Showing posts with label Saratani ya Ovari. Show all posts
Showing posts with label Saratani ya Ovari. Show all posts

Babyjohnson:Fidia poda zenye kemikali ya talc zilizosababisha saratani ya ovariAfyaclass Forum •

Fidia poda zenye kemikali ya talc zilizosababisha saratani ya ovari.

Johnson & Johnson imesema watalipa dola bilioni 6.5 ili kumaliza maelfu ya kesi nchini Marekani zinazodai kuwa poda zenye kemikali ya talc zilisababisha saratani ya ovari.

Mpango huo utasaidia J&J kusuluhisha kesi hizo kupitia kesi tatu za kampuni tanzu ya LTL Management.

Kutakuwa na kipindi cha miezi mitatu cha kupiga kura kwa wadai, kwa matumaini ya kufikia makubaliano juu ya madai yote ya sasa na yatakayokuja dhidi ya saratani ya ovari.

Takriban asilimia 99% ya kesi zinazohusiana na talc zilizowasilishwa dhidi ya J&J na kampuni tanzu zinatokana na saratani ya ovari.

Babyjohnson:Fidia poda zenye kemikali ya talc zilizosababisha saratani
ya ovari
0 Comment

Dalili za Saratani ya Ovari, fahamu kuhusu Saratani ya OvariAfyaclass Forum •

Fahamu kuhusu Saratani ya Ovari(ovarian cancer)

Saratani ya Ovari, hii ni Saratani ambayo hutokea kwenye vifuko vya mayai(Ovaries),

Saratani hii huhusisha tatizo la seli hai zilizopo eneo la vifuko vya mayai kukuwa na kuongezeka kuliko kawaida.

Dalili za Saratani ya Ovari

Dalili za Saratani ya Ovari ni pamoja na;

– Mgonjwa kuhisi haja ya kukojoa kila mara

– Mgonjwa kushiba haraka sana wakati wa kula

– Mgonjwa Kuhisi tumbo kujaa sana

– Kubadilika kwa mzunguko wako wa hedhi

– Kublid mara mbili ndani ya mwezi mmoja

– Uzito wa mwili kupungua kwa kiasi kikubwa

– Mgonjwa kupata shida ya choo kigumu

– Wakati mwingine kupata maumivu ya tumbo chini ya kitovu

Kundi ambalo lipo kwenye hatari ya kupata Saratani ya Ovari

WATU AMBAO WAPO KWENYE HATARI YA KUPATA KANSA YA VIFUKO VYA MAYAI NI PAMOJA NA;

• Watu ambao kuna mgonjwa wa tatizo hili katika familia yao

• Watu ambao huanza kuona siku zao za hedhi wakiwa na umri mdogo sana

• Watu ambao huwahi kukoma hedhi yao ya mwezi yaani Menopause

• Wanaotumia vidonge vya uzazi wa mpango hovio

MATIBABU YA Saratani ya Ovari au Saratani ya VIFUKO VYA MAYAI

– Yapo matibabu mbali mbali ya aina hii ya kansa kama vile;

  • Njia ya upasuaji na kuondoa ovary moja au zote mbili kama zimeathirika na kansa hii,
  • Huduma ya Chemotherapy
  • pamoja na matibabu mengine ambayo huhusu zaidi kudhibiti dalili za ugonjwa huu wa kansa ya vifuko vya mayai

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dalili za Saratani ya Ovari, fahamu kuhusu Saratani ya Ovari
0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD