Showing posts with label Rais Samia Suluhu Hassan. Show all posts
Showing posts with label Rais Samia Suluhu Hassan. Show all posts

Rais Samia Suluhu Hassan afanya uteuzi na mabadiliko ya Viongozi mbali mbaliAfyaclass Forum •

Rais Samia Suluhu Hassan afanya uteuzi na mabadiliko ya Viongozi mbali mbali

Leo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi  kwenye nafasi mbali mbali Serikalini,

Moja ya Uteuzi uliofanyika ni wa Angela Charles Kizigha ambaye ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais, Masuala ya Jamii,

Pia Rais Samia suluhu amemteua Mobhare Holmes Matinyi kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika nchi ya Algeria. Mabadiliko hayo yamefanyika ndani ya Muda huu....

0 Comment

RAIS Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kufuatia ajali iliyotokea SameAfyaclass Forum •

 DAR ES SALAAM;RAIS Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kufuatia ajali iliyotokea jana Same mkoani Kilimanjaro, huku akiwataka madereva waendelee kuzingatia kwa umakini mkubwa sheria za usalama barabarani.

"Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya vifo vya ndugu zetu 37 na majeruhi 30 kutokana na ajali ya barabarani iliyotokea jana jioni eneo la Sabasaba, Barabara Kuu ya Moshi - Tanga, Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, kwa magari mawili kugongana na kuungua moto.

"Ninawaombea kwa Mwenyezi Mungu marehemu wote wapumzike kwa amani, na majeruhi wote wapone kwa haraka. Ninatoa salamu za pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mheshimiwa Nurdin Babu, familia zote za wafiwa, ndugu, jamaa na marafiki. Mwenyezi Mungu awape faraja na nguvu katika kipindi hiki kigumu.

“Kama ambavyo nilieleza Juni 27 katika hotuba yangu ya kuhitimisha shughuli za Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ajali za barabarani zimeendelea kugharimu maisha ya wapendwa wetu. Ninawasisitiza madereva kuendelea kuzingatia kwa umakini mkubwa sheria za usalama barabarani, na Jeshi la Polisi kuendelea kusimamia kikamilifu sheria hizo," ameandika Rais Samia kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii.

0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Forum Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Forum ASANTE.
UNDERSTOOD