Showing posts with label chakula. Show all posts
Showing posts with label chakula. Show all posts

Faida Za Nanasi Mwilini mwako,Soma hapa kufahamuAfyaclass Forum •

Nanasi ni tunda la kitropiki ambalo huchukua miaka mitatu kukomaa. Nanasi ni tamu, huongeza vitamini na virutubisho mbalimbali kwa afya ya mlaji. Pia hupambana na magonjwa.

Nanasi lina faida mbalimbali za afya, ikiwa ni pamoja na kuboresha usagaji wa chakula, kuondoa hatari ya saratani, na kuondoa maumivu.

Hata hivyo, wale walio na mzio wanapaswa kuepuka matunda haya na wale wanaotumia dawa za kupunguza damu wanapaswa kuwa waangalifu.

Kupambana na magonjwa

Tunda hili lina utajiri mkubwa wa vitamini C na magnishiamu. Vitamini C ni muhimu katika kusaidia kinga ya mwili.

Magnishiamu husaidia kupambana na seli zinazoweza kuleta madhara katika mwili, husaidia kuzuia uvimbe ambao unaweza kusababisha saratani na magonjwa mengine sugu.

Nanasi ni chanzo muhimu cha kupambana na magonjwa. Kutumia nanasi mara kwa mara kunaweza kukupunguzia hatari ya kupata ugonjwa wa moyo na kisukari.

Usagaji wa chakula

Tunda hili lina enzaimu wa kusaidia usagaji chakula waitwao bromelain, ambao husaidia kurahisisha usagaji wa chakula.

Bromelain huvunja molekuli za protini, ikimaanisha utumbo wako mdogo unaweza kuzifyonza kwa urahisi zaidi.

Hilo ni muhimu sana kwa watu walio na upungufu wa maji ya kongosho, hali inayoifanya kongosho kutotengeneza vimeng’enya vya kutosha vya kusaga chakula.

Kwa kuwa lina nyuzinyuzi nyingi, pia husaidia mfumo wa usagaji chakula na kuboresha afya ya vijidudu vyenye faida ambavyo hukaa kwenye utumbo wako.

Uponyaji baada ya kuumia

Tafiti kadhaa zinaonyesha kuwa bromelain ambayo pia inapatikana katika nanasi, husaidia kupunguza uvimbe na michubuko baada ya jeraha au upasuaji.

Nanasi linaweza kuwa muhimu ikiwa utakula kabla ya ung’oaji wa jino, husaidia kupunguza maumivu na kutoa ahueni kama vile dawa ya kuzuia maambukizi.

Utafiti wa taasisi ya Vitro (uliofanywa katika maabara), pia umeonyesha bromelain husaidia katika uponyaji wa jeraha.

Kupunguza maumivu ya viungo

Tatizo la maumivu ya viungo, ni ugonjwa unaohusisha viungo kuvimba, kuwa vyekundu na kuleta maumivu. Ugonjwa huu ni matokeo ya mfumo wa kinga kushambulia tishu zenye afya kimakosa.

Tafiti nyingi, zilizoanzia miaka ya 1960, zimeonyesha jinsi bromelaini inavyoweza kuwa muhimu katika kutuliza maumivu yanayohusiana na viungo.

Maumivu ya viungo huathiri zaidi ya watu wazima milioni 54 huko Marekani. Kuna aina nyingi za ugonjwa wa maumivu ya viungo, lakini mengi ya magonjwa hayo huhusisha kuvimba kwa viungo.

Virutubisho vya bromelaini, husaidia kuondoa maumivu katika sehemu ya chini ya mgongo kama sawa na matibabu ya maumivu.

Kusaidia kinga ya mwili

Utafiti wa wiki tisa wa watoto wa shule ambao walikula kiasi cha wastani cha mananasi kila siku, walikuwa na hatari ndogo sana ya kuambukizwa virusi au bakteria kuliko wale ambao hawakula.

Mbali na hayo, wale waliokula kiasi kikubwa walipata mara nne ya idadi ya seli nyeupe za kinga za kupambana na maambukizi.

Nanasi pia kusaidia kurekebisha mfumo wa kinga, na linaweza kuwa bora kwa wale walio na kinga dhaifu za mwili.

Kusaidia mfumo wa moyo

Kwa mara nyingine tena, ni bromelain ambayo inaonekana kuwa na umuhimu kwa moyo na mfumo wa mzunguko wa damu, kwa kuzuia au kupunguza ukali wa mshtuko wa moyo.

Uchunguzi kwa wanyama unaonyesha bromelain pia huzuia shinikizo la damu, kuganda kwa damu kwa kuzuia utengenezwaji wa protini inayoitwa fibrin ambayo inahusika katika kuganda kwa damu.

Kupunguza hatari ya pumu

Juisi ya nanasi pia inaweza kuwa na ufanisi katika kupunguza dalili zinazohusiana na pumu. Katika utafiti wa wanyama, watafiti waligundua kuwa bromelain zinaweza kuwa na faida kwa watu wanaoishi na pumu.

Zaidi ya hayo, nanasi lina vitamini C, ambavyo hulainisha mirija ya mapafu. Na katika matukio ya mashambulizi ya pumu kutokana na baridi, vitamini C vilikuwa ya manufaa

Nanasi ni salama kwa kila mtu?

Kama huna mzio na nanasi, kwa ujumla inatambulika kuwa nanasi ni salama kwa watu wengi na ni sehemu ya lishe bora.

Hata hivyo, kula au kunywa kiasi kikubwa kunaweza kusababisha shida ya usagaji chakula. Jambo jingine ni kujiepusha kula nanasi ambalo halijaiva kwa sababu, linaweza kusababisha kuhara na kuwasha koo.

Zaidi ya hayo, ikiwa unakabiliwa la asidi ya reflux, nanasi linaweza kuongeza dalili zako. Asidi hiyo inaweza kusababisha kiungulia.

Wale wanaotumia dawa za kupunguza damu wanapaswa kukumbuka kwamba bromelaini iliyo katika nanasi inaweza kuathiri uwezo wa damu kuganda na inapoliwa kwa wingi, na kwa kushirikiana na dawa za kupunguza damu, inaweza kuongeza hatari ya kutokwa na damu.

Licha ya faida zake, ni muhimu kukumbuka kuwa juisi ya mananasi ina nyuzinyuzi kidogo lakini ina sukari nyingi sana.

Hii inamaanisha haitakuwa na uwezo wa kukujaza tumbo lako kama kula nanasi la kawaida la kiwango hicho hicho, lakini inaweza kusababisha uzito kwa baadhi ya watu.

Via:Bbc



0 Comment

Madhara ya nyama nyekunduAfyaclass Forum •

Madhara ya nyama nyekundu

Nyama nyekundu maarufu kama “Red Meat” ni nyama ambayo wataalam wengi wa afya wamekuwa wakiizungumzia hasa kwa upande wa kuleta madhara kwenye afya zetu japo sio kama ina hasara tu bali hata faida zipo(kila kitu chenye faida kina hasara zake pia).

Tafiti mbali mbali za afya hufanyika kila siku kuhusiana na madhara ya nyama nyekundu yaani Red Meat kwenye afya ya Mwili wa Binadamu, na katika makala hii tumechambua baadhi ya madhara katika tafiti mbali mbali za afya kuhusu madhara ya nyama nyekundu,

MADHARA YA KULA NYAMA NYEKUNDU NI PAMOJA NA;

– Nyama nyekundu(Red Meat) huchangia mtu kupatwa na magonjwa mbali mbali ya moyo ikiwa ni pamoja na tatizo la mishipa ya damu ndani ya moyo kuziba,

hii ni kwa sababu ya kuwepo kwa kiwango kikubwa cha mafuta yaani SATURATED FAT na matokeo yake ni kuwa na kiwango kikubwa cha Cholestrol(Lehemu) mwilini, Cholestrol nyingi mwilini ni mojawapo ya vihatarishi vikubwa vya magonjwa mbali mbali ikiwemo magonjwa ya moyo

– Nyama nyekundu(Red Meat) huongeza uwezekano wa mtu kupatwa na tatizo la  saratani au Kansa ya Tumbo,

– Pia kuna utafiti ambao umefanywa na Taasisi ya Afya ya Taifa nchini Marekani, umebaini kwamba asilimia kubwa ya watu wanaopenda kula nyama nyekundu yaani Red Meat kwa kiasi kikubwa kwenye maisha yao, hufariki mapema zaidi kuliko wale wanaokula kiasi kidogo cha nyama hiyo.

JE NYAMA YA NGURUWE NI NYAMA NYEKUNDU?

Swali hili watu wengi wameniuliza sana, kwani nyama ya Nguruwe ukiiangalia sio nyekundu ni nyeupe, je nayo ipo kwenye kundi la nyama nyekundu?

Ukweli ni kwamba hata nyama ya nguruwe ipo kwenye kundi la Nyama nyekundu hata kama kwa muonekano wa nje ni nyeupe, soma hii hapa,

Kutokana na utafiti wa Wizara ya Kilimo ya nchini Marekani, kiwango cha protini aina ya ‘myoglobin’ kilichomo kwenye misuli ya nyama yoyote ndicho kinachoonesha aina ya nyama,

Hivo basi,Nyama ya nguruwe inawekwa kwenye kundi la nyama nyekundu yaani Red Meat kutokana na uwepo wa kiwango kikubwa cha protein aina ya ‘myoglobin’ kuliko kile kilichomo kwenye nyama nyeupe za kuku na samaki.

Hivo unashauriwa kupunguza sana ulaji wa nyama nyekundu yaani Red Meat,kwa sababu matumizi ya kiwango kikubwa cha nyama nyekundu sio salama kwa afya yako.

Lakini pia mbali na ulaji wa nyama nyekundu,wataalam wa afya hushauri kuepuka kula nyama zenye mafuta mengi,kwani mafuta haya huweza kuwa chanzo cha magonjwa mbali mbali mwilini kama vile magonjwa ya moyo n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Madhara ya nyama nyekundu
0 Comment

kukosa ladha ya chakula mdomoniAfyaclass Forum •

kukosa ladha ya chakula mdomoni

Kukosa ladha ya chakula mdomoni ni tatizo ambalo kwa kitaalam hujulikana kama Ageusia, ikiwa na maana Loss of Sense of Taste.

Tatizo hili huweza kusababishwa na sababu mbali mbali ikiwemo;

  • Maambukizi ya magonjwa
  • Baadhi ya Dawa
  • Tatizo la Lishe,Upungufu wa virutubisho mwilini au nutritional deficiencies
  • Pamoja na Sababu Zingine

Pia,Kwa baadhi ya Watu,inaweza kuwa dalili kwa Mtu mwenye COVID-19. Na asilimia kubwa,kutibu chanzo husika cha tatizo hili huweza kukurudisha kwenye hali yako ya kawaida.

Kukosa ladha ya chakula mdomoni au tatizo la Ageusia huweza kusababisha iwe Vigumu kwa Mtu Kujua ladha mbali mbali za vitu yaani ladha kama vile;

  1. Tamu| sweet,
  2. Chachu|sour,
  3. Chumvi|salty 
  4. Au Chungu|bitter.

Kukosa ladha ya chakula mdomoni ni tatizo ambalo huweza kumpata Mtu yeyote,wa umri wowote, ingawa hutokea Zaidi ikiwa umri wako ni mkubwa,mfano Zaidi ya Miaka 50.

Tatizo hili sio Kubwa Sana, na baadhi ya tafiti zinaonyesha, Kati ya Watu 1,000, mtu 1 au 2 wanaweza kuwa na tatizo hili la Kukosa ladha ya chakula mdomoni.

Dalili Za Tatizo la Kukosa ladha ya chakula mdomoni

Dalili kubwa ni Mtu kushindwa kutofautisha ladha ya chakula chochote anachokula, Lakini pia unaweza kupata dalili Zingine ikiwemo;

– Kukosa Hamu ya Kula

– Shinikizo la Damu kuwa Juu

– Shida ya Pua Kuziba

– Kupata shida ya Kupumua n.k

Chanzo cha tatizo la Kukosa ladha ya chakula mdomoni

Zipo Sababu nyingi ambazo huweza kuchangia hali hii, na baadhi ya Sababu hizo ni Pamoja na;

  • Maambukizi ya magonjwa kama Vile COVID-19 n.k
  • Maambukizi au Sinus infection (sinusitis)
  • Tatizo la Mafua
  • Tatizo la Pharyngitis (sore throat).
  • Strep throat.
  • Maambukizi kwenye tezi la Mate au Salivary gland infections.
  • Magonjwa ya meno au Fizi,Gum (periodontal) disease.
  • Kuumia kichwani au kwenye Masikio n.k,(Injuries to your head or ear).

Pia,tatizo la Kukosa ladha ya chakula mdomoni huweza kuhusishwa na matatizo mengine ya Kiafya kama vile;

1. Tatizo la Unene au Uzito kupita kiasi(Obesity/overweight)

2. Ugonjwa wa Kisukari

3. Uvutaji wa Sigara

4. Lishe duni au Poor nutrition.

5. Matatizo kama vile Sjogren’s syndrome,Shinikizo la Juu la Damu

6. Upungufu wa Virutubisho mwilini kama vile zinc pamoja na vitamin B-12.

7. Tatizo la Mdomo mkavu Dry mouth (xerostomia)

8. Magonjwa kama vile Alzheimer’s disease,Parkinson’s disease,Multiple sclerosis (MS).n.k

9. Matumizi ya baadhi ya Dawa kama vile lithium, dawa za kutibu Saratani,dawa za tezi la thyroid n.k

Tatizo hili hukaa kwa Muda Gani?

Ageusia inaweza kudumu kwa muda gani?
Inategemea. Kwa kawaida, dalili zinaendelea hadi hali ya msingi itatibiwa. Watu ambao wana ageusia kama dalili ya COVID-19 kawaida hupona baada ya wiki moja hadi tatu. (Kumbuka: Watu wengi ambao huendeleza ageusia kama dalili ya coronavirus pia wana anosmia – kupoteza hisia.)

Vipimo vya tatizo la Kukosa ladha ya chakula mdomoni

Matatizo ya ladha kama vile ageusia kwa kawaida hutambuliwa na mtaalamu wa masikio, pua na koo (ENT). Watakuuliza maswali kuhusu dalili zako na kukagua historia yako ya afya ili kubaini ikiwa hali zozote zilizopo zinaweza kusababisha upotevu wako wa ladha.

Matibabu ya tatizo la Kukosa ladha ya chakula mdomoni

Ndiyo. Katika hali nyingi, kutibu hali ya msingi ambayo imesababisha ageusia husaidia kurejesha uwezo wako wa ladha ya chakula Mdomoni.

Ni mara ngapi baada ya matibabu nitajisikia vizuri?

Inategemea kile kilichosababisha tatizo la kukosa ladha mdomoni. Ikiwa mzio, baridi au homa ilisababisha ageusia, ladha yako inaweza kurudi baada ya kutumia dawa jamii ya antihistamines au decongestants.n.k

Maambukizi yanaweza kutibiwa na dawa jamii ya antibiotics. Mtoa huduma wako wa afya anaweza kukusaidia kuamua ni hatua gani ya kuchukua. Mara tu unapopona ugonjwa wako, hisia zako za ladha zitarudi.

Wakati mwingine, ageusia inaweza kutatuliwa kwa kuboresha tabia yako ya maisha. Kwa mfano, watu wanaoacha kuvuta sigara wanaweza kurejesha hisia zao za ladha katika muda wa saa 48. Ikiwa ageusia yako inahusiana na ugonjwa wa fizi, kuhakikisha usafi wa kinywa kunaweza kusaidia kurejesha utendakazi wako wa ladha haraka.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO HILI,TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

kukosa ladha ya chakula mdomoni
0 Comment

Maini, figo chanzo kikuu cha viinilishe mwiliniAfyaclass Forum •

Maini, figo chanzo kikuu cha viinilishe mwilini

By DK. SHITA SAMWEL

Upo uvumi wa miaka mingi duniani kuhusu ulaji maini na figo za ng’ombe, mbuzi na kuku kuwa una madhara kutokana na ogani hizo kufanya kazi ya kuondoa sumu mwilini.

Kiujumla minofu ya nyama ya wanyama wanaoliwa ni moja ya vyakula ambavyo huwa na virutubisho mbalimbali, ikiwamo protini nyingi, iliyo muhimu kwa afya zetu.

Katika nyama hiyo, moja ya sehemu ambazo zina virutubisho vingi zaidi kuliko unavyoweza kupata katika minofu ni ogani ya ini. Sehemu hii ina protini nyingi zaidi kuliko ile inayopatikana katika minofu.

Ini ni ogani kubwa kuliko nyingine ndani ya tumbo, lina kazi kubwa na muhimu katika mwili, ikiwamo kuvunjavunja na kuchakata sumu, kemikali na dawa zenye usumu.

Vitu hivyo bila kuchakatwa na ini vikiingia katika mfumo wa damu na kusambaa maeneo mbalimbali ya mwili moja kwa moja zinaweza kudhuru.

Hapa unapata picha kuwa ini inafanya kazi hiyo tu, halifanyi kazi ya kuzihifadhi sumu hizo. Kazi hiyo ambayo kitabibu hujulikana kama detoxication.

Ikiwa utakula kitu chenye sumu au hata dawa lazima itapita katika ini, itavunjwa vunjwa hatimaye kufifishwa au kuondolewa sumu, aidha kwa kubadilishwa kuwa katika hali isiyo na madhara.

Baadaye baada ya uchakataji huo huweza kufika katika figo, ambazo zenyewe huchuja damu na kuondoa takasumu na mabaki yasiyohitajika mwilini kwa njia ya mkojo.

Figo nayo ina kazi nyingi, lakini kazi kuu mbili huwa ni kuondoa takasumu mwilini na kuweka usawa wa maji na madini.

Mkojo unaotengenezwa na figo ni salama, ambao huhifadhiwa katika kibofu mpaka pale mwili utakapohisi haja. Mkojo umebeba sumu za urea na nyingine zinazokuwa sumu endapo tu zitabaki ndani ya mwili kwa kiwango kikubwa.

Na wenyewe siyo sumu unapokuwa nje ya mwili. Kwa hiyo ile imani potofu ambayo unaweza kuikuta mtaani au mitandaoni kuwa ulaji wa maini na figo si sahihi, hawana ufahamu wa kina juu ya kazi za ini na figo kisayansi.

Kama ini na figo zingekuwa zinahifadhi sumu, ina maana kuwa ulaji wake ungelikuwa si salama. Maana makali ya sumu hizo yangekuwa palepale na ingeliweza kumdhuru yule atakayekula ogani hizi.

Ini huwa na kazi nyingi mwilini, ikiwamo kuhifadhi viini lishe, uundwaji wa protini, kudhibiti sukari ya mwili, kudhibiti joto la mwili, kuzalisha nyongo ambayo inahusika kusaga vyakula vya mafuta.

Kutokana na kazi zake, ndiyo maana huwa limesheheni virutubisho vingi vyenye faida kubwa kiafya kwa mlaji, ikiwamo madini kama kopa, chuma, patasiamu na vitamini kama A, B na D.

Protini inayopatikana katika ini huwa ni nyingi, ikiwa katika ubora wa juu ukilinganisha na ile ya minofu.

Kwa upande wa madaktari wa mifugo, wanashauri kutokula mnyama mgonjwa au ambaye amekula kitu na kumfanya aumwe.

Ndiyo maana inashauriwa kula nyama ambayo imekaguliwa na mabwana afya, ambazo ndizo zinazouzwa katika masoko ya nyama au machinjio maalumu.

Ulaji wa figo na maini ni salama kwa sababu zinavunja vunja, kufifisha sumu na hatimaye kuziondoa mwilini. Ogani hizi hazihifadhi sumu yoyote mwilini. Ni salama kuliwa na ni chanzo kikubwa cha viinilishe.

 

Maini, figo chanzo kikuu cha viinilishe mwilini
0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD