali kutibu macho, ni rahisi kuharibu kioo cha mbele cha jicho na maumivu yanayotokea huwa makali.

Amesema wakati mwingine unaweza kupoteza uoni kwa sababu ya kuharibu kioo hicho.

“Tunapokea wagonjwa wengine wana hali mbaya, lakini hawezi kuwa mkweli, unajua mgonjwa hawezi kuja kusema alitumia kitu fulani, mara nyingi wanafichaficha labda tatizo liwe kubwa zaidi ndipo wanasema ukweli,” amesema.

Dk Neema amesema kama mgonjwa ametumia vitu hivyo na hajapata athari hawezi kupata athari baadaye.

“Si kwamba athari hizo zinakuwa za taratibu, kama amepona na haikuonekana kupata shida yoyote haiwezi kutokea tena baadaye,” amesema.

Meneja Mpango wa Taifa wa huduma za macho kutoka Wizara ya Afya, Dk Bernadetha Shilio amesema wapo wagonjwa wanaopata athari, lakini hawana takwimu, akisisitiza ni muhimu wagonjwa kuzingatia maelekezo ya wataalamu.

“Taarifa hizi zinatolewa na wataalamu wa afya, yaani madaktari kwenye vituo husika, labda mimi kuna mtu amekuja amefanya hivi na vile lakini kutoa hali ilivyo kwa sasa wangapi wamethirika kwa sasa bado.

“Hata leo nimepewa taarifa kuna mtu anatumia sijui vitu gani, lakini pia kuna taarifa za uvumi kuna mtu katoka huko anashauri wagonjwa wanywe Azuma inatibu, huo ni uongo,” amesema.

Dk Shilio amewataka wagonjwa waepuke kutibu macho kwa kutumia kitunguu saumu kwa kuwa kunaweza kusababisha michubuko kwenye ngozi ya jicho na kioo cha mbele ya jicho, hivyo kuathiri uwezo wa jicho kuona.

“Maji ya chumvi yanaweza kusababisha michubuko au kidonda kwenye kioo cha mbele cha jicho, hivyo kutengeneza kovu litakalopunguza uwezo wa jicho kuona au ulemavu wa kutoona wa kudumu,” amesema.

“Matumizi ya chai ya rangi katika kutibu macho yanaweza kusababisha vidonda kwenye kioo cha jicho na kusababisha kovu kwenye jicho litakalokufanya upate uoni hafifu au upoteze uwezo wa kuona kabisa,” amesema.

Dk Shilio amewataka wagonjwa pia kuepuka kutibu macho kwa mkojo, kwani ni hatari kwa usalama wa macho kwa kuwa mkojo hubeba uchafu na vijidudu vinavyoweza kusababisha maambukizi mengine na kupoteza uwezo wa kuona kabisa.

Amewataka kuzingatia kunawa mikono mara kwa mara na wapatapo ugonjwa huo kuwahi kituo cha afya kwa uchunguzi na matibabu sahihi na kwa wakati.

Via Mwananchi.

Soma Zaidi hapa Dawa ya Kutibu Ugonjwa wa macho mekundu(Red Eyes)

Mkojo,Chumvi, kitunguu saumu sio dawa ya kutibu ‘red eyes
0 Comment

Dawa ya red eyes,Ifahamu dawa ya macho mekundu hapaAfyaclass Forum •

Dawa ya red eyes,Ifahamu dawa ya macho mekundu hapa

Je unahitaji kutumia Dawa ya red eyes? na kama ni hivo ni ipi Dawa ya red eyes?

Ingawa ugonjwa wa red eyes huiisha au kuondoka wenyewe, kuna wakati unahitaji matibabu maalumu kutoka kwa wataalam wa afya ikiwa umekusababishia madhara Zaidi.

Hakikisha unaongea na wataalam wa afya Ili kupata Dawa ya red eyes haraka Zaidi ikiwa unapata hali hizi hapa;

– Unahisi maumivu makali sana kwenye Macho

– Uwezo wako wa kuona umeathiriwa na ugonjwa wa Red Eyes

– Macho yako yanaogopa mwanga

– Macho yanazidi kuwa mekundu siku hadi siku badala ya kupungua wekundu

– Unapatwa na Homa

– Macho kutoa Usaha badala ya tongotongo n.k

Dawa ya red eyes

Hizi hapa ni jamii ya Dawa ambazo huweza kutumika kutibu Ugonjwa wa Red Eyes Duniani, si dawa Zote utazipata hapa Tanzania,

Hivo ni muhimu kuwasaliana kwanza na wataalam wa afya au tuwasiliane hapa afyaclass ili kupata Dawa ya red eyes sahihi na inayopatikana hapa kwetu Tanzania.

Kumbuka; Matibabu ya ugonjwa wa red eyes huhusika na chanzo husika.

Dawa ya red eyes ni pamoja na;

✓ Naphazoline, ambayo hupatikana kwenye dawa jamii ya Clear Eyes Itchy Eye Relief.

Naphazoline ni dawa jamii ya decongestant ambayo hutibu macho mekundu(red eyes) ikiwa chanzo chake ni mzio au allergic reactions.

✓ Tetrahydrozoline, ambayo hupatikana mfumo wa matone kama vile Visine. Tetrahydrozoline ni dawa jamii ya decongestant kama vile naphazoline,

Hivo huondoa wekundu kwenye macho ambao hutokana na Mzio(allergy, exhaustion, and irritation).

✓ Eye lubricant drops. Pia zipo dawa za macho ambazo kazi yake kubwa ni kuwa kama vilainishi machoni, hizi pia huweza kutumika kama Dawa ya red eyes.

✓ Dawa ya red eyes, Haya ni matibabu mengine ya Ugonjwa wa red eyes;

Ikiwa umepata shida ya red eyes kwa sababu kama hizi allergies, conjunctivitis, au blepharitis, unaweza kufanya matibabu haya rahisi kwako;

SOMA ZAIDI HAPA: Kuhusu Dawa Za Ugonjwa wa macho

(1) Kutumia vitu vya baridi(Apply a cool compress). kuweka kitu cha baridi juu ya macho ukiwa umefunika macho yako huweza kusaidia kupunguza dalili za wekundu na kuvimba kwa macho.

(2) Tumia baadhi ya dawa(Take over-the-counter (OTC) medications).

Kama nilivyokwisha kueleza,dawa jamii ya antihistamines au decongestants huweza kutumika kama dawa ya Red eyes, ambapo husaidia kupunguza na kuondoa  dalili za wekundu wa macho.

Pia dawa kama vile ibuprofen pamoja na acetaminophen huweza kutumika kupunguza maumivu na Uvimbe.

(3) Epuka vitu vyote vinavyoweza kuingia machoni(Avoid irritants).

Hapa tunazungumzia vitu kama vile Vumbi, Moshi, pollens, chemical fumes n.k.

(4) Hakikisha unanawa mikono(Wash your hands).

Hakikisha unanawa mikono yako mara kwa mara kwa kutumia maji safi tiririka na Sabuni.

Epuka kabsa kugusa macho yako au eneo la karibu na macho yako hasa ukiwa hujanawa mikono yako.

(5) Epuka makeup au kuvaa miwani.

Epuka kutumia makeup au kuvaa miwani kam ikiwezekana mpaka dalili za ugonjwa wa red eyes ziondoke.

(6) Epuka kutazama vitu kama Simu,TV, au computer kwa muda mrefu.

Kutumia muda mwingi mbele ya kompyuta, TV au skrini ya simu kunaweza kusababisha macho kuwa na mkazo zaidi(eyestrain) na kuwa makavu, kwa hivyo jaribu kupunguza muda wako wa kutumia kifaa kama hivi.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Ugonjwa wa Macho Mekundu(RED EYES),chanzo,dalili na Matibabu

Dawa ya red eyes,Ifahamu dawa ya macho mekundu hapa
0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Forum Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Forum ASANTE.
UNDERSTOOD