Showing posts with label chanjo ya rubella. Show all posts
Showing posts with label chanjo ya rubella. Show all posts

Kampeni ya chanjo Kitaifa dhidi ya Surua/rubella kuanza Februari 15 hadi18, 2024Afyaclass Forum •

Kampeni ya chanjo Kitaifa dhidi ya Surua/rubella kuanza Februari 15, 2024  hadi Februari 18, 2024.

Watoto zaidi ya milioni 8 nchini kupatiwa chanjo ya surua na rubella

Serikali kupitia Wizara ya Afya imezindua kampeni ya Kitaifa ya Chanjo ya Surua na Rubella ambapo kwa nchi nzima wanatarajia kuwafikia watoto 8,908,810 wenye umri chini ya miaka mitano.

Hayo yamebainishwa Leo Jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Kinga kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Tumaini Haonga akimuwakilisha Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu katika uzinduzi wa kampeni ya chanjo Kitaifa Februari 15, 2024 katika maeneo mbalimbali nchini na inatarajiwa kumalizika Jumapili Februari 18, 2024.

Dkt. Haonga amesema kuwa lengo la kampeni hii ni kuhakikisha wanazuia kuenea kwa ugonjwa surua na rubella pamoja na kuongeza kinga kwa walengwa.

Dkt. Haonga amesisitiza usimamizi wa chanjo hiyo kutokana na umuhimu wake kwani inaongeza kinga kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano.

Ameongeza kuwa zaidi ya vituo 7,373 katika maeneo mbalimbali nchini vimetengwa kwa ajili ya kuhakikisha wanatoa Huduma hiyo kikamilifu ili kuweza kufikia lengo waliojiwekea..

Hata hivyo amewataka Wakuu wa Mikoa,Wilaya na Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha wanasimamia kikamilifu zoezi kuwapatia chanjo watoto wenye umri kuanzia miezi tisa mpaka 59 (chini ya miaka mitano)

“Niwaombe wazazi kuitumia fursa hii kuwapeleka watoto wao waweze kupatiwa chanjo kwani ni muhimu kwa watoto kupata chanjo hiyo,”ametoa wito Dkt. Haonga.

Dkt. Haonga amesema wamepata mrejesho tangu kuanza kwa chanjo kwa zoezi hilo katika maeneo mbalimbali wazazi wamejitokeza kwa wingi na wanaendelea kujitokeza ili kulinda afya za watoto wao.

Via:WAF, Dodoma

>>Soma zaidi kuhusu ugonjwa wa Surua hapa

Kampeni ya chanjo Kitaifa dhidi ya Surua/rubella kuanza Februari 15
hadi18, 2024
0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD