Showing posts with label Ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo. Show all posts
Showing posts with label Ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo. Show all posts

Nigeria yaleta chanjo mpya ya 5-in-1 dhidi ya homa ya uti wa mgongo,meningitisAfyaclass Forum •

Nigeria yaleta chanjo mpya ya 5-in-1 dhidi ya homa ya uti wa mgongo,meningitis.

Wahudumu wa afya wazindua kampeni ya chanjo inayolenga kuwafikia watu milioni moja

Katika hatua ya kihistoria, Nigeria imekuwa nchi ya kwanza duniani kutoa chanjo mpya (inayoitwa Men5CV) iliyopendekezwa na Shirika la Afya Duniani (WHO), ambayo inawalinda watu dhidi ya aina tano za bakteria wa meningococcus.

Shughuli za chanjo ya dharura zinafadhiliwa na Gavi, Muungano wa Vaccine, ambao unafadhili hifadhi ya chanjo ya uti wa mgongo duniani kote, na kusaidia nchi za kipato cha chini kwa chanjo ya kawaida dhidi ya homa ya uti wa mgongo.

Nigeria ni mojawapo ya nchi 26 zenye homa ya uti wa mgongo barani Afrika, iliyoko katika eneo linalojulikana kama Ukanda wa homa ya Uti wa mgongo barani Afrika. Mwaka jana, kulikuwa na Zaidi ya asilimia 50% ya visa vya kila mwaka vya homa ya uti wa mgongo iliyoripotiwa kote barani Afrika.

Nchini Nigeria, mlipuko wa serogroup C wa Neisseria meningitidis (meningococcus) ulisababisha visa 1742 vinavyoshukiwa kuwa homa ya uti wa mgongo, ikijumuisha visa 101 vilivyothibitishwa na vifo 153 katika majimbo saba kati ya 36 ya Nigeria (Adamawa, Bauchi, Gombe, Jigawa, Katsina, Yobe, Zamfara) 1 Oktoba 2023 na 11 Machi 2024.

Ili kuzima mlipuko huo hatari, kampeni ya chanjo imefanywa tarehe 25–28 Machi 2024 ili kufikia zaidi ya watu milioni moja wenye umri wa miaka 1-29.

Homa ya uti wa mgongo ni maambukizi makubwa ambayo husababisha kuvimba kwa utando (meninjis) unaozunguka na kulinda ubongo na uti wa mgongo. Kuna sababu nyingi za ugonjwa wa meningitis, ikiwa ni pamoja na virusi, bakteria, pamoja na vimelea vingine. Dalili mara nyingi ni pamoja na maumivu ya kichwa, homa na shingo kuwa ngumu au kukaza.

Homa ya Uti wa mgongo inayotokana na bakteria ndio mbaya zaidi, Inaweza pia kusababisha tatizo la septicemia na unaweza kulemaza au kuua ndani ya masaa 24 kwa wale wanaougua.

#SOMA ZAIDI HAPA kuhusu Ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo,meningitis.

Nigeria yaleta chanjo mpya ya 5-in-1 dhidi ya homa ya uti wa
mgongo,meningitis
0 Comment

Ugonjwa wa uti wa mgongoAfyaclass Forum •

Ugonjwa wa uti wa mgongo

Utangulizi kuhusu Ugonjwa wa uti wa mgongo, Soma Hapa;

Fahamu,Ugonjwa wa uti wa mgongo hutokea iwapo utando unaofunika ubongo na uti wa mgongo utapatwa na maambukizi.

Ugonjwa wa Uti wa mgongo husababishwa na nini?

Ugonjwa huu husababishwa na vimelea mbalimbali vya makundi ya bakteria, virus na hata fungus. Tukivigawanya visababishi hivi katika makundi haya, tutaona kuwa bakteria wanaosababisha ugonjwa wa uti wa mgongo ni kama vile; bakteria wajulikanao kama Beta-streptococci, Hemophilus influenza, Escherichia coli, Listeria monocytogenes, Neisseria meningitides, Streptococci pneumoniae pamoja na Mycobacteria tuberculosis, ambao pia ni maarufu kwa kusababisha ugonjwa wa kifua kikuu.

Aidha kutoka kundi la virus, virus wanaojulikana kwa kusababisha ugonjwa huu wa uti wa mgongo ni pamoja na Herpes simplex type 2, HIV pamoja na Varicella zoster.

Vimelea vya fungus ambavyo hujulikana kwa kusababisha ugonjwa wa uti wa mgongo ni pamoja na wale wajulikanao kama Coccoidiodomycosis pamoja na Cryptococci meningetides.

Chanzo cha Ugonjwa wa Homa ya uti wa mgongo(Meningitis)

Homa ya uti wa mgongo  kwa kitaalam hujulikana kama meningitis, ni tatizo ambalo huhusisha maambukizi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa kwenye sehemu kuu mbili ubongo pamoja na Uti wa mgongo.

Homa ya uti wa mgongo hutokea iwapo utando unaofunika ubongo na uti wa mgongo utapatwa na maambukizi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa,soma hapa chini kujua visababishi vya tatizo la homa ya uti wa mgongo.

VISABABISHI VYA UGONJWA WA HOMA YA UTI WA MGONGO NI PAMOJA NA;

1. Maambukizi ya Bakteria mbali mbali kama vile; Beta-streptococci, Hemophilus influenza, Escherichia coli, Listeria monocytogenes, Neisseria meningitides, Streptococci pneumoniae na Mycobacteria tuberculosis

2. Maambukizi ya Virus mbali mbali kama vile; Herpes simplex type 2, HIV na Varicella zoster.

3. Maambukizi ya Fangasi mbali mbali kama vile; Coccoidiodomycosis na Cryptococci meningetides.N.k

DALILI NA VIASHIRIA VYA TATIZO LA HOMA YA UTI WA MGONGO NI PAMOJA NA;

1•Shingo kukakamaa na kuwa ngumu isivyo kawaida

2•Mgonjwa kujihisi homa kali au joto la mwili kuwa juu sana

3•Mgonjwa kupata Maumivu makali sana ya kichwa

4•Mgonjwa kupoteza fahamu au uwezo wa kukumbuka vitu

5•Mgonjwa kupatwa na degedege (seizures) na mwili kukakamaa

6•Mgonjwa kushindwa kuvumilia mwanga (photophobia)

7•Mgonjwa kutoweza kukaa sehemu yenye makelele (phonophobia)

8•Kwa watoto, kuvimba utosi n.k

MADHARA YA TATIZO HILI LA HOMA YA UTI WA MGONGO NI PAMOJA NA;

1•Kuamshwa kwa chembechembe za damu zinazo sababisha damu kuganda kitaalamu hujulikana kama – Disseminated Intravascular Coagulopathy (DIC).

2•Kuvuja damu katika tezi za adrenalin na kupelekea kutokea kwa ugonjwa ambao kitaalamu unaitwa – waterhouse friderichsen syndrome.

3•Kwa watoto, ugonjwa huu unaweza kusababisha mtoto kuwa na kichwa kikubwa – hydrocephalus pamoja na madhara mengine.

MATIBABU YA UGONJWA WA HOMA YA UTI WA MGONGO

Kwa wagonjwa waliopoteza fahamu ni vizuri kuhakikisha wanapumua vizuri, na njia za hewa ziko wazi. Halikadhalika, iwapo itathibitika kuwa bakteria ndiyo wanaosababisha ugonjwa huu, mgonjwa anaweza kupewa mojawapo ya dawa hizi za antibiotiki kama cefotaxime au Cefriaxone. Aidha baadhi ya madaktari hupendelea kuongeza dawa za steroids kama dexamethasone kama sehemu ya matibabu.

Iwapo itathibitika ugonjwa huu umesababishwa na virus, dawa kama Acyclovir huweza kutumika. Hali kadhalika, ikithibitika kuwa vimelea waliosababisha ugonjwa huu ni wa kundi la fungus, dawa kama Amphotericin B au flucytosine zaweza kutumika. Mgonjwa pia hupewa Paracetamol kwa ajili ya kushusha homa na kuondoa maumivu ya kichwa.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Ugonjwa wa uti wa mgongo
0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD