Trump Aeleza Uzito na Hatari ya Kazi ya Urais Baada ya Tukio la Usalama
Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema kuwa angejua mapema uzito na hatari ya kazi ya urais, huenda asingegombea nafasi hiyo.
Kauli hiyo ameitoa kufuatia tukio la kiusalama lililotokea wakati wa hafla ya White House Correspondents’ Dinner, ambapo milio ya risasi ilisikika na kusababisha taharuki miongoni mwa wageni waliohudhuria.
Trump alimrejelea Marco Rubio akisema kama angepewa picha halisi ya changamoto za kazi hiyo mapema, huenda angefanya uamuzi tofauti kuhusu kugombea urais.
Katika maelezo yake kwa waandishi wa habari, Trump alisema kazi ya urais ni yenye changamoto kubwa na hatari, lakini ameendelea kusisitiza kuwa anajivunia kulitumikia taifa lake na yupo tayari kutekeleza wajibu wake.
Baada ya tukio hilo, maafisa wa usalama walichukua hatua za haraka kwa kuwaondoa Trump pamoja na viongozi wengine waliokuwepo ukumbini, huku wakihakikisha eneo hilo linawekwa salama.
Kwa mujibu wa taarifa za polisi, mshukiwa ametambulika kama Cole Tomas Allen, mwenye umri wa miaka 31 kutoka California. Inadaiwa alikamatwa na kupelekwa hospitali kwa uchunguzi zaidi, wakati maafisa wa FBI wakiendelea na uchunguzi wa tukio hilo. Afisa mmoja wa usalama anaripotiwa kujeruhiwa lakini anaendelea kupatiwa matibabu.



.jpeg)
