Showing posts with label Events. Show all posts
Showing posts with label Events. Show all posts

Wapandikizwa Ini baada ya kula Uyoga wenye sumuAfyaclass Forum •

Wapandikizwa Ini baada ya kula Uyoga wenye sumu

Mwanamume mmoja nchini Ujerumani na watoto wawili wamelazimika kupandikizwa ini katika Hospitali ya Chuo Kikuu katika mji wa magharibi mwa Ujerumani wa Essen, baada ya kula uyoga wenye sumu.

Mgonjwa wa nne, ambaye ni mvulana mdogo wa miaka mitano, alipata nafuu bila kupandikizwa ini, imesema hospitali hiyo. Wote wanne, mmoja wao akiwa ni baba wa mmoja wa watoto hao, wamekuwa katika uangalizi wa wagonjwa mahututi katika hospitali hiyo tangu siku ya Jumanne.

"Hali za wagonjwa wote zinaendelea vizuri na wanafuatiliwa kwa karibu na kwa umakini," ilisema taarifa iliyotolewa na hospitali hiyo.

Wagonjwa hao walilazwa hospitalini wakiwa na hali mbaya. Wawili walifanyiwa upasuaji wa kupandikiza ini muda mfupi baada ya kufikishwa hospitali na mtoto mmoja alifanyiwa baadaye.

Uyoga huo aina ya Amanita huliwa, lakini pia una vimelea vya sumu.

Katika kisa tofauti huko mjini Münster, mgonjwa mmoja mwanamke ameendelea kupatiwa matibabu ya kina baada ya kula uyoga wenye sumu wiki iliyopita. Inaaminika kuwa mgonjwa huyo alikula uyoga wa aina hiyo ya Amanita.

Msemaji katika hospitali anakotibiwa mgonjwa huyo alisema siku ya Jumatatu kwamba mgonjwa huyo bado ana hali mbaya na anapatiwa huduma ya wagonjwa mahututi. Aidha pia bado wanatafuta mtu anayeweza kuchangia ini ili waweze kumfanyia upandikizaji.

Bado haijafahamika ikiwa wagonjwa hao walichuma uyoga mwituni au walikula ni wapi walipoula uyoga huo.

0 Comment

Fahamu kuhusu Siku ya Kitaifa ya kutafuta Ujauzito,Siku ya MimbaAfyaclass Forum •

Fahamu kuhusu Siku ya Kitaifa ya kutafuta Ujauzito,Siku ya Mimba

Wafanyakazi wa Urusi walipewa likizo ya kufanya ngono leo ili kuongeza kiwango cha kuzaliwa, siku hii ilitangazwa kuwa Siku ya Mimba huko Ulyanovsk, ambapo wanandoa waliambiwa waende nyumbani ili kupata muda wa kuongeza uzao.

Ili kufanikisha jambo hili, walitangaziwa zawadi ya kushinda gari, pesa taslimu au friji, chini ya mpango wa baraza la jiji la “Zaa kwa Patriot”, kwa wale ambao wangejifungua Juni 12, ambayo ndiyo siku maalum kwa Urusi kwa tukio hilo na wengineo pia wangepata tuzo.

Wanandoa walioshinda zawadi kuu (gari la 4×4), lililotengenezwa ndani ya nchi hiyo, watapitishwa kwa vigezo vya Kamati ya kama vile “heshima” na “malezi ya kupongeza” mpango ambao ulisimamiwa na Gavana wa Ulyanovsk, Sergei Morozov.

Septemba 12, 2006 ndipo Rais wa Urusi alihutubia taifa hilo na kutangaza janga la idadi ndogo ya watu kuwa ni tatizo la dharura na akatangaza jitihada za kuongeza kiwango cha idadi ya watu na kuongeza uzazi nchini Urusi.

Alisema Serikali ingetoa motisha ya pesa taslimu kwa familia ambazo zina zaidi ya mtoto mmoja, ili zihamasike kuongeza watoto, ndipo siku hiyo ya Septemba 12 kila mwaka ikawa ni siku muhimu ambayo ilipewa heshima kama ‘siku ya kupeana ujauzito kwa raia wa Urusi.

Badaye Serikali ikaanzisha siku ya mapumziko kwa umma, ikiwa ni maalumu kwa ajili ya kuwapa wanandoa muda wa faragha kwa matumaini kwamba watashika mimba na Wazazi ambao watoto wao huzaliwa miezi tisa baadaye wakapewa fursa ya kushinda zawadi hizo na Watoto wanaozaliwa Septemba 12 hupata zawadi kutoka kwa Mamlaka.

Tangu mpango huo uanze, kiwango cha kuzaliwa katika eneo hilo kiliongezeka, ikikumbukwa kwamba kupungua kwa viwango vya kuzaliana, kuongezeka kwa wahamiaji na watu kwenda nchi zingine, mfumo dhaifu wa huduma ya afya na mambo mengine yalichangia tangu kuanguka kwa Soviet mnamo 1991.

0 Comment

Mbio za kuleta faraja kwa watoto waliozaliwa na tatizo la afya ya akili (Usonji)Afyaclass Forum •

Mbio za kuleta faraja kwa watoto waliozaliwa na tatizo la afya ya akili (Usonji)

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa leo Septemba 07, 2024 ameshiriki matembezi ya hisani ya 𝐌𝐚𝐞𝐧𝐝𝐞𝐥𝐞𝐨 𝐁𝐚𝐧𝐤 𝐌𝐚𝐫𝐚𝐭𝐡𝐨𝐧 ‘Hatua ya Faraja’ Msimu wa Pili Jijini Dar es Salaam

Mhe. Majaliwa ameongoza mbio hizo za kuleta faraja kwa watoto Lengo likiwa ni kukusanya zaidi ya milioni 200 kwa ajili ya Kuchangia ukarabati wa Kituo cha watoto waliozaliwa na tatizo la afya ya akili (Usonji) wa kituo cha Mtoni Diakonia na pia kwa ajili ya kununua mashine maalum za kuwahifadhi watoto wanaozaliwa kabla ya wakati yaani watoto njiti, katika Hospitali ya rufaa ya KCMC.

Katika mbio hizo Waziri mkuu ameambatana na Naibu waziri wa afya Dkt. Godwin Mollel pamoja na viongozi wengine wa serikali ikiwa ni kuunga mkono juhudi za kuendelea kuboresha sekta ya afya katika kutoa huduma bora kwa wananchi.



0 Comment

TUKIO:Raia wa China ajifungua mapacha watatu DarAfyaclass Forum •

TUKIO:Raia wa China ajifungua mapacha watatu Dar

RAIA wa China, Liya Zhang (31), ambaye amejifungua watoto mapacha watatu wa kiume katika hospitali ya Regency ya jijini Dar es Salaam ameshukuru kwa huduma nzuri alizopata.

Raia huyo alijifungua watoto hao siku ya Jumapili usiku hospitalini hapo na mpaka sasa anaendelea vizuri yeye na watoto wake hao watatu.

Akizungumza hospitalini hapo, Liya alisema awali wakati anahudhuria kliniki alidhani kuwa ana ujauzito wa mtoto mmoja lakini baada ya vipimo alishtuka kuambiwa kuwa  ana watoto wa tatu.

“Nawashukuru sana madaktari bingwa wa watoto, Dk. Rahim na Dk. Supriya Khan kwa namna walivyonihudumia tangu awali mpaka najifungua, nimepata huduma nzuri sana hapa Regency na watoto wangu kama unavyowaona wako vizuri kabisa,” alisema Liya kwa lugha ya Kiswahili fasaha.

Liya alisema si mara yake ya kwanza kujifungua hospitalini hapo kwani mwaka 2009 alijifungua mtoto wa kwanza wa kike hospitalini hapo na baadaye alikuja kujifungua mengine wawili wa kiume pia hospitaini hapo hapo na sasa amefurahi kupata watoto wa kiume watatu.

“Nilipata mtoto mmoja wa kike mwaka 2009 na baadaye nikapata  mapacha wawili wa kiume na juzi Jumapili nimepata mapacha watatu kwa hiyo sasa nina jumla ya watoto sita na wote nimejifungua katika hospitali hii hii ya Regency na nadhani nitakuwa nimemaliza kwa kweli inatosha,” alisema Liya huku akicheka kwa nguvu.

Daktari bingwa wa watoto wa Regency, Dk. Rahim alisema wamekuwa wakimhudumia Liya tangu uzao wake wa kwanza ambapo alipata mtoto wakike hospitalini hapo na ujauzito wa pili ambapo alifanikiwa kupata watoto wa kiume mapacha.

“Na huu ni ujauzito wake wa mara ya tatu ambapo amefanikiwa kupata mapacha watatu wote wa kiume na uziri ni kwamba anaimani nasisi kwa muda mrefu kwani kila anapotaka kujifungua amekuwa akija hapa Regency na tunashukuru watoto wake wote wanaendelea vizuri sana,” alisema

“Tumekuwa tukihudumia wanawake wengi sana wanaojifungua lakini hii ni mara ya kwanza hapa Regency kuhudumia mwanamke kupata watoto watatu, hii ni habari njema kwetu sote,” alisema

TUKIO:Raia wa China ajifungua mapacha watatu Dar
0 Comment

Madaktari wa Anambra wasimamisha mgomo kufuatia kuachiliwa kwa mwenzao aliyetekwa nyaraAfyaclass Forum •

Madaktari wa Anambra wasimamisha mgomo kufuatia kuachiliwa kwa mwenzao aliyetekwa nyara

Chama cha Madaktari cha Nigeria (NMA), Tawi la Anambra, kimesitisha mgomo ulioanzishwa kupinga kutekwa nyara kwa Dk Stephen Ezeh katika jimbo hilo.

Katika taarifa ya Jumapili,  Agosti 25, NMA, ilisema uamuzi wa kusitisha mgomo ulifuatia kuachiliwa kwa Ezeh kutoka utumwani Jumamosi, Agosti 24.

Taarifa hiyo ilitiwa saini na Dkt Princeston Okam na Dkt Ifeanyi Obiaeli, Mwenyekiti na Katibu wake.

Taarifa hiyo ilisema: “Mgomo wa jumla na usiojulikana ulioitishwa na NMA Tawi la Anambra kupinga kutekwa nyara kwa mwanachama wetu, Dk Stephen Ezeh, umesitishwa kufuatia kuachiliwa kwake. Huduma za kliniki zitaanza saa 08:00 Jumapili, Agosti 25.

“Tunawashukuru watu wema wa Anambra kwa kuvumilia pamoja nasi katika nyakati hizi za majaribu huku tukiomba kwa dhati kwamba dhiki hii isitokee tena.

“Tunawashukuru wenzetu kwa mshikamano wao na ushupavu wao katika kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekta hii, hasa ukosefu wa usalama na tunawaomba waendelee kuwa na uthubutu na kujitolea katika kufikisha huduma za afya kwa watu wa Anambra.”

Madaktari wa Anambra wasimamisha mgomo kufuatia kuachiliwa kwa mwenzao
aliyetekwa nyara
0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD