Showing posts with label hali ya joto kali. Show all posts
Showing posts with label hali ya joto kali. Show all posts

Ripoti Mpya;Ongezeko la Joto Duniani lisilolakawaidaAfyaclass Forum •

Kulingana na ripoti mpya iliyotolewa na Huduma ya Mabadiliko ya Tabia nchi ya Muungano wa Ulaya ya Copernicus, wastani wa hali joto duniani umekuwa juu ya nyuzi joto 1.5 za Selsiasi kwa miezi 12 mfululizo jambo ambalo si la kawaida na mara ya mwisho kushuhudia hali kama hii ilikuwa mwaka 2015/2018.

Data za Huduma ya Mabadiliko ya Tabia nchi ya Muungano wa Ulaya, Copernicus ERA5, zinaonesha kwamba mwezi juni ulikuwa na nyuzi joto 1.50 za Selsiasi juu ya makadirio ya awali ya Mwezi Juni kwa mwaka 1850 – 1900 wakati wa mapinduzi ya viwanda ikiwa huu ni mwezi wa 12 mfululizo hali joto kuvuka nyuzi joto 1.5.

“Takwimu hizi za hivi karibuni  kutoka kwa Huduma ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa ya Copernicus kwa bahati mbaya zinaangazia kwamba tutakuwa tukizidi kiwango cha nyuzijoto 1.5 za selsiasi kwa muda na kuongezeka kwa marudio, kila mwezi. Hata hivyo, ni muhimu kusisitiza kwamba ukiukaji wa muda mfupi haumaanishi kuwa lengo la 1.5 °C litapotea kabisa kwa sababu hii inahusu ongezeko la joto la muda mrefu kwa angalau miongo miwili,” Anasema Katibu Mkuu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) Celeste Saulo.

Katika mkataba wa Paris, nchi zilikubaliana kuweka wastani wa halijoto wa muda mrefu  kuwa ni chini ya nyuzi joto 2 kabla ya kuanza kwa viwanda na baadae wakaweka kikomo hadi nyuzi joto 1.5 kufikia mwisho wa karne hii, huku wanasayansi wameonya mara kwa mara kwamba ongezeko la joto la zaidi ya nyuzi joto 1.5 linasababisha athari mbaya zaidi za mabadiliko ya tabianchi.

Hata, Katika viwango vya sasa vya ongezeko la joto duniani, tayari kuna athari mbaya za hali ya hewa ambazo ni Pamoja na joto kali, mvua kali na ukame, barafu ya bahari, kuongeza kasi ya kupanda kwa kina cha bahari na joto la bahari.

“Juni ilishuhudiwa kuenea na kuongezeka kwa joto kwa muda mrefu katika nchi nyingi, na athari kubwa katika nyanja zote za maisha ya watu. Hii ilikuwa hata kabla ya kilele cha jadi cha majira ya joto ya kaskazini mwa ulimwengu, ambayo bila shaka itaona joto kali zaidi. Halijoto iliyorekodiwa kwenye uso wa bahari inatia wasiwasi mkubwa kwa mifumo ya ikolojia ya baharini na pia inatoa nishati kwa vimbunga vya kitropiki vinavyoshangaza zaidi – kama tulivyoona kwenye Kimbunga Beryl,” Amesema Celeste Saulo.

WMO hutumia hifadhi data sita za kimataifa, ikiwa ni pamoja na ERA5, kwa hali yake ya ufuatiliaji wa tabianchi. Ni muhimu kutambua kwamba hifadhi data nyingine huenda zisithibitishe mfululizo wa miezi 12 ulioangaziwa na Huduma ya Mabadiliko ya Tabianchi ya Copernicus, kutokana na ukingo mdogo zaidi ya nyuzi joto 1.5 ya viwango vya joto duniani ERA5 kwa Julai na Agosti 2023 na Mei na Juni 2024.

Mkurugenzi wa Huduma ya Mabadiliko ya Tabianchi ya Copernicus, Carlo Buontempo anatoa tahadhari kwamba hata kama hali hii ya kuongeza kwa hali joto itaisha kwa wakati Fulani, lakini kuna uwezekano mkubwa wa jambo hili kujirudia tena, hivyo dunia inapaswa kuangalia namna ya kuacha kuongeza hewa chafu kwenye ang ana bahari ili kuepukana na athari za baadae endapo jambo hili litajirudia tena.

Ripoti Mpya;Ongezeko la Joto Duniani lisilolakawaida
0 Comment

Mahujaji 14 wa Hajj kufariki dunia kisa joto kaliAfyaclass Forum •

Mahujaji 14 wa Hajj kufariki dunia kisa joto kali

Takriban raia 14 wa Jordan wamefariki dunia wakati wa ibada ya Hijja nchini Saudi Arabia kutokana na joto kali, maafisa wamesema.

Wizara ya mambo ya nje ya Jordan ilisema raia wake 14 wamefariki “baada ya kupigwa na jua sana kutokana na wimbi la joto kali” na wengine 17 wameripotiwa kupotea.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, Shirika la Red Crescent la Iran limethibitisha kuwa mahujaji watano wa Iran pia wamepoteza maisha, lakini haikueleza jinsi walivyofariki.

Maafisa wa Jordan walisema msako unaendelea kuwatafuta waliotoweka.

Katika taarifa yake wizara ya mambo ya nje ya Jordan ilisema kuwa inawasiliana na mamlaka ya Saudia kuhusu taratibu za kuzika au kusafirisha miili ya marehemu, kulingana na matakwa ya familia zao.

Hajj ni moja ya mikusanyiko mikubwa ya watu duniani ambapo zaidi ya mahujaji milioni 1.8 wanashiriki hijja mwaka huu, kulingana na maafisa wa Saudi.

Lakini ina historia ya majanga makubwa ikiwa ni pamoja na mikanyagano na moto wa mahema. Lakini kwa miaka mingi, changamoto kuu hutokana na joto kali.

Halijoto wiki hii ilizidi 46C (114.8F) na kufanya tamaduni nyingi zinazofanywa nje na kwa miguu kuwa na changamoto hasa kwa wazee

Via:Bbc

Mahujaji 14 wa Hajj kufariki dunia kisa joto kali
0 Comment

Zaidi ya watu 50 wamefariki dunia India kwa siku tatu zilizopita kutokana na hali ya joto kaliAfyaclass Forum •

Zaidi ya watu 50 wamefariki dunia India kwa siku tatu zilizopita kutokana na hali ya joto kali

Zaidi ya watu 50 wamefariki dunia nchini India katika muda wa siku tatu zilizopita huku hali ya joto kali ikiendelea kukumba sehemu za nchi hiyo.

Takriban watu 33 walikufa katika jimbo la kaskazini la Uttar Pradesh mwishoni mwa juma kutokana na joto.

Katika jimbo la Odisha (Orissa), takriban watu 20 walikufa kutokanana wimbi kali la joto, afisa aliliambia shirika la habari la ANI.

Vingi vya vifo hivi viliripotiwa tarehe 1 Juni wakati India ilipopiga kura katika awamu ya mwisho ya upigaji kura kwa uchaguzi wake mkuu.

Matokeo ya uchaguzi huo yamepangwa kutangazwa tarehe 4 Juni.

Kila baada ya miaka mitano, India hufanya uchaguzi wake mkuu katika miezi ya kiangazi ya Aprili na Mei.

Lakini mwaka huu, hali ya joto imekuwa ikivunja rekodi, huku nchi ikikumbwa na mawimbi ya joto ya mara kwa mara, makali zaidi na marefu zaidi.

Wizara ya afya ya serikali kuu inasema kwamba kumekuwa na vifo 56 vilivyothibitishwa vya mawimbi ya joto kutoka 1 Machi hadi 30 Mei. Karibu visa 24,849 mawimbi ya joto viliripotiwa katika kipindi hicho.

Zaidi ya watu 50 wamefariki dunia India kwa siku tatu zilizopita
kutokana na hali ya joto kali
0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD