Showing posts with label afya ya uzazi. Show all posts
Showing posts with label afya ya uzazi. Show all posts

Mambo 5 yanayopunguza Ubora wa Mbegu za KiumeAfyaclass Forum •

Mambo 5 yanayopunguza Ubora wa Mbegu za Kiume

Katika Makala hii tumechambua baadhi ya Mambo makubwa ambayo huweza kuathiri ubora wa Mbegu za Kiume(Sperm quality),Soma Makala hii Mpaka mwisho kufahamu.

MAMBO 5 YANAYOPUNGUZA UBORA WA MBEGU ZA KIUME

Ubora wa mbegu za kiume ni muhimu kwa afya ya uzazi. Hata hivyo, mtindo wa maisha na mazingira yanaweza kuathiri uzalishaji na ubora wake. 

Hapa ni mambo 5 yanayoweza kupunguza ubora wa mbegu za kiume:

1. Msongo wa Mawazo (Stress)

Msongo wa mawazo huathiri uzalishaji wa homoni muhimu kwa uzazi, kama vile homoni ya testosterone, na kusababisha kupungua kwa idadi na kasi ya mbegu za kiume.

2. Lishe Duni

Upungufu wa virutubisho kama vile zinki, vitamini C, na antioxidants unaweza kupunguza uzalishaji wa mbegu zenye afya. Epuka vyakula vyenye mafuta mengi na sukari kupita kiasi.

3. Uvutaji wa Sigara na Matumizi ya Pombe Kupita Kiasi

Nikotini na kemikali nyingine kwenye sigara huathiri moja kwa moja uzalishaji wa mbegu za kiume. Pombe pia hupunguza viwango vya testosterone, hivyo huweza kuathiri uzazi.

4. Joto Kali Sehemu za Siri

Kuvaa nguo za kubana, matumizi ya laptop kwenye mapaja, au kukaa muda mrefu kwenye viti vyenye joto (kama vile kwenye gari) huongeza joto kwenye korodani na kupunguza uzalishaji wa mbegu.

5. Kutopata Usingizi wa Kutosha

Usingizi duni huathiri usawa wa homoni mwilini, na hivyo kupunguza uzalishaji wa mbegu za kiume. Hakikisha unapata saa 7-8 za usingizi bora kila usiku.

♻️ Badilisha mtindo wa maisha ili kuboresha afya ya uzazi!

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

#AfyaYaUzazi #MbeguZaKiume #AfyaBora

0 Comment

Maumivu Ya Chini Ya Kitovu,Mgongo Na Matiti Baada Ya Kujifungua/KuzaaAfyaclass Forum •

MAUMIVU YA CHINI YA KITOVU,MGONGO NA MATITI BAADA YA KUJIFUNGUA/KUZAA

Maumivu ya tumbo hasa chini ya kitovu,
mgongo na matiti mara baada ya
kujifungua/kuzaa na ambayo huongezeka
wakati wa kunyonyesha kitaalamu yanaitwa "afterpains"

Mara kadhaa watu wamekuwa wakiamini kuwa maumivu yanayoambatana na zoezi zima la kujifungua hupotea mara baada ya kujifungua. Kitu ambacho inawezekana si sahihi kwa wote.

Nyakati za awali mara baada ya kujifungua inaaminika kunakuwa na mabafiliko katika baadhi ya maeneo ya ubongo ambayo kwa namna moja ama nyingine hupelekea fikira na mitazamo ambayo hupelekea kuhisi maumivu makali isivyo kawaida.

Kuzaa kwa upasuaji au kuzaa kwa njia ya kawaida lakini kwa kusaidiwa na vifaa kunaambatana na maumivu makali baada ya kujifungua ukilinganisha na unapozaa kawaida. Kwa kawaida maumivu haya hutegemea hisia, mawazo na mtazamo.

Maumivu ya tumbo hutokea ikiwa ni matokeo ya mji wa mimba kunywea au kupungua kwa mji wa mimba katika hatua ya kurudi katika umbo la awali kabla ya kubeba ujauzito.

Namba ya nzao inahusishwa na kiwango cha maumivu haya. Katika mimba ya kwanza maumivu haya huweza kuwa sio makali sana n uweza kuisha ndani ya muda mfupi, lakini baada ya mimba mbili na kuendelea inaaminika maumivu huongezeka kutokana ukweli kuwa misuli ya mji wa mimba inakuwa imepunguza nguvu ya mvutano hivyo hupitia katika kipindi cha kunywea na kujilegeza hivyo kupelekea maumivu kuwa endelevu kwa muda.

Mimba zenye mapacha, watoto wakubwa, kiwango kikubwa cha maji katika mfuko wa mtoto, maambukizi nk zinaaminika kuambatana na maumivu haya mara baada ya kujifungua.

Kunyonyesha huweza kuleta au kuongeza kiwango cha maumivu kwasababu kitendo cha kunyonyesha hupelekea kutolewa kwa homoni ya oxytocin ambayo huchochea kunywea kwa mji wa mimba na hivyo maumivu.

Maumivu haya huweza kuwa chini ya kitovu, mgongoni au kwenye matiti.

Asilimia 64 ya kinamama hufananisha maumivu haya na maumivu ya hedhi. Baadhi hufananisha na maumivu au hisia mtoto akicheza awapo tumboni, wengine hufananisha na maumivu ya njaa na wengine huyafananisha na kitu kigumu kinachotembea kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

NAMNA YA KUZIA AU KUPUNGUZA
kukojoa mara kwa mara, kulalia tumbo (kulala kifudi fudi) AU kujikanda na maji ya vuguvugu inaweza kusaidia.

Matumizi ya dawa , za kutuliza maumivu, hupelekea kukata au kutulia kwa maumivu haya

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Ni mara ngapi unaweza kuhitaji kubadilisha pedi yako kila siku?Afyaclass Forum •

 Ni mara ngapi unaweza kuhitaji kubadilisha pedi yako kila siku?

Kukaa na Pedi kwa Muda Mrefu huweza kuongeza hatari ya Mwanamke kupata magonjwa mbali mbali ikiwemo Fangasi.

Ni mara ngapi unaweza kuhitaji kubadilisha pedi yako kila siku?

Hii inaweza kutegemea kiwango chako cha Hedhi unachopata, jinsi mtiririko wako ulivyo mzito, na aina ya pedi unayotumia. Lakini unapaswa kuibadilisha kabla haijajaa.

Kwa Mujibu wa "The American College of Obstetricians and Gynecologists (ACOG)" wanapendekeza ubadilishe pedi yako angalau kila baada ya saa 4 hadi 8, lakini hayo ni masaa ya jumla tu.

Ni mara ngapi unabadilisha pedi yako inategemea na sababu mbali mbali ikiwemo; mtiririko wako, aina ya pedi unayotumia n.k.

0 Comment

AFYA YA UZAZI KWA WANAUMEAfyaclass Forum •

 AFYA YA UZAZI KWA WANAUME

Hapa tunazungumzia mfumo mzima wa uzazi ikiwemo,

via vya uzazi vya Mwanaume pamoja na mbegu za kiume.

Uwezo wa kufanya tendo la ndoa vizuri bila shida yoyote,

Pamoja na uzalishaji wa mbegu za kiume zenye ubora na kiwango kinachotakiwa.

ZINGATIA HAYA KWENYE AFYA YA UZAZI KWA MWANAUME

• Hakikisha unakula mlo kamili na kuepuka kula vyakula vyenye virutubisho vya aina moja kwa kiwango kikubwa

kama vile kula wanga mwingi,mafuta mengi n.k

• Epuka matumizi ya Pombe kama unataka kuboresha afya ya uzazi

• Epuka matumizi ya Sigara pamoja na dawa zingine za kulevyia

• Epuka matumizi ya dawa hovio pasipo maelekezo kutokwa kwa wataalam wa afya

• Zingatia matumizi ya maji ya kutosha kila siku,angalau lita 2.5 mpaka 3

• Fanya mazoezi mbalimbali ya mwili

• Epuka kuwa na uzito mkubwa au unene obesity/overweght

• Jilinge au jikinge na magonjwa yote ya zinaa, na pata tiba mara moja kama una ugonjwa wowote ambao unashambulia sehemu zako za siri.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584



0 Comment

IDADI YA MAYAI KWA MWANAMKE(Toka kuzaliwa kwake hadi ukomo wa Hedhi)Afyaclass Forum •

 IDADI YA MAYAI KWA MWANAMKE(Toka kuzaliwa kwake hadi ukomo wa Hedhi)

Je Mwanamke ana Idadi ya Mayai Mangapi toka anazaliwa mpaka ukomo wake wa hedhi yaani Menopause?

IDADI YA MAYAI KWA MWANAMKE(Toka kuzaliwa kwake hadi ukomo wa Hedhi)

Kutokana na "American College of Obstetricians and Gynaecologists (ACOG), Mtoto jinsia ya kike akiwa tumboni kwa mama yake(female fetus) Ujauzito ukiwa na wiki 20 yaani 20 Weeks Gestation age anakuwa na mayai takribani Million 6-7,

Na mayai hayo huanza Kupungua mpaka kufikia Milioni 1-2 wakati anazaliwa,

Hivo basi kutokana na ACOG Mwanamke anazaliwa akiwa na Idadi ya Mayai takribani Millioni 1-2.

Na hyo ndyo Idadi kubwa ya Mayai ambayo mpaka anafariki hataifikia tena, kwani baada ya hapo mayai yataendelea kupungua siku hadi siku toka siku ya kwanza anazaliwa.

SWALI; JE KWANINI HEDHI ISIANZE TOKA SIKU YA KWANZA MTOTO WA KIKE ANAZALIWA?

- Licha ya kwamba Mwanamke anakuwa na Mayai mengi sana(Millions of eggs) kwenye vifuko vya mayai(Ovaries),Mayai hayo yanakuwa hayajakomaa mpaka kufikia kipindi cha Balehe Yaani Puberty.

Na kwa hali ya kawaida mayai ambayo hayajakomaa hayawezi kutoka kwenye Ovaries(hivo hakuna ovulation) na kama hakuna Ovulation, hata hedhi pia haitakuwepo.

Na kipindi cha balehe huanza wakati eneo la Ubongo ambalo hujulikana kama hypothalamus kufanya kazi kubwa ya uzalishaji wa vichocheo au hormones ambayo hujulikana kama gonadotropin-releasing hormone (GnRH).

Na kwa Idadi kubwa ya Wanawake kipindi cha balehe huweza kuanza kati ya miaka 12-13 japo kuna baadhi huwahi zaidi kama miaka 8 n.k na wengine huweza kuchelewa zaidi.

Na mpaka Mwanamke kufikia kipindi cha balehe(puberty), anakuwa na Idadi ya Mayai takribani 300,000–500,000, na mayai hayo huendelea kupungua kwa kasi kila mwezi.

Mbali na mayai ambayo hupungua au kutoka kipindi cha hedhi, pia kuna sababu zingine nyingi ambazo husababisha mayai kupungua sana.

IDADI YA MAYAI KWA MWANAMKE AKIWA NA MIAKA YA 30(30s)

Mwanamke anakuwa na uwezo mkubwa sana wa kubeba mimba(high fertility) kuanzia miaka ya 20 hapo, ambapo anakuwa na asilimia 25-30% za kubeba mimba kwa kila Mwezi.

Kutokana na ACOG, wanasema uwezo wa mwanamke kubeba Mimba hupungua sana kuanzia kwenye Miaka ya 32 ambapo atakuwa na wastani wa mayai 120,000, huku uwezo wa kubeba mimba ukiwa ni wastani wa asilimia 20% kwa kila mzunguko.

Na Mayai yataendelea kupungua sana na kwa kiasi kikubwa Mwanamke akifikia umri wa Miaka 37 ambapo atakuwa na wastani wa mayai 25,000.

Kutokana na Centers for Disease Control and Prevention (CDC) wanasema, Couples Moja(1) kati ya tano(5) ambapo Mwanamke ana umri wa Miaka 30-39 Wanapata changamoto ya kupata mtoto.

UWEZO WA KUBEBA MIMBA KWA MWANAMKE MWENYE UMRI WA KUANZIA MIAKA YA 40(40S)

Kwa mwanamke mwenye umri wa Miaka 40, uwezo wa kubeba Mimba hushuka mpaka asilimia 5%, Ingawa pia kuna wanawake wengi hubeba mimba kwenye miaka hii ya 40-44,

KIPINDI CHA UKOMO WA HEDHI(Menopause)

- Wakati Mwanamke anafikia kipindi cha ukomo wa hedhi yaani menopause,anakuwa na takribani ya Mayai chini ya 1,000,

Kadri umri unavyosogea, Mayai ambayo hayajakomaa(Immature eggs) huwa resistant kwa FSH, Na kadri mayai yaliyokomaa hupungua, ndipo Ovaries huaza kuzalisha kiwango kidogo sana cha estrogen and progesterone tofauti na hapo mwanzo.

Hali hii hupelekea ukomo wa hedhi yaani Menopause, ambapo mayai hayatolewi tena kwenye ovaries(stops ovulation).

Na sababu kama vile; Idadi ya mayai ambayo umezaliwa nayo, magonjwa ambayo umeyapata kipindi cha maisha yako, matibabu ambayo umepata ikiwemo dawa n.k huweza kusababisha utofauti wa kipindi cha ukomo wa hedhi(menopause) kati ya mwanamke mmoja na mwingine.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.


0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD